Habari wana jf.
Kama nilivyo andika kwenye kichwa cha habari,huu ni mwezi kama wa 8 hivi nipo katika mahusiano na dada mmoja,kwa kumuangalia kwa kweli. ni dada mrembo sana na anaejitambua,sasa tatizo linakuja kila siku jioni alikua ananiaga anaenda kwa rafiki yake,mwanzoni niliona ni kawaida tu sababu nilikua namwamini sana, mda ulivokua unazidi kwenda nikawa napatwa na wasiwasi,siku mmoja niliamua kufanya upelelezi mimi binafsi,aliniaga anaenda kwa rafiki yake kama kawaida yake,nilikaa kama dk 10 baada ya kuondoka na mie nkamfata mpaka nyumbani kwa rafiki yake,sikuingia ndani nilichungulia tu dilishani,niliwakuta wakivuta bangi bahati nzuri awakuniona,nirudi nyumbn sikuhyo sikumuuliza kitu,umepita kama mwezi hvi, juzi nikamuuliza kama anatumia bangi,bahati nzuri hakua na ubisha alikubali,anasema bangi anayovuta haina matatizo yoyote kwake eti ni starehe tu kama mimi nnavyokunya pombe.tumegombana sana,naombeni ushauri wenu kama kweli bangi na pombe ni sawa na kama anafaa japo tabia nyingi nying za ajabu kwa sasa bado sijaziona.
Najua yupo jamii forum na najua atausoma huu uzi na najua ataanzisha mtiti mwingine, poa tu mi natafuta ushauri tu.