Mpasuko ndani ya chama, Rais Samia awaomba vijana wasitoe fursa

mtoto wa mchungaji

JF-Expert Member
Oct 24, 2020
279
480
Akiongea na vijana wa UVCCM Pemba leo mama amewatahadharisha vijana kukataa kutumika na watu wenye nia ovu ndani ya chama wanaotaka kukipasua chama vipande vipande.

Vijana hao ambao wamekunywa na kugida maji ya bendera walionyesha kumuelewa mama huku wakisikiliza kwa hisia kubwa hotuba hiyo na wakati mwingine wakimkatiza mama na kuanza kuimba kuwa TUNAIMANIII NA MAMAAA OYAA OYAAA.

Mnaweza changia.

================

Rais Samia Suluhu: La pili kwenu vijana ni mpasuko ndani ya chama, naomba msitoe fursa, msitoe fursa kutumiwa kukipasua chama. Jeuri yenu, makidai yenu, kwenda kwenu kifua mbele kwasababu chama kiko imara. Mtakapokipasua vipande vipande hamtafanya haya mliyoyafanya leo.

Kwahiyo niwaombe sana, nendeni mkaimarishe chama chenu, kaimarisheni jumuiya yenu, vijana msitumike vibaya.
 
List ya hao watu ipo ....mmoja kaenda, bado mwenezi wa kale
 
Mama anapresha na uchaguzi naona anaandaa kikosi chake vzr, na amesema ataongea nao vzr kabla ya uchaguzi wao
 
Mh, mamaaa,Kama uko vitani na umetanabahisha hivyo unao majemedari,makamanda na wapiganaji waaminifu kweli? Maana nijuavyo Mimi ukitangaza Vita adui nae anaingia vitani rasmi na hapo mtanange unaanza kiukweli na sio mafichoni!
Mama umezungukwa na watu wanafiki haijapata kutokea ndio maana hawakuambii hata huo ukweli,huku chini Hali sio shwali Akina mama walio wengi wanaupinga utawala wa CCM hadharani na bila uoga Hali hii haijawahi kutokea toka tupate uhuru.
Mama pambana huko juu lakini huku chini panateketea mpaka chawa watakapo kutanabahisha itakuwa huna la kufanya zaidi ya kuwa raisi aliyetawala kipindi kifupi zaidi Tena kwa kudra za Mungu.
Usinichukie nakutanabahisha tu.
 
Back
Top Bottom