Mpenzi wangu hanipi muda lakini yupo online muda wote

Kuna kitu kinaniumiza sana kwenye mahusiano yangu, lakini sijui kama mimi ndiye ninayefikiria sana au kweli kuna tatizo.

Mpenzi wangu siku hizi hanipi muda kabisa. Nikimpigia simu mara nyingi anasema yupo busy. Nikimtumia ujumbe anaweza kunijibu baada ya muda mrefu sana, wakati mwingine hata siku nzima inapita bila kuongea naye vizuri.

Kinachonichanganya zaidi ni kwamba nikifungua WhatsApp namkuta online. Anaonekana kupost status, kuangalia status za watu na wakati mwingine anaonekana kwenye mitandao kwa muda mrefu.

Nikijiuliza, kama ana muda wa kuwa online, kwa nini hana hata dakika chache za kuongea na mimi?

Nimejaribu kumuuliza kama kuna tatizo au kama amechoka na mimi, lakini ananiambia sina sababu ya kuwa na mashaka na kwamba ana mambo mengi ya kufanya.

Lakini ukweli ni kwamba nimeanza kujisikia kama sina umuhimu tena kwake.

Kitu kinachoniumiza zaidi ni kwamba zamani alikuwa mtu wa kunitafuta. Angeuliza nimeamkaje, nimefika salama au siku yangu imekwendaje. Sasa mimi ndiye ninayelazimika kuanzisha mazungumzo karibu kila mara.

Sijui kama mapenzi yamepungua au labda nimekuwa nikimlazimisha mtu ambaye tayari ameshaanza kuniacha moyoni.

Nimefika mahali najiuliza kama niache kumtafuta kabisa nione kama atanisikia au atanitafuta mwenyewe.

Kama ungekuwa kwenye nafasi yangu, ungefanya nini? Ungeendelea kumtafuta, ungekaa kimya mpaka yeye akufuate, au ungeamua kuachana?

View attachment 3654176
jifunze kumuacha ukiweza muache.hilo penzi litakutesa
 
Aisee
 
Tatizo ni consistency

Mimi mwanzo kabisa wa mahusiano huwa sianzishi kitu ambacho najua sitoweza kukiendeleza.

kupigiana sana simu na sms nyingi mwanzoni. Kutumiana hela ovyoovyo ndo inabidi iwe hivyo siku zote maana umemzoesha. ukija kuacha au kupunguza tayari anawaza umebadilika

so mimi mwanzoni tu naweza kuchat leo muda mrefu halafu siku zinazofuata ni mara moja moja tu, kwahyo mtu anaelewa mapema kuwa toka mwanzo nilikuwa hivyo.

Pesa ndo kabisaa "sina hata mia" zinakuwa nyingi, nampa kwa mda mda so anakuwa hana 100% ya kupata pesa kwangu

hakuna cha kuwa busy, hiyo ndo tabia yake halisi ameshindwa kuwa na consistency ya tabia fake
 
Jina tu la halima ni wabinafsi sana wanapenda husto za kijinga sana, wanajiona wao ni malaika full kuwalaumu wenzao ila wao wanajiona wako sawa

Wewe si umekosa attention njoo kwangu

Nikugalagaze kiherehere kiishe
 
Kwahiyo mleta mada wakati anaomba msaada kuhusu mpenzi wake kutompa muda, nyie ndo mkapata muda wa kupenzika hapo hapo 😆, hii dunia kweli haipo fair
Mtoto anataka muda tu na mapenzi basi
 
  • Fire
Reactions: ---
Back
Top Bottom