Mpango wa shirika la Ndege ATC uko wapi?

Mpango wa shirika la Ndege ATC uko wapi?

Kamundu

Platinum Member
Joined
Nov 22, 2006
Posts
9,879
Reaction score
15,746
Naona tunanunua ndege, sio jambo baya lakini watu wengi wanapinga kwasababu hakuna mpango ambao unajulikana bado vizuri wa hili shirika.

Je hizi ndege ni kusafiri Africa yote? mikoa yote? Ulaya na US? wa watafanya ushirikiano na mashirika mengine?

Je wana vibali vya kusafiri nchi hizo za nje?..... .

Kama kuna mtu ana plan atuwekee hapa ili tuone. Inakuwa ngumu ku support kitu bila kujua lengo maana kwa sasa kuna ndege nyingi tu zinakuja TZ!
 
Mipango tutaifanya mbele ya safari. Wacha kwanza tufurahie ndege mpya.
 
Swali zuri sana na kama huo mpango upo ni jambo jema. Kingine ningejaribu kufikir ni muda muafaka wa ATCL kujipanga ikae kibiashara.

Hii ya kubebwa na serikali isiwe ndio tegemeo maana kiukweli potential wanayo nzuri mno na kwa ndege zao wanaweza kuwa na nafasi nzuri ya ushindani kwa soko la ndani.

Kinachotakiwa sasa ni wao kujipanga na kukaa kibiashara ili hata siku serikali ikijitoa wataweza kujisimamia vizuri tu.
 
Mpango unaoulizia siyo PUBLIC DOCUMENT ni chombo cha kimkakati cha ndani cha kufanyia kazi ili kufikia malengo ambayo ndiyo hayo ya kuongeza route na kuongeza abiria.

Mpango mkakati wa kibiashara au Business Strategic Plan is a "secret internal document" ambayo adui au mshindani wako wa kibiashara akiuona anaweza kuutumia kukushinda au hata kukuhujumu.

How ever seen such a document for anyother airline company? Tujuze with evidence!
 
Kangi angejibu kwamba, MPANGO KAZI WA SHIRIKA LA NDEGE Tanzania, upo kwenye kitabu cha ILANI YA CHAMA.... tehteehhh.....

Na baada ya ya hapo, angewaomba viongozi wakuu wa shirika hilo wamuonyeshe vitabu kwa kila mmoja kunyenyua chakwake juu..... hahahaha
 
Plan pekee iliyokuwepo ni kumiliki ndege na kuweza kupiga nayo picha, mengine yatajipanga yenyewe. Jiwe ni nabii na siku zote nabii haojiwi maana huona mbali.
Hayo ni maneno ya wapinga maendeleo wote! Hata wakati wa Mwalimu Nyerere tulipokuwa tunajenga Reli Ya TAZARA, walisema mengi sana, hasa wakoloni na wapambe wao eti hii ni bamboo rail haitadumu mara hili mara lile ili mradi kuonyesha kujeli ya aina moja au nyingine ingawa walikuwa anajua ukweli kuwa reli hiyo "ni chuma cha pua" na silaha muhimu dhidi ya ukoloni. Na historia imewaumbua kama itakavyo waumbua watu wengi katika nchi hii wasiopenda kuuona ukweli wa uwekezaji wa aina hii. Ndege imefika jan, nyingine inakuja na picha zitazidi kupigwa - iwe mvua iwe jua iwe masika iwe el nino!
 
Kangi angejibu kwamba, MPANGO KAZI WA SHIRIKA LA NDEGE Tanzania, upo kwenye kitabu cha ILANI YA CHAMA.... tehteehhh.....
Na baada ya ya hapo, angewaomba viongozi wakuu wa shirika hilo wamuonyeshe vitabu kwa kila mmoja kunyenyua chakwake juu..... hahahaha
Wale wale na mambo na majibu ya mzaha kwa mambo MAZITO. Kamuulize hata Rais D.J.Trump kama chake hakina PARTY MANIFESTO!
 
Swali zuri sana na kama huo mpango upo ni jambo jema. Kingine ningejaribu kufikir ni muda muafaka wa ATCL kujipanga ikae kibiashara. Hii ya kubebwa na serikali isiwe ndio tegemeo maana kiukweli potential wanayo nzuri mno na kwa ndege zao wanaweza kuwa na nafasi nzuri ya ushindani kwa soko la ndani. Kinachotakiwa sasa ni wao kujipanga na kukaa kibiashara ili hata siku serikali ikijitoa wataweza kujisimamia vizuri tu.
Mtu mwenye kufikiri anaweza kugundua tofauti yako na Kamundu mleta uzi. Haya ndiyo mawazo ya kujenga.
 
wewe mtoa mada huna hata plan ya maisha yako binafsi hata tukikupa B/P ya ATCL hutojua kitu mambo mengine waachie wanaojua ..........[HASHTAG]#watapatatabusana[/HASHTAG].
 
Swali zuri sana na kama huo mpango upo ni jambo jema. Kingine ningejaribu kufikir ni muda muafaka wa ATCL kujipanga ikae kibiashara. Hii ya kubebwa na serikali isiwe ndio tegemeo maana kiukweli potential wanayo nzuri mno na kwa ndege zao wanaweza kuwa na nafasi nzuri ya ushindani kwa soko la ndani. Kinachotakiwa sasa ni wao kujipanga na kukaa kibiashara ili hata siku serikali ikijitoa wataweza kujisimamia vizuri tu.
Ila hii ndege ya dreamliner ukubwa wake kwa safari za ndani itakua hasara tu, kwanza route fupi sana kwa kiwango cha hii ndege, frequent take offs and landing in less than one hour itaichosha ndege pia, inatakiwa at least ikae angani angalau minimum masaa sita kabla ya kutua!
 
Tunanunua tunatupia stoo kwanza maana ni bidhaa adimu zinaweza kuisha huko zinakotengenezwa ikatugharimu kama taifa kwa kukosa kitu muhimu. Hiyo mipango yako ni baadae zikishatosha kukidhi haja ya kila Mtanzania.
 
Swali zuri sana na kama huo mpango upo ni jambo jema. Kingine ningejaribu kufikir ni muda muafaka wa ATCL kujipanga ikae kibiashara. Hii ya kubebwa na serikali isiwe ndio tegemeo maana kiukweli potential wanayo nzuri mno na kwa ndege zao wanaweza kuwa na nafasi nzuri ya ushindani kwa soko la ndani. Kinachotakiwa sasa ni wao kujipanga na kukaa kibiashara ili hata siku serikali ikijitoa wataweza kujisimamia vizuri tu.
Nia ni njema ila tungeanzia kwanza kwenye mwendo kasi maana tumehama tiketi kukaguliwa na mashine (digital) tumeingia kukagua kwa kuzichana kwa mikono (analogy)
 
Mpango unaoulizia siyo PUBLIC DOCUMENT ni chombo cha kimkakati cha ndani cha kufanyia kazi ili kufikia malengo ambayo ndiyo hayo ya kuongeza route na kuongeza abiria. Mpango mkakati wa kibiashara au Business Strategic Plan is a "secret internal document" ambayo adui au mshindani wako wa kibiashara akiuona anaweza kuutumia kukushinda au hata kukuhujumu. How ever seen such a document for anyother airline company? Tujuze with evidence!
Adui kwenye hili ni nani? Plan za mashirika mbona zipo kwenye website zao na report za miezi mitatu za mapato hasa kwenye kampuni zinazoendeshwa kibiashara!? hivyo huu si ukweli. Hiyo secret plan imeandaliwa na nani ? Je wameonyesha bunge la wananchi?. Sasa kama ni plan za siri za kibiashara ni nani ambaye atahakikisha pesa ya wananchi inatumika vizuri? GAG naye anaruhusiwa au ni siri kwake pia? Ukweli ni kwamba kama plan haipo mseme badala ya kujifanya mnayo na kuishia kwenye hasara maana makampuni ya ndege ni gharama sana kuendesha na faida mengi hayana
 
[QUOTE="Kamundu, post: [/QUOTE]
Good
 
Naona tuna nunua ndege sio jambo baya lakini watu wengi wanapinga kwasababu hakuna mpango ambao unajulikana bado vizuri wa hili shirika. Je hizi ndege ni kusafiri Africa yote? mikoa yote? Ulaya na US? wa watafanya ushirikiano na mashirika mengine? Je wana vibali vya kusafiri nchi hizo za nje?..... . Kama kuna mtu ana plan atuwekee hapa ili tuone. Inakuwa ngumu ku support kitu bila kujua lengo maana kwa sasa kuna ndege nyingi tu zinakuja TZ!
Mkuu Kamundu, alichukujibu Mzee Mukaruka ni ukweli mtupu, strategic business plan ya biashara yoyote ni secret internal document ambayo washindani wako hawapaswi kuifahamu!.

Ila pamoja na siri hiyo, kiukweli kabisa na bila kuwaonea, hizi ndge tumenunua na pupa na papara bila business plan ili tuu kuonyesha tunaweza. Ndege zikiisha wasili ndipo tunaandaa business plan!. Hivyo ndivyo tulivyofanya kwa Bombadier na labda ndivyo tunavyofanya kwa Dreamliner, ndege imewasili siku ya Jumapili, kesho yake Jumatatu, ATCL wamekaa na TTB kusainiana MOU kupeleka ndege Ghwanzou, Mumbai na London, huku wanajua fika hutuna landing rights, na ATC haina air worthiness certificate kutoka IATA, kitu ambacho Watanzania tunachofanyiwa ni kutoelezwa ukweli bayana!, aliyetoa siri ndege yetu imeshikiliwa kwa kudaiwa, mnakijua kilichomkuta!.

Ili Dreamliner yetu ivuke mpaka wa kutua popote nje ya bara la Africa ni kwanza lazima tuikodishe kwa mashirika wenye landing rights hizo, vinginevyo tulipe deni la IATA tunadaiwa Zaidi ya US $ million!.

Ni ukweli usiofichika, kuirusha Dreamliner kwa routes za ndani ambazo zote ni short distance less than 1 hour, sio tuu kutaichosha, kuichakaza na kuishorten its life span kutokana na engine wear and tear kwa take off na landing ya short distances kunaichokesha bure engine ya mtulinga!, ila pia operational wise, it's not worth it. This will be a loss making exercise. Enzi za Mwinyi tuliibeba ATC na kuifeed kwa spoon fed while making losses. Mkapa akaruhusu ubia na SAA, JK akagoma kuendelea kuibeba na kuifeed. Sasa JPM kaifufua kwa nguvu kubwa kuliko uwezo wetu to operate haya madubwana makubwa ya long hauls. Hivyo ATC will be making losses lakini JPM will feed it, ila awamu nyingine ikija ndipo itagundua kuwa ATC is a baby that never grows, it's still sucks.

Ili kuinusuru ATCL, tunahitaji a political will ambayo tayari rais Magufuli ameishaionyesha, lakini political will pekee yake bila business viability, ni kuonyeshea just the pride of wings of Kilimanjaro on airwaves but at the expense of poor Tanzanians. Kanisome hapa
Je, ATCL inahujumiwa kibiashara? Tutumie a political will kuinusuru au tuiache iangamizwe na ushindani?
P.
 
Back
Top Bottom