Mpenzi/Mke akisema "naondoka" mwanamme afanye nini?

Ni kweli. Alikuwa ananituhumu 'kufanya kitu' ambacho mimi nilikuwa na uhakika 100% kuwa hakikuwepo/sikukifanya....so nilikuwa na 'confo' la kumwacha afanya analotaka. Nadhani alifanya uchunguzi akagundua kuwa 'kachemka' ikabidi arudi. Hata hivyo nilipitia kipindi kigumu sana.....it was the worst time of my marrige!

pole sana, wanawake tumezidi kutingisha vibiriti. Ingawa inaumiza lakini akijirudisha mwenyewe anakuwa na adabu.
 
Inategemea na kosa,
mengine wanaume huwa mnakera ndo maana anaamua kuchukua uamuzi huo
amekata tkt jibu ni kwamba hatanii wala kuzuga hiyo ni safari.
 
Asante. Baada ya kurudi, siku za mwanzo hata yeye alikosa amani kwa sababu hakutegemea ingekuwa simple vile.....alikuwa anahisi najiandaa kumfanyia kitu kibaya/kulipiza kisasi. Anyway, yalikwisha....na sasa tunatoa uzoefu wetu kwa wengine.
 
Imefika mahali mwanamke anasema "I'm leaving you" au "Naondoka" na anaweza hata kuanza kufunga virago na hata kukata tiketi. Je ina maana gani? Je mwanamme afanye nini? Je anatingisha kiberiti tu au ni hasira? Au mwanamme amwambie tu "nenda kwani nani kakukataza?". Hivi dada zetu wanaposema hivi huwa wanamaanisha kweli? Je mwanamme akionekana hajali kama ataondoka au la ni sahihi au ndio kutegeana...?

Unanchekesha, huyo si wakuondoka "mwenye kuondoka haagi".
 
khaaa jamani mbona hii inanigusa sana,nimepata jibu maana na mimi nipo njiani kuondoka
 
Lakini kama ukimuacha akaondoka na kakuacha nyumba na watoto; utamfuata? Kuna ule wimbo wa zamani wa "najuta najuta umaarufu umeniponza"...
 
wakuondoka kikweli wala hasemi...anafungasha kimya kimya..unarudi kutoka kazini unampata kaondoka...huyo anakutingishia tu ahahahhaha
 
Lakini kama ukimuacha akaondoka na kakuacha nyumba na watoto; utamfuata? Kuna ule wimbo wa zamani wa "najuta najuta umaarufu umeniponza"...

Mwanamme mwenye kumpenda mkewe hata siku moja hamwachi mamaa ahamishe hata pochi kutoka chumbani!
Mwanaume wa ukweli hamwachi mkewe hata ahame chumba sembuse kuhama nyumba!
Mwanaume anayemkubalia mkewe harakaharaka ujue huyo ana hila na alikuwa
anamfanyia mke vitimbi makusudi ili ule usemi wa "akufukuzaye hakwambii toka" utimie.

Sasa basi wewe mwanaume mwenye hila, mke akikuachia nyumba na watoto ujue kumekucha!
Ukimleta huyo bi-mdogo wako ujue ndio "mwanzo wa mwisho wako" umefika.
Watakuja watu hapa kukupa shuhuda zao im sure.
 
Usiumize kichwa we mfungulie mlango, muonyeshe njia aanze safari! usihangaike nae kwani siku hizi maisha ni kusaka mahela huyo atakupotezea muda. Kama ataona umuhim wa ndoa baada ya kutafakari basi mruhusu ajieleze nini kasoro isiyotatulika!
 
Kwanini inaonekana wanaume wengi tuna attitude tu ya "mwache aende kama anataka" ni kana kwamba tuko tayari kushusha mzigo safari iendelee.
 
Mwanaume hupaswi kuchoka kubembeleza ndio kazi yenu haswaa. Unaweza sema anatikisa kiberiti kumbe ndo kimoja. Kama unampenda kweli kweli how much energy does it take kumbembeleza? Tena usibembeleze kwa sijuhi kumnumnulia kanga sijuhi nini; by words. Many of us women prefer maneno matamu kuliko zawadi. Maana kama ni mavazi naweza nunua mwenyewe nataka love. Those sweet words are more valuable than gold.
 
  • Thanks
Reactions: BAK

sasa labda kina dada nao wanafikiria kila mwanamme anajua kutumia maneno matamu...sasa kwa wanaume ambao hawana kipaji cha maneno yenye ulimbo hawa wanaweza kusaidiwa vipi? Maana wapo wengine wana kigugumizi - huyu akianza kukubembeleza si unaweza hata ukalia? wengine ni wa kimya tu kwa asili sasa ukimwambia "naondoka" ukitarajia ataanza kukuimbisha si ndio imekula kwako? Au wanawake wanafikiria wanaume wote wana maneno matamu?
 
Imefika mahali mwanamke anasema "I'm leaving you" au "Naondoka" na anaweza hata kuanza kufunga virago na hata kukata tiketi. Je ina maana gani? Je mwanamme afanye nini? Je anatingisha kiberiti tu au ni hasira? Au mwanamme amwambie tu "nenda kwani nani kakukataza?". Hivi dada zetu wanaposema hivi huwa wanamaanisha kweli? Je mwanamme akionekana hajali kama ataondoka au la ni sahihi au ndio kutegeana...?

Kwanza inabidi uifahamu fika sababu iliyomfanya aamue kufunga virago na kuondoka. Kama unakubaliana na sababu yake iliyomfanya aamue kufanya hivyo nawe unaona kweli ulifanya kosa kubwa ambalo ilibidi kuomba samahani kwa kosa lako na pia unaliona kosa hilo ni kubwa kiasi ambacho kinaweza kumfanya mke kuamua kuondoka, basi hakuna ubaya kujaribu kuomba samahani ili abadilishe msimamo wake huo, vinginevyo kama hukubaliani na kosa lililotokea lilikuwa ni kubwa kiasi cha kuamua afunge virago basi unaweza ukala ngumu na kumuacha afanye atakavyo, lakini majuto ni mjukuu unaweza baadaye kujutia kwanini hukujaribu kumshawishi abadili uamuzi wake.
 
kimsingi mwanafanya hiyo,kutii mila na desturi na tamaduni fulani.mwanaume hutakiwa kutii amri hiyo ili
kushinikizwa kukubaliana na jambo fulani ikiwa pamoja na kuangalia kiasi cha upendo kilichobakia kwa mwanaume
. kumbuka kuvumbuka ndo nini hasa?
 
mwache aondoke.......ila baadae ulizia kama amefika huko alikoenda au wape taarifa ndugu zake kuwa ameondoka............ then kaa kimya wala usimfatefate!
akirudi kama bado unampenda inabidi muanze zile procedures za watu wanaokutana kwa mara ya kwanza maana alikotoka hujui alkua na nani!!:focus:
 
Back
Top Bottom