Mpenzi/Mke akisema "naondoka" mwanamme afanye nini?

  1. Mapenzi kitu ajabu, yakutia bumbuwazi
    Yakufanya uwe bubu, kujibu huwa huwezi
    Shubiri kwako zabibu, na vitamu huviwezi.
  2. Wamkuta kaemewa, asemayo hayajuwi
    Aumba akiumbuwa, aona maruwiruwi
    Vigumu kumuopowa, na kwa ngisi kumvuwi.
  3. Hukumbuka ya zamani, yote walofanyiana
    Nyumbani barabarani, ayaona kama jana
    Akili yake ya nyani, aruka inagongana.
  4. Wangoja nyota ya jaha, kutwa wewe unahaha
    Mawazo yako silaha, akukwaaye usaha
    Usifanyiwe msaha, waugeuza karaha.
  5. Kalelewa kaleleka, utani kwake ni mwiko
    Njiani yeye na kaka, hapokei mualiko
    Ghadhabu zake za paka, hapendi maziko
 
Akikuambia hivyo halafu hana sababu ya maana mpuuze,lakini kukiwa na sababu ya msingi zungumzeni akigoma mwache aende!
 
Imefika mahali mwanamke anasema "I'm leaving you" au "Naondoka" na anaweza hata kuanza kufunga virago na hata kukata tiketi. Je ina maana gani? Je mwanamme afanye nini? Je anatingisha kiberiti tu au ni hasira? Au mwanamme amwambie tu "nenda kwani nani kakukataza?". Hivi dada zetu wanaposema hivi huwa wanamaanisha kweli? Je mwanamme akionekana hajali kama ataondoka au la ni sahihi au ndio kutegeana...?
MWanakijiji... this is sensitive

But I believe a woman would never leave without alternative, the best thing to say is goodbye and goodluck, and you need to agree how you gonna help the kids if she s leaving with them. Never stop a woman who wants to leave, they never come back (at least emotionally) and you dont want that

Unless they are joking or childish
 
anayataka kuondoka wala hua hakuambii. unakuta keshafunga virago kaondoka. wa kusema anaondoka, huyo anakupima tempreture, wala si muondokaji.
 
Back
Top Bottom