Nyani Ngabu
Platinum Member
- May 15, 2006
- 97,103
- 136,762
Mwanamke akiwa peke yake asiingie bar ili asidhaniwe anategesha?
Hapana, simaanishi hivyo. Pesa si pesa zake bana, sasa kama anazo kwa nini naye asiingie kwa lengo la kuburudika tu? Na aingie tu.
Ninachozungumzia ni perception. Na perception mara nyingi huwa hazitoki tu out of nowhere. Zina genesis zake na moja ya genesis za hizo perceptions za wadada kuketi kwenye baa peke yao ni wale wadada wauza sukari ambao nao hupenda sana kwenda kutegesha kwenye mabaa as opposed kusimama barabarani.
Sasa, fairly or unfairly, hawa wagawa sukari huharibu sifa za wanawake wengi hasa kwenye muktadha wa viota vya burudani.