Mpenzi wangu kagegedwa nampenda nifanyeje?

Mpenzi wangu kagegedwa nampenda nifanyeje?

MSHINO

JF-Expert Member
Joined
Jul 26, 2013
Posts
1,069
Reaction score
713
Wana jamii naombeni ushauri wenu kijana mwezenu yamenikuta, mimi nina girlfriend tangu mwaka jana, nimekuwa nikimpa support ya shule kama ada na mahitaji mengine kadri ninavyoweza. Mwaka jana aliombwa na dada yake akampe campani huko mbagara kwaani alikuwa amepata mtoto mchanga. Tangu aende kuishi kwa dada yake alianza kubadirika katika mawasiliano, aliniambia kuwa hakuwa free kama alipokuwa kwa wazazi wake temeke. Kwaani kila nikimhitaji ilkuwa ni ngumu au kwa nadra sana mfano tuliweza kuonana mara moja kila baada ya miezi 1-2. Mawasiliano yetu makubwa yalikuwa ya simu. Kwa sababu ya mawasilano yetu kuwa finyu tuliweza kutofautiana mara kwa mara hivyo hata ile support yangu ikawa inapungua kwa sababu ilikuwa ni lazima niende kwenye tigopesa kumuwezesha nayopia ilitegemea nimepata muda gani kulingana na mazingira ya kazi yangu.

Bahati nzuri mpenzi wangu amerudi nyumbani kwa wazazi sasa yapata mwezi mmoja na tunaweza kuonana mara kwa mara na mahusiano yetu yamestawi vizuri tena. Kwa bahati mbaya juzi siku ya Eid simu yangu nilimwazima mdogo wangu alikuwa amepoteza simu yake huku akiwa na issue ya pesa. Hivyo mpenzi wangu hakuweza kunipata alichukia sana mpaka akawa hapigi simu wala hajibu sms zangu kwa muda wa siku 3. Ijumatatu wiki hii baada ya kazi nilienda kujua kulikoni, aliponiona tu aliniambia nimefuata nini? Nilimshangaa sana, akasema kuwa najifanya sijui kwa nini sikupokea simu yake siku ya Eid. Nilimwelewesha na kumwomba msamaha. Baadae nilimuuliza kuwa nilikuwa nimeona gari pale nyumbani kwao na nikajifanya kama nimepata taarifa kuwa ni ya mtu wake, alinijibu kuwa kwa hiyo nina amuaje? Niliamua kuchukua simu yake kwa nguvu nikaondoka nayo. Usiku iliingia sms iliyokuwa inamtaka wakafanye mapenzi kwaani ilikuwa yapata miezi 4 tangu wafanye mara ya mwisho. Sikuamini nilichokiona. Jana jioni nilienda kukutana nae na kumuuliza kuhusu sms hiyo alilia na kuomba nimsamehe kwani alifanya mara moja kwa kuwa hatukuwa na mawasiliano mazuri kipindi hicho akiwa Mbagara eti alihisi tulikuwa tumeachana na alikuwa na shida ya shule hivyo ilimbidi kumkubari mtu bila kupenda. Zaidi aliniambia kuwa mbona yeye alinisamehe mwaka jana alipopata uja uzito tukautoa hata bila ya wazazi wake au dada yake kujua? Ni kweli tulitoa mimba ya mwezi 1.5. Lakini tulishauliana kuwa asome kwanza hayo mengine ndiyo yafuate. Akakubari.

Wana jamii naombeni ushauri wenu nifanyeje kijana mwenzenu yamenikuta na binti nampenda lakini kwa sababu ya hili la kutokuwa mwaminifu nimemwambia kuwa tangu jana tumeachana, kiukweli usiku kucha sijapata usingizi hata dk 5. Hapa nilipo nawaza sana. Na yeye ananiomba msamaha hatarudia ilitokea bahati mbaya.
 
Mtu yeyote fa'la fa'la anayesema MBAGARA badala ya MBAGALA na MALA MWISHO badala ya MARA YA MWISHO lazima demu wake agegedwe.

Ulishindwa nini kumwambia huyo mayala kuwa unampa simu mdogo wako kwa hiyo hutakuwa hewani? Halafu usiishi kwa hisia bwana mdogo, aliyegegedwa ni demu wako na wewe ndio una maumivu, ushauri wa watu wengine hautaondoa mbegu mwilini mwa huyo mayala.

Jifunze lugha fasaha uje Mbezi nikupatie demu wa maana.
 
Pole sana! sasa kama umemwambia toka jana kuwa mmeachana unataka ushauri gani? Ni makosa makubwa siku za holiday kama EID, Christmass, Pasaka n.k.....kutopokea simu ya mpenzi wako hata kama ungekuwa wewe ungefikiriaje? nahisi kama siku hiyo ulikuwa na mambo fulani hivi ila umeona utoe sababu ambayo haijitoshelezi. Is up to u coz naona hata usiku hujalala.
 
Tatizo una mapenzi ya kitoto mapenzi ya kulialia hadi kwenye keyboard. Hivi mko kidato cha ngapi maana mnaonekana wote bado wanafunzi. Mimi hata mke wangu akigegedwa nampiga chini hiyo ndio principle yangu hata yeye anajua. Uache mapenzi ya kulialia
 
Mabwege wamezidi jamani.......!!!khaa...jitu linauliza kama toto dogo kabisa...nya.mba.f
 
Mpenzi wako anagegedwa? Afu unampenda? Ha ha ha ha ha ha ha ha
Mapenzi ni kitendawili
 
Pole sana! sasa kama umemwambia toka jana kuwa mmeachana unataka ushauri gani? Ni makosa makubwa siku za holiday kama EID, Christmass, Pasaka n.k.....kutopokea simu ya mpenzi wako hata kama ungekuwa wewe ungefikiriaje? nahisi kama siku hiyo ulikuwa na mambo fulani hivi ila umeona utoe sababu ambayo haijitoshelezi. Is up to u coz naona hata usiku hujalala.

Hayo mapenzi ni ya kizamani sana na kama utumwa eti mtu anune kisa sitapokea cmu upuuzi mtupu
 
Pole lakini sio sana, ivi ingekua yeye ndio amefanya hivyo na siku kama hiyo ungekua na mawazo gani? au wewe unajua kama cm hutokua nayo kwanini hamkumalizana kwenye cm kama tukutane wapi au nakuja nyumbani au chochote au hata vibandani ulishindwa kwenda kuongea nae? ebu sema ukweli ulikua wapi,na umeona sms umeshindwa kulala unageona live?
kufa unataka kuzimia unaogopa ushamwambia basi umeshaachana nae sasa unakosa usingizi wa nini...
 
Mpenzi wako anagegedwa? Afu unampenda? Ha ha ha ha ha ha ha ha
Mapenzi ni kitendawili

Analeta mambo ya shetta na diamond ya nidanganye danganye tu hata akimkuta utupu amekumbatiwa kisa unampenda
 
Umesahau Ijumatatu badala ya Jumatatu

Mtu yeyote fa'la fa'la anayesema MBAGARA badala ya MBAGALA na MALA MWISHO badala ya MARA YA MWISHO lazima demu wake agegedwe.

Ulishindwa nini kumwambia huyo mayala kuwa unampa simu mdogo wako kwa hiyo hutakuwa hewani? Halafu usiishi kwa hisia bwana mdogo, aliyegegedwa ni demu wako na wewe ndio una maumivu, ushauri wa watu wengine hautaondoa mbegu mwilini mwa huyo mayala.

Jifunze lugha fasaha uje Mbezi nikupatie demu wa maana.
 
aksanteni kwa ushuri wenu, Lugha ndugu yangu ni janga tumeathiuliwa na lugha za nyumbani km ungelijua hilo usingesema hayo, turudi kwenye mada, ni sawa EID simu alikuwa nayo dogo, sina la kuficha hapa natafuta ushauri. lakini aligegedwa tangu mwezi 4 siyo juzi siku ya EID, na juzi niliomba msamaha kwa makosa yangu ya simu. ni sawa ni uamzi wangu kuamua kusimamia nililosema jana, lakini pia kupata mawazom katika jamii au kwa marafiki siyo mbaya, huu ni sawa na ushauri nasaha.
 
Wote mna matatizo......!jirekebisheni muanze upya,kama bado unampenda.
 
Unampenda sawa...
Una wivu sawa....
Utoto nao sawa.....

Mapenzi sio kihivyo ....

1.Usichunguze bata kala nini hata siku moja hutamla...inaitwa simu ya kiganjani ni mali ya mtu kwanini usome msg zake....

2.Mawasiliano ni moja ya nguzo za mapenzi ...fikiria angefanya hivyo yeye wewe ungejisikiaje...

3.Uongo unatakiwa kwenye mapenzi ila uwe na mantiki...umempa simu mdogo wako atumie ulishindwa kumwambia ampe taarifa shemejiye au wewe ulishindwa kutoa taarifa....

4.Acha mambo ya kusadikika maana Hisia mbaya nazo huvunja uhusiano

5.Distance love....mara nyingi linatakiwa kukuza mapenzi sio kuvunja

6.Kujiamini...Siku zote amini wewe ndio mpenzi pekee kwake usitake kuweka viulizo .....ziba masikio kwa maana nyingine
 
Binti wa uswahilini lazima awe na vidumu,ni kawaida hiyo mkuu!hata ukimuoa ataliwa tuu
 
Pole lakini sio sana, ivi ingekua yeye ndio amefanya hivyo na siku kama hiyo ungekua na mawazo gani? au wewe unajua kama cm hutokua nayo kwanini hamkumalizana kwenye cm kama tukutane wapi au nakuja nyumbani au chochote au hata vibandani ulishindwa kwenda kuongea nae? ebu sema ukweli ulikua wapi,na umeona sms umeshindwa kulala unageona live?
kufa unataka kuzimia unaogopa ushamwambia basi umeshaachana nae sasa unakosa usingizi wa nini...

swala la simu tulisolve kugegedwa ni tangu april siyo siku ya EID.
 
Mtu yeyote fa'la fa'la anayesema MBAGARA badala ya MBAGALA na MALA MWISHO badala ya MARA YA MWISHO lazima demu wake agegedwe.

Ulishindwa nini kumwambia huyo mayala kuwa unampa simu mdogo wako kwa hiyo hutakuwa hewani? Halafu usiishi kwa hisia bwana mdogo, aliyegegedwa ni demu wako na wewe ndio una maumivu, ushauri wa watu wengine hautaondoa mbegu mwilini mwa huyo mayala.

Jifunze lugha fasaha uje Mbezi nikupatie demu wa maana.

Huyo ni kijana wa bongo fleva tena standard 7 failure.....muonee huruma unga unamsumbua tu.
 
Back
Top Bottom