Jaman wanajamvi mim ni
kijana mwenzenu, nilianza uhusiano na mdada flan tangu 2011wakati huo
yeye alikua anasoma diploma chuo flan huko mkoan, mim nilikua first year
chuo kipo hapa dar, baada ya mda mpenzi wangu alinunua laini mpya ya
simu bila kuniambia kwamba anamiliki lain hyo baadae alisahau na
kujikuta siku moja amenitafuta kwa lain hyo, nikamuuliza hiyo namba ni
ya nani? Akajibu ni rafiki yangu,
Mm binafsi nilipata mashaka san hivyo ile namba nikaisave ili mwisho wa
siku nijue ukwel, baada ya siku nying kupita nilianza kupiga ile namba
lakin haipokelewi hata mara moja, nikapata wasiwasi zaidi, aliporudi
likizo nikamuuliza vizuri akasema siyo namba yake hapo nikapata wazo la
kuangalia mwenye hyo namba kwenye tigo pesa nikakuta ni jina la mpenzi
wang, nikamsihi aseme ukweli na hapo akafunguka na kuniomba samahani
nami nikamsamehe lakin baada ya mda nikamuomba aseme ukweli kua hyo lain
kwann alikua anaitumia akasema alikua anatumia kuwasiliana na mpenzi
wake wa zaman anapotaka kumsalimia na akaongeza kua hakua na nia mbaya,
mm nikakubali ili yaishe na yeye akasema hyo lain ameisha ivunja.
Likizo iliisha akarudi chuo baada ya mda mrefu nikajaribu kupiga ile
namba nikakuta inatumika siku hiyo kwa sabab na mm nilipiga na namba ya
rafiki yangu hivyo baada ya yeye kumaliza kuongea akaona missed call
akapiga nikapokea alivyosikia ni mm akakata simu na kuitoa hiyo lain,
siku hyo kwangu ilikua mbaya sana, baadae tukaongea nikasamehe.
Haikuishia hapo alinunua nyingine tena nayo niliipata baada ya
kujichanganya na kunitumia meseji kwa namba mpya maana alikua anatumia
simu ya lain mbili,nikauliza akajibu samahani hii lain ni friend wangu
nikamwambia una uhakika? Hapo akawa na kigugumizi sikuendelea na hyo
topic, siku zikapita nikarudia kuitafuta ile namba ikaita sana bila
majibu, nikamwambia akawa mkali sana, ikabidi mm niwe mpole ili nijue
mambo zaidi.
Baada ya mda nikaangalia jina lain ni ya kwake na alikua anajiamini kwa
sabab mm natumia mtandao tofauti na hyo lain hvyo sio rahisi kumuangalia
kwenye tigo pesa, nilipojua akaomba samahani tena.
Nilichowaza ni kwamba mpenzi wang sio mkweli hivyo nikaamua kumuondoa
moyoni, siku zikapita kuna siku nimepiga simu akapokea mwanaume
nikashtuka sana wala sikuamin ikabidi nikate simu nilipopiga tena
akapokea mpenzi wang nikauliza nani alipokea simu akasema kua ni yeye
mwenyewe alipokea, nikawa mpole tu, kuna wakati kila tulipomaliza
kuagana simu yake ilitoweka hewani kila siku tena kwa lain zake zote na
ikifika saa 12 asubuhi anapatikana nikiuliza anasema mtandao unasumbua
huko mkoa.
Hivi juzi tu Baada ya visa hivyo niliamua kuchepuka ili nimsahau na
niondoe stresse, na kwa bahati nzuri amejua na kuniuliza baada ya kuona
profile picture ya mdada kwenye whatsapp yang, alichokifanya alisema kwa
mama yake na jana mama yake alinipigia simu kua niende ana mazungumzo
na mm, je ndugu mnanishaurije? Niende au nisiende? Mm tayari
nimeshamwambia ukweli kua nimechepuka