Mpenzi wangu anatumia namba mpya ya simu kwa siri.

Mpenzi wangu anatumia namba mpya ya simu kwa siri.

Good Father

JF-Expert Member
Joined
Feb 28, 2014
Posts
10,320
Reaction score
18,599
Jaman wanajamvi mim ni kijana mwenzenu, nilianza uhusiano na mdada flan tangu 2011wakati huo yeye alikua anasoma diploma chuo flan huko mkoan, mim nilikua first year chuo kipo hapa dar, baada ya mda mpenzi wangu alinunua laini mpya ya simu bila kuniambia kwamba anamiliki lain hyo baadae alisahau na kujikuta siku moja amenitafuta kwa lain hyo, nikamuuliza hiyo namba ni ya nani? Akajibu ni rafiki yangu,

Mm binafsi nilipata mashaka san hivyo ile namba nikaisave ili mwisho wa siku nijue ukwel, baada ya siku nying kupita nilianza kupiga ile namba lakin haipokelewi hata mara moja, nikapata wasiwasi zaidi, aliporudi likizo nikamuuliza vizuri akasema siyo namba yake hapo nikapata wazo la kuangalia mwenye hyo namba kwenye tigo pesa nikakuta ni jina la mpenzi wang, nikamsihi aseme ukweli na hapo akafunguka na kuniomba samahani nami nikamsamehe lakin baada ya mda nikamuomba aseme ukweli kua hyo lain kwann alikua anaitumia akasema alikua anatumia kuwasiliana na mpenzi wake wa zaman anapotaka kumsalimia na akaongeza kua hakua na nia mbaya, mm nikakubali ili yaishe na yeye akasema hyo lain ameisha ivunja.
Likizo iliisha akarudi chuo baada ya mda mrefu nikajaribu kupiga ile namba nikakuta inatumika siku hiyo kwa sabab na mm nilipiga na namba ya rafiki yangu hivyo baada ya yeye kumaliza kuongea akaona missed call akapiga nikapokea alivyosikia ni mm akakata simu na kuitoa hiyo lain, siku hyo kwangu ilikua mbaya sana, baadae tukaongea nikasamehe.

Haikuishia hapo alinunua nyingine tena nayo niliipata baada ya kujichanganya na kunitumia meseji kwa namba mpya maana alikua anatumia simu ya lain mbili,nikauliza akajibu samahani hii lain ni friend wangu nikamwambia una uhakika? Hapo akawa na kigugumizi sikuendelea na hyo topic, siku zikapita nikarudia kuitafuta ile namba ikaita sana bila majibu, nikamwambia akawa mkali sana, ikabidi mm niwe mpole ili nijue mambo zaidi.
Baada ya mda nikaangalia jina lain ni ya kwake na alikua anajiamini kwa sabab mm natumia mtandao tofauti na hyo lain hvyo sio rahisi kumuangalia kwenye tigo pesa, nilipojua akaomba samahani tena.

Nilichowaza ni kwamba mpenzi wang sio mkweli hivyo nikaamua kumuondoa moyoni, siku zikapita kuna siku nimepiga simu akapokea mwanaume nikashtuka sana wala sikuamin ikabidi nikate simu nilipopiga tena akapokea mpenzi wang nikauliza nani alipokea simu akasema kua ni yeye mwenyewe alipokea, nikawa mpole tu, kuna wakati kila tulipomaliza kuagana simu yake ilitoweka hewani kila siku tena kwa lain zake zote na ikifika saa 12 asubuhi anapatikana nikiuliza anasema mtandao unasumbua huko mkoa.

Hivi juzi tu Baada ya visa hivyo niliamua kuchepuka ili nimsahau na niondoe stresse, na kwa bahati nzuri amejua na kuniuliza baada ya kuona profile picture ya mdada kwenye whatsapp yang, alichokifanya alisema kwa mama yake na jana mama yake alinipigia simu kua niende ana mazungumzo na mm, je ndugu mnanishaurije? Niende au nisiende? Mm tayari nimeshamwambia ukweli kua nimechepuka
 
Ujue mbwa wanapenda kuchezea manyoa ya kuku? Ukiona manyoya anaweza kuwa kalambwa na mbwa tu, usihofu. Fuatilia ligi kwa karibu, yawezekana anataka kufungua dirisha dogo la usajili au keshasajili na mchezaji wnajifanyia warm up.
 
Unaitwa na mama yake mlitambulishana kwa wazazi?
 
Unaitwa na mama yake mlitambulishana kwa wazazi?

Hapana hatujawahi kutambulishana mkuu isipokua kwao niliwahi kufika maana kuna wakati mama yake alikua mgonjwa sana hivyo ikanibidi niende kumsalimia tu
 
Hapana hatujawahi kutambulishana mkuu isipokua kwao niliwahi kufika maana kuna wakati mama yake alikua mgonjwa sana hivyo ikanibidi niende kumsalimia tu
Kama hamjatambulishana huenda anakuita kwa swala jingine jaribu kumuuliza kwenye simu kama hutaki kwenda umwambie upo busy.
Lakini je mwanae/huyo mpenzi wako bado unataka kuendelea nae?
 
Nimpenzio au mkeo?
Maana mpaka anashtak kwa mamaye ujue ni mkeo na anamwambia mama yake ili iweje, line atumie kisiri tena kakudanganya, umemsamehe na bado amwambia mamaye kuhusu wewe kuchepuka.
Hepu tulia wewe uende wapi wajinga ndoo waliao na sio kila jogoo akiwika nikumekucha shauli yako!!
 
Kama hamjatambulishana huenda anakuita kwa swala jingine jaribu kumuuliza kwenye simu kama hutaki kwenda umwambie upo busy.
Lakini je mwanae/huyo mpenzi wako bado unataka kuendelea nae?

Mm sina hata hamu naye kabisa na hata nikiamua kwenda kwao najua hiyo ndo topic inayofanya niitwe na ikitokea mama anashauri turudiane mm kiukweli ni mdhaifu sana hua siwezi kua na mpenzi zaidi ya mmoja hivyo huyu mpenzi wang wa sasa nitamwambia nn endapo atajua maana ananiamini sana wala sitaki kumuumiza hata chembe
 
Profile pic ya whatsapp uliweka picture ya nani???

Niliweka picha ya mpenzi wang wa sasa kwa sababu yeye nilikua nimeshaamua kumpotezea tu ila tangu arudi anakua na bidii za kunitafuta sana yale aliyonitendea wakati yuko chuo huko mkoa amesahau tena, wakati mwingine anataka hata kuja home kwa sabab anajua nipo chuo nimeshamaliza na sijaanza mishe yoyote
 
Kwangu nikijua una line nyingine na hujaniambia basi kwenu unaenda, sipendi ujinga na kudanganywa laa sivyo utaja juta
 
kati ya vitu visivoisha stori na mikada hapa duniani ni suala zima la mapenzi.....
 
Mm sina hata hamu naye kabisa na hata nikiamua kwenda kwao najua hiyo ndo topic inayofanya niitwe na ikitokea mama anashauri turudiane mm kiukweli ni mdhaifu sana hua siwezi kua na mpenzi zaidi ya mmoja hivyo huyu mpenzi wang wa sasa nitamwambia nn endapo atajua maana ananiamini sana wala sitaki kumuumiza hata chembe

Unafurahisha sana mkuu....sana!
 
kati ya vitu visivoisha stori na mikasa hapa duniani ni suala zima la mapenzi.....
 
Niliweka picha ya mpenzi wang wa sasa kwa sababu yeye nilikua nimeshaamua kumpotezea tu ila tangu arudi anakua na bidii za kunitafuta sana yale aliyonitendea wakati yuko chuo huko mkoa amesahau tena, wakati mwingine anataka hata kuja home kwa sabab anajua nipo chuo nimeshamaliza na sijaanza mishe yoyote

we nae mbona mwanaume mzima huna msimamo mtu ushamuona anatabia ya kukudanganya lkn bado uko nae unataka akuletee magonjwa ndio umuache . achana na huyo binti endelea na huyu mpya. na kwao usiende we unajua kamwambia nini mama yk. sasa we nenda hafu ukute kamwambia mama yk anamimba yk shauri yk
 
Back
Top Bottom