Dr Akili
JF-Expert Member
- Aug 21, 2011
- 4,953
- 4,326
Ni zaidi ya mwaka mmoja sasa tangia waziri wa nishati, Mh. January Makamba, atangaze mpango wa serikali utakaoiwezesha nchi yetu kuwa petrol hub itakayokuwa inasambaza mafuta haya kwa nchi nyingi za SADEC na Afrika Mashariki.
Mpango ulikuwa kwa kushirikiana na nchi rafiki za OPEC+ kujengwa kwa kituo kikubwa kabisa jijini Dar es Salaam cha kupokea na kuhifadhi mafuta haya (yaani petrol hub) kwa soko la ukanda wa Afrika Mashariki na Kati. Katikq mpango huo serikali ya Tanzania ingalikuwa inayanunua mafuta hayo moja kwa moja mafuta hayo kutoka nchi hizo rafiki za OPEC+ kwa bei ya asilimia 25% tu ya bei inayoyanunua kwa sasa kutoka kwa watu wa katikati. Serikali ilitembelea hizo nchi rafiki za OPEC+ na kukubaliana na mpango huu. Mwezi Septemba 2021 majaribio ya ununuzi yalifanyika ambapo serikali iliweza kununua mafuta hayo kwa USD 20 kwa pipa badala ya USD 86 kwa pipa iliyokuwa inayanunua kupitia watu wa katikakati.
Ni zaidi ya mwaka mmoja sasa umepita tangia mpango huo ukubaliwe kati ya serikali yetu na hizo nchi rafiki lakini wizara ya nishati imekuwa kimya kueleza maendeleo wa huo mpango. Jee umetupwa kapuni?