Mpenzi au mke wako akibakwa... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mpenzi au mke wako akibakwa...

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Mzee Mwanakijiji, Sep 26, 2011.

 1. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #1
  Sep 26, 2011
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Yaweza kuwa ni mpenzi wako au mke wako au mama wa watoto wako; linatokea tukio ambapo anabakwa (ujambazi, kuvamiwa, kutegeshwa n.k). Na anakuja na machozi na kukulia na kusema tukio hilo na ni kweli vipimo vya hospitali vinaonesha katendewa jambo hilo.

  a. Unafanya nini?
  b. Unamuamini?
  c. Utamsaidia kupita kwenye tukio hilo?
  d. Utaendelea kuwa naye.

  Je kama wewe ndio mwanamke na tukio hilo limekutokea na unawezekano wa kulificha kwa mwenza wako je utaficha hutamwambia? Ukiamua kumwambia unatarajia nini?
   
 2. Rejao

  Rejao JF-Expert Member

  #2
  Sep 26, 2011
  Joined: May 4, 2010
  Messages: 9,239
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  hapa ndipo mtu anakuwa na wakati mgumu sana,,,
  kwa sasa ukisema utafanya hivi au vile kabla huijakutokea, utakuwa unajidanganya!
   
 3. ndetichia

  ndetichia JF-Expert Member

  #3
  Sep 26, 2011
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 27,641
  Likes Received: 236
  Trophy Points: 160
  mmmhh hapa inahitajika busara zaidi na sio kukurupuka maana ishu kama hizi hupelekea watu wengine kujiua au kujiingiza kwenye mambo mabaya(pornography) na kupotea moja kwa mojakwa kile anachodhani kuwa hakutendewa haki na jamii haitomuelewa..
   
 4. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #4
  Sep 26, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,345
  Likes Received: 19,529
  Trophy Points: 280
  si utaenda kufanya vipimo lakini?
   
 5. Rejao

  Rejao JF-Expert Member

  #5
  Sep 26, 2011
  Joined: May 4, 2010
  Messages: 9,239
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  tatizo siyo kupima...psychological utakuwa affected sana
   
 6. King'asti

  King'asti JF-Expert Member

  #6
  Sep 26, 2011
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 27,508
  Likes Received: 2,249
  Trophy Points: 280
  kubakwa ni kitu ambacho kinaathiri kisaikolojia,sio kwa mhanga pekee,bali pia hata kwa familia na watu wa karibu. mwenza wa mhanga wa kubakwa anahitaji msaada karibu sawa na aliyebakwa. ataadhirika kisaikolojia,lakini cha kwanza atakua kwenye denial phase. hatoamini, halafu hatoamini kama mbakwaji alibakwa bila ridhaa ama kusababisha mwenyewe.
  kama mimi ndie mhanga, cha kwanza ni kumtaarifu umpendae (anaweza kuwa sio mwenza,itategemea na mahusiano yetu yakoje kikawaida na wakati wa tukio). they say when u ar not happy u call the person whom u think loves u the most. and when u ar happy u call the person whom u lov the most. so wa kwanza kumuambia na ku-share nae the grief ni yule unaejua anakupenda sana (anaweza kuwa mwenza/mpenzi, mama, dada, rafiki wa karibu wa kike ama wa kiume).
   
 7. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #7
  Sep 26, 2011
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Jinsi tunavyochukuliana na wenz\i wetu wakati wa majonzi na majaribu kama haya ndio kipimo kizuri sana cha kuonyesha upendo wetu. Ni rahisi sana, kwa kuwaza haraka haraka, kwa mtu kudhani kuwa unaweza kumsaidia mtu kama huyo katika yote atakayoyahitaji wakati huo. Lakini kutenda hivyo ni vigumu sana.
  Kama mimi ndio nipo kwenye nafasi ya mtoa msaada, jambo la kwanza ni kumwonyesha, kwa dhati, kuwa u pamoja naye. lakini msaada mkubwa anaohitaji pamoja na mambo mengine ni ushauri nasaha ili kuitengeneza saikolojia yake iweze kukubaliana na yaliyotokea na aweze kuishi nayo bila kumletea matatizo makubwa. Hii itakuwa ni fursa yangu ya kuonyesha uopendo wangu wkake kwa kumpatia kila aina ya msaada atakaouhitaji kutoka kwangu
   
 8. BADILI TABIA

  BADILI TABIA JF-Expert Member

  #8
  Sep 26, 2011
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 30,873
  Likes Received: 6,225
  Trophy Points: 280
  kumsupport. Hapo unapiga moyo konde, ziweke hsia zako kando. Kuwa nae bega kwa bega hadi awe sawa
   
 9. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #9
  Sep 26, 2011
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,323
  Likes Received: 22,152
  Trophy Points: 280
  upendo huvumilia. Kwenye furaha na majonzi daima pamoja. Nitampenda zaidi ili afarajike na kusahau maumivu
   
 10. Gaijin

  Gaijin JF-Expert Member

  #10
  Sep 26, 2011
  Joined: Aug 21, 2007
  Messages: 11,850
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 0
  Na ukiwa umebakwa kabla ya kuwa na mpenzi wa kudumu, jee umhadithie ukiwa nae pamoja au uuchune tu?
   
 11. Gaijin

  Gaijin JF-Expert Member

  #11
  Sep 26, 2011
  Joined: Aug 21, 2007
  Messages: 11,850
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 0
  Sio rahisi kujiweka kwenye viatu vya uhanga wa ubakaji. Na inaonyesha kumpigia mtu umpendae ukishabakwa si rahisi na takwimu huonyesha kuwa wanaobakwa hawafanyi hivyo, hata kumwambia mama yako inakuwa tabu licha ya kuwa wengi wanaamini kuwa hakuna awapendae kama mama zao.
   
 12. Dark City

  Dark City JF-Expert Member

  #12
  Sep 26, 2011
  Joined: Oct 18, 2008
  Messages: 16,277
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160
  Mkuu,

  Tunajua kwamba mambo mabaya mengi huweza kututokea wakati wowote ikiwemo hayo unayoeleza au hata kifo...Ila si vizuri kuyafikiria saaana kwana yanaweza kumpa mtu msongo wa mawazo na hata kuathiri maisha yake kabisa endapo atakuwa anayafikiria mara kwa mara. Kwangu mimi binafsi hupenda kuamini kwamba hayatatokea!!

  Sasa kama jambo hilo likimtokea mwenzangu....ni jukumu langu kuhakikisha kuwa anamalizana nalo salama na kurudi katika maisha ya kawaida. Ni kipindi ambacho nitaonesha upendo wa hali ya juu na kujitolea kwa lolote kama vile wakati namwona kwa mara ya kwanza. Siwezi kumwonesha hata chembe ya shaka hata kama maelezo yake yana makona kona.

  In short...Kama mke wangu anataka kunifool basi anieleze kabakwa hata kama alifanya hivyo kwa hiari. Kwani hawezi kubakwa na mtu yule yule zaisi ya mara moja!!

  Babu DC!
   
 13. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #13
  Sep 26, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,345
  Likes Received: 19,529
  Trophy Points: 280
  yap ni kweli...hapa sasa inabidi watafutwe wana saikologi.bila hivyo kuna uwezekano wa kujinyonga
   
 14. Mamndenyi

  Mamndenyi JF-Expert Member

  #14
  Sep 26, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 29,081
  Likes Received: 6,544
  Trophy Points: 280
  nitarudi tena.
   
 15. S

  SURUMA JF-Expert Member

  #15
  Sep 26, 2011
  Joined: Mar 22, 2011
  Messages: 2,908
  Likes Received: 124
  Trophy Points: 160
  Mwana Kijiji hii kusema UTAFANYA NINI kabla haijatokea ni ngumu saaana...NI sawa na kusema SIKU NIKIMFUMANIA JAMAA NA MKE WANGU NITAFANYA kadha wa kadha...SI KWELI KWANI MAAMUZI MENGINE NI SENSITIVE MNO na hutegemea zaidi na muda limetokea, wewe upo katika hali gani muda huo na factors nyingine nyingi ambazo kwa kusema kabala haijatokea tunakuwa tunajifariji (kama si kujidanganya) zaidi.....

  Mfano hai ni jamaa aliyembiwa mkewe ana mahusiano na njemba ingine.Mme akasema anaweza kuvumilia kuona TUKIO ili kupata kidhibiti...Mbona alizimia siku anachungulia tundu la ufunguo kupata kidhibiti kwa yaliyokuwa yakisemwa....NI NGUMU Mwana Kijiji ki ukweli
   
 16. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #16
  Sep 26, 2011
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Hili swali lina implications nyingi sana; vipi kwamba baada ya kubakwa mama anapata ujauzito? - wapo watu mashuhuri ambao walizaliwa kutokana na rape! vipi kama katika kubakwa akapata kilema au kuambukizwa?
   
 17. RR

  RR JF-Expert Member

  #17
  Sep 26, 2011
  Joined: Mar 17, 2007
  Messages: 6,719
  Likes Received: 206
  Trophy Points: 160
  Kwa matukio ya aina hii ni ngumu sana mtu kujiwekea msimamo, kwamba unatafanya nini likitokea tukio...
  Unajisikiaje kujenga picha ya mwenzi wako kubakwa? Pia ni sawa pia kumwambia mwanamke aseme atafanyaje akibakwa......
  Au mtu uulizwe utafanya nini mwenza wako akifa....

   
 18. Tausi Mzalendo

  Tausi Mzalendo JF-Expert Member

  #18
  Sep 26, 2011
  Joined: May 23, 2010
  Messages: 1,471
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0

  No woman i believe will tell her man if she has been raped!! Ukweli usemwe tu hapa. Wanaume hawaangalii tukio hilo kama uhalifu bali kama kitendo cha ngono.Ukimwambia kuwa umebakwa si ajabu ukajikuta unadhalilika mara ya pili kwa maana ya kulaumiwa kuwa umejitakia.
   
 19. Gaijin

  Gaijin JF-Expert Member

  #19
  Sep 26, 2011
  Joined: Aug 21, 2007
  Messages: 11,850
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 0
  Utaulizwa masuala kama why did you open the door na unajua uko peke yako? Why does he even know your address kama hukumpa? Na shutuma nyingi kama inasababishwa na the way you dress up, the way you conduct yourself in front of him

  Na hofu ya kusema inazidi hasa ikiwa mbakaji ni mtu unaemjua
   
 20. ndetichia

  ndetichia JF-Expert Member

  #20
  Sep 26, 2011
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 27,641
  Likes Received: 236
  Trophy Points: 160
  hata kama humjui bado inakuwa nakaugumu fulani kuwa atanielewaje..
   
Loading...