Mpango wa Rais Samia kuimarisha huduma za kibingwa bobezi

kalacha mateo

Senior Member
Sep 27, 2021
118
237
Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan, imeongeza fedha za kusomesha Wataalamu bingwa na bobezi hadi kufikia shilingi Bilioni 8 kutoka Shilingi Bilioni 3 za mwaka wa fedha 2021/22, utakaosaidia kuboresha huduma kwa wananchi na kupunguza Rufaa za nje ya nchi.

Mpango huo umepewa jina la SAMIA HEALTH SUPER SPECIALISATION PROGRAMME IN TANZANIA. Miongoni mwa madaktari watakaosomeshwa ni madaktari Bingwa wa Mionzi, Muuguzi Bingwa wa Mionzi, Mteknolojia Mionzi, Muuguzi Bingwa wa Figo, Muuguzi Bingwa wa Usimamizi wa huduma za chumba cha upasuaji kwa wagonjwa wa Figo na Mtaalamu wa Vifaa Tiba vinavyotumika kwa ajili ya matibabu ya figo.

Jumla ya watumishi 139 wamechaguliwa kupata ufadhili wa masomo ambapo kati ya hao 136 watasomeshwa nje ya nchi na watatu (3) ndani ya nchi, Sambamba na kufadhili watumishi 139 kwa utaratibu wa set pia watumishi 318 watafadhiliwa kwa utaratibu wa mtu mmoja mmoja na kufanya jumla ya watumishi watakaofadhiliwa kuwa 457 kwa mwaka wa fedha 2022/23, ambapo 146 (32%) ni wanawake. Kati ya watumishi 457 watakaofadhiliwa, 157 (34%) watasoma kwenye Taasisi za nje ya nchi.
 
Chini ya Rais Samia Suluhu huduma za afya zimeboreshwa sana hatutaenda india tena kutibiwa matibabu yote yatapatikana nchini
 
Back
Top Bottom