Mpango uliovuruga mbwembwe za EX-Girlfriend

huyo binti wa kinyamwezi kama.namjua hivi
 
Tatizo ni utapindua meza mara ngapi? Yani dunia hii kuumizwa kupo tu. Utajihusisha na huyo chotara, atakuacha kisha utataka kumwonyeshea tena nk. Hakuna sababu ya kuonyesheana na mtu. Demu alikuwa anajionyesha na workmate wake, na ww ukaamua kumwonyeshea. Alikuingiza mkenge, na ww ukazama. Ukaingia gharama nk. Furaha uliyoipata ni ya muda mfupi. Pambana upate amani ya ukweli. Kama ni $$$, basi pambana uwe nazo. Kama ni familia, pambana uwe nayo. Hayo ya kupindua meza wala hayana mantiki. Hapo hata huyo mwanamke atakuheshima heshima unayistahili. Na sio heshima ya ku-show off.
 
kwake yana mantiki as long he was happy with that
 
Umesoma vizuri alichoandika jamaa?

Mwishoni ameandika kuwa mambo mengi ni maigizo kwa wapenzi, jambo la muhimu ni kila mtu kuendelea na maisha yake.

Labda nikuuulize hela ni mbadala wa mapenzi?

Wenye hela huwa hawapitii hizi changamoto za kimapenzi?

Huu muda unaopoteza hapa si ungekuwa unatafuta hela kama hizo hela ndio kila kitu.

Maana hapa mtu akiposti kitu basi watu mnakuja na habari ya hela
 
kwake yana mantiki as long he was happy with that
Watu wengi wanafanya makosa ya kupata furaha feki. Hio ni furaha feki. Demu sio wake. Na sio wa kudumu. Watu wanapenda sana instant gratifications badala ya delayed gratifications. Ili mtu ufanikiwe kimaisha, ni vizuri to focus kwenye delayed gratification.

Kama ni mimi yeye, ningefurahi sana kuona msichana huyo Ex wangu ana mpenzi wake. Ningewapongeza sana sana. Na hata kukaa nao na kuwa rafiki. Nisingeonyesha inaniuma hata kama inauma sababu maumivu ya mapenzi yanaishaga tu.
 
Suala la hela ni mfano tu. Kuna watu hela inawapa furaha, ndio nikasema waitafute hio. Kuna watu familia inawapa furaha, nikasema watafute familia. Mimi nina hela zangu ndg. Niko sawa kabisa kiuchumi. Napenda JF sababu najifunza mengi. Kuwa na hela haimaanishi kujitenga na watu.
 
Ww post yangu yote ulichoona ni hela tu? Una matatizo ww.
 
Furaha muda mwingine lazima ufake huwezi kua mnyonge kila saa.
 
bora hata hiyo furaha feki wewe huoni mtoa maada alivyojiona kidume tena mpaka huyo x wake kaumia huo ni ushindi tosha kwake
 
Paragraph ya mwisho
"... Sio kila unachokiona ndivyo kilivyo. Wakati mwingine X anaweza kutaka kukuumiza tu. Relax na ufanye mambo yako...."
 
Furaha muda mwingine lazima ufake huwezi kua mnyonge kila saa.
Mimi nilikuwa maskini sana, nikaenda abroad nikashika milioni 140 kwa mwaka. Nikaja tz ku-show off. Nikachezea muda na hela sana kupata furaha feki na watu ambao mambo yalipoharibika baadae walinitupa wote.

Mungu akasaidia nikarekebisha mambo na kupata $$ ya kutosha. Naishi maisha yangu ya furaha wala sihitaji ku-show off. Nyumba zipo magari yapo, ila mara moja moja napanda daladala au hata toyo. Heshima yangu iko palepale hata nipande toyo sababu watu wanajua nilivyojijenga kiuchumi.

Ni vizuri kupata heshima halisia na sio sababu ya ku-show off
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…