Mpenzi wangu hanipi muda lakini yupo online muda wote

Mpenzi wangu hanipi muda lakini yupo online muda wote

Kuna kitu kinaniumiza sana kwenye mahusiano yangu, lakini sijui kama mimi ndiye ninayefikiria sana au kweli kuna tatizo.

Mpenzi wangu siku hizi hanipi muda kabisa. Nikimpigia simu mara nyingi anasema yupo busy. Nikimtumia ujumbe anaweza kunijibu baada ya muda mrefu sana, wakati mwingine hata siku nzima inapita bila kuongea naye vizuri.

Kinachonichanganya zaidi ni kwamba nikifungua WhatsApp namkuta online. Anaonekana kupost status, kuangalia status za watu na wakati mwingine anaonekana kwenye mitandao kwa muda mrefu.

Nikijiuliza, kama ana muda wa kuwa online, kwa nini hana hata dakika chache za kuongea na mimi?

Nimejaribu kumuuliza kama kuna tatizo au kama amechoka na mimi, lakini ananiambia sina sababu ya kuwa na mashaka na kwamba ana mambo mengi ya kufanya.

Lakini ukweli ni kwamba nimeanza kujisikia kama sina umuhimu tena kwake.

Kitu kinachoniumiza zaidi ni kwamba zamani alikuwa mtu wa kunitafuta. Angeuliza nimeamkaje, nimefika salama au siku yangu imekwendaje. Sasa mimi ndiye ninayelazimika kuanzisha mazungumzo karibu kila mara.

Sijui kama mapenzi yamepungua au labda nimekuwa nikimlazimisha mtu ambaye tayari ameshaanza kuniacha moyoni.

Nimefika mahali najiuliza kama niache kumtafuta kabisa nione kama atanisikia au atanitafuta mwenyewe.

Kama ungekuwa kwenye nafasi yangu, ungefanya nini? Ungeendelea kumtafuta, ungekaa kimya mpaka yeye akufuate, au ungeamua kuachana?

View attachment 3654176
Pole sana jamani.
 
Tafuta kazi ya kukuweka busy! mtu asiwe online kidogo ushatuma msg ushapiga video call.

Muda mwingine mtu yupo online anawasiliana na wateja.
1787305229663.png
 
Ukweli ni kwamba mwanaume anayekupenda na kukuhitaji kwa dhati hawezi kukosa muda wa ku-spend na mpenzi wake.

Ukipata muda wa kuongea nae ana kwa ana mwangalie usoni bila kupepesa macho ila usikodoe sasa halafu muulize kwa upole na eleza wasiwasi wako na jinsi hali hiyo inavyokupa wakati mgumu kihisia, ukimaliza mnaweza kufanya tantric sex.

Baada ya hapo kama hajaonyesha kuguswa na hali hiyo anza kutafuta namna uondoke tu dada inawezekana jamaa ana mipango mingine ambayo wewe hutakiwi kuhusika.
 
Tafuta kitu cha kukuweka bize, acha kuwa idle.
 
  • Thanks
Reactions: ---
Back
Top Bottom