Mpango mzima wa kuihusisha CHADEMA na ugaidi mpya huu hapa

Mpango mzima wa kuihusisha CHADEMA na ugaidi mpya huu hapa

Mtoi, nina maangalizo kadhaa kutokana na maelezo yako yanayojikanganya,

1. Chanzo -CDM Diaspora unategemea nini kama sio habari za upande mmoja...kwa sasa ni vema kumsikiliza bwana Yona kwanndiye mtekwaji na pia kwani kila Mbowe na Slaa wanapowasiliana na viongozi lazima wakushirkishe? kuna ukweli alionywa na uongozi kwamba aache mahusiano naZitto kwani hata sasa uongozi wa CDM umeagiza viongozi na wanachama kutoshirikiana na Zitto , Hili lina ukweli

2. Zitto na wenzake wamefukuwa kutokana na waraka wa kutwaa madaraka kinnyume na Katiba......Wewe unatueleza kwamba Mwakembe katangaza kugombea uenyekiti Temeke, je sio uhaini? Kileo kajhalalisha kwamba yeye ndiye mgombea mteule wa Ubunge Mwanga bila kufuata katiba....je nikweli hamna wana CDM wengine wenye nia....kama ambavyo mnasisitiza siku zote kwamba wagombea wafuate utaratibu uliopo kwenye katiba, au kuna wanaoruhusiwa kwenda kinyume?

3. Ni ngumu kutenganisha utesaji wa Yona na CDM,kama ilivyo ngumu kutenganisha utesaji wa Ulimboka na Serikali!

3.
Yaani wewe mtu ni mjinga wewe.Sijui ulikula makamasi ulivyokuwa mdogo?
 
Mtoi omba uwe mtiifu siku zote kwa hao wauaji siku ya kujitambua na kusimamia ukweli utajikuta matatizoni pia.
 
mimi katika vitu nisivyoamini katika hii bongo muvi ni hivi.
1.haiwezekani mtu akatekwa ba kuchubuliwa usoni kama kaanguka na baiskeli halafu atupwe vichakani alale hapo mpaka wapiga picha waje.
2.haijawahi watekaji wakabishana na waliyemteka ambaye wanafahamiana na kuchubua usoni(badala ya kumuua).
3.kwa vile limeshaingia mikononi mwa director wa muvi ssp kova linakosa uhalali kama la dr uli.
4.kama ulimboka alitupwa mabwepande akiwa hoi bin taaban na yona ametupwa ununio akalaa hapo mpaka waandishi wa habari wakaja na alipofikishwa hospitalini akaishia opd ana mengi ya kutueleza kuhusu hiyo tamthilia.

namalizia kwa kumwambia kova kuwa historia anayoitengeneza ndani ya jeshi letu la polisi itamhukumu kabla hajaonja mauti.
 
pamoja na kwamba mimi sio mpenzi,mfuasi wala mwanachama wa ccm, lakini kamwe siwezi kubishana na ukweli.
sio lowasa tu!! viongozi wote wa ccm hawawezi kuhama ccm kwa sababu huko ndiko iliko salama yao. na kuhusu uwezekano wa ''ETI CHADEMA KUCHUKUA DOLA" hilo kila mwenye akili anajua ni ndoto za mtembea juani.
THIS COUNTRY WILL NEVER BE GIVEN TO DOGS...
Haswa katika kipindi hichi ambacho'' DOGS ARE CHASSING PATRIOTIC MEN/WOMAN TO POSSES THE PART''

Jukwa hili ni jukwaa huru kwa kutoa maoni lakini umepitiliza na umevunja kanuni kabisa kwa kuwaita binaadamu 'Mbwa' ,aisee umekosa busara sana .
 
Hawa akina kova, kamhanda, shilogile, mulongo, na wengine woote! wanahangaika kutafuta vyeo bos wao.
 
Uimara wa Chadema ndo unasababisha wa wapinzani wajr na wasaliti kutumia mblinu mufilisi kukihujumu na wanaonal hawana jinai ya kipenya kisambaratiwha nyome yake. Kwa mtu yeyote timamu hawezi kusema Chadema ni dhaifu. Uimara wale unawamyima magamba usingizi kila siku. Vyama dhaifu wavijua kabisa havina ushawishi wala public reputation. Huu ni mwendelezo wa hujuma lakini tutapita tu. Hili sio kubwa kama la Lwakatare,Kileo,La mabomu Arusha na yake yote ya uchaguzi 2010. Mungu ni mwema na sala za wenye haki na machozi yao zitasimama kwa ajili ya ukombozi wa kweli. Tuna machungu wana moyoni kwa udhalimu huu. Laiti mngalijua jinai Ccm inavyochuliwa na wengi na hawana nafaai 2015, ndo matendo yenu yote yatakuwa hadharani. Mtahama nchi?



Haya yote yanatokea kutokana na udhaifu wa chadema katika kulisolve swala hili.
Wapinzani wa chadema wanatumia weakness za chadema kuzidi kuisambaratisha.
 
SIRI YAFICHUKA SOMA HAPA A - Z KUTEKWA, KUTESWA KWA MWENYEKITI CHADEMA

Makongoro Oging na Haruni Sanchawa
MWENYEKITI wa Chadema wilayani Temeke, jijini Dar Joseph Yona,33, ameeleza A-Z sakata la kutekwa, kuteswa kwake na vijana sita wakati akienda nyumbani kwake Mtoni kwa Azizi Ally.
Mwenyekiti wa Chadema wilaya ya Temeke na Mjumbe wa Kamati Kuu ya chama hicho, Joseph Yona akipelekwa Kitengo cha Mifupa Muhimbili (MOI) kutoka wodini.
Akisimulia mkasa huo kwa mwandishi wa gazeti hili juzi Jumanne akiwa Hospitali ya Taifa, Muhimbili, Yona ambaye pia ni Mjumbe wa Baraza Kuu, Taifa Chadema alikuwa na haya ya kusema: “ Majira ya usiku nikiwa na baadhi ya vijana wa Chadema Tawi la Ukombozi lililopo karibu na kwangu maeneo ya Benki Klabu, Mtoni kwa Azizi Ally tulikuwa tukiongea.
“Ilipofika saa sita tukatawanjika mimi nikawa naelekea nyumbani, kabla sijafika mbali nikashitukia vijana sita wakinivamia na kunikaba kisha kunivua tisheti na kunifunga usoni, wakaniingiza katika gari ambalo walikuwa wamepaki pembeni.
“Nilipowauliza mnanipeleka wapi? Wakawa wanajifanya ni askari kwani walikuwa wanasema, ‘tumeshamkamata, tunamleta huko kituoni afande’, tukiwa njiani waliniambia niseme Zitto ni msaliti badala yake nikawaambia kuwa hilo waulizeni viongozi wa juu.


“Baada ya kuona tumesafiri kwa muda mrefu niliwauliza mbona hatufiki kituoni? Wakasema wewe ndiye tulikuwa tunakutafuta, utakiona cha moto, usipokufa utawasimulia wenzako. Walinipeleka mpaka kwenye msitu, baadaye ikafahamika kuwa ni Ununio, Tegeta wilayani Kinondoni. Huko walinipiga sana kisha kunitelekeza katika pori hilo nikiwa nimezimia.
“Baadaye nilipata fahamu nikajikokota kwa taabu hadi kwenye nyumba moja, nikagonga lakini hawakunifungulia. Nikaenda nyumba ya pili kugonga napo hawakunifungulia. Nyumba ya tatu nilipoigonga wakanifungulia. Walinishangaa na kuniuliza kulikoni umelowa damu? Nikawaeleza kilichonipata.
“Watu hao waliwasiliana na polisi ambao walikuja na kunichukua mpaka hapa Muhimbili nilipofanyiwa uchunguzi nikahamishiwa Taasisi ya Mifupa na Mishipa ya Fahamu (Moi). Lakini kule porini wale watekaji walichukua vitu vyangu kama vile simu mbili na pochi yenye fedha na waliondoka nazo.”
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi wa Temeke, SACP Engelbert Kiondo akiongea na mwandishi wetu ofisini kwake alikiri kutokea kwa tukio hilo. “Msako mkali unaendelea ili kuwabaini na kuwakamata wale waliohusika na unyama huo ili wafikishwe mahakamani,” alisema Kiondo
 
mimi katika vitu nisivyoamini katika hii bongo muvi ni hivi.
1.haiwezekani mtu akatekwa ba kuchubuliwa usoni kama kaanguka na baiskeli halafu atupwe vichakani alale hapo mpaka wapiga picha waje.
2.haijawahi watekaji wakabishana na waliyemteka ambaye wanafahamiana na kuchubua usoni(badala ya kumuua).
3.kwa vile limeshaingia mikononi mwa director wa muvi ssp kova linakosa uhalali kama la dr uli.
4.kama ulimboka alitupwa mabwepande akiwa hoi bin taaban na yona ametupwa ununio akalaa hapo mpaka waandishi wa habari wakaja na alipofikishwa hospitalini akaishia opd ana mengi ya kutueleza kuhusu hiyo tamthilia.

namalizia kwa kumwambia kova kuwa historia anayoitengeneza ndani ya jeshi letu la polisi itamhukumu kabla hajaonja mauti.
Tafuta ile video ya Lwakatare utagundua ukweli,kuna sehemu Lwaka anasema lengo ni kuwatisha.Tafakari msukule
 
sasa tumuamini nani aliyetekwa akapigwa nusu kufa au wewe brother ambaye hata eneo la tukio hukuwepo???

tujadili ya msingi, namna gani tutatoka kwenye hili tope kabla ya uchaguzi 2015... haya yakutekana yameanza miaka miwili hii,, upinzani ulikuwepo toka 1995, kabla CDM haijawa na nguvu,, NCCR walikuwa na nguvu tena naweza sema kuliko CDM lakini hatukusikia utekaji huu ambao mnasema unaratibiwa na CCM..
me nafikili kunakitu kipya ndio kimekuja nahizi fikra,, kwa sababu wengine ni walewale wa zamani ambao wangefanya haya toka zamani, WATZ kwa sasa tunafikili na tunafanya simple research penye kweli tunaona penye sanaa tunaona.
 
Siku zote Mungu husimama na wenye haki..kamwe haitakuja kutokea Giza(CCM) likawa bora kuliko nuru(CHADEMA)..watafanya hila zao,lakini siku zao zinahesabika..ipo siku kila hila wanayoitumia itakuwa ni silaha ya kuwaangamiza..
 
Nilimwangalia Kova juzi ITV ilibidi nicheke tu, yaani Kova anaona watanzania ni mazuzu ya kupokea chochote kile bila kutafakari. Hii muvi nishaiona tangu mwanzo wake. Heko kwa MOI kwa kutoendekeza propaganda za kijinga.
 
Hawa akina kova, kamhanda, shilogile, mulongo, na wengine woote! wanahangaika kutafuta vyeo kwa bos wao.
 
Hivi wewe mtoi na huyo alieshambuliwa nani mkweli?

MOHAMED MTOI hana tofauti na durex au raflyder, anajipendekeza kwa BABU ili mradi mkono uende mdomoni, shame wauaji wakubwa DJ na BABU ka mkono
 
ccm ndio tatizo....hizi ni zaidi ya siasa maji taka.
 
Kinachonishangaza Abdsalom(?) Kibanda Mhariri wa Mtanzania ni mhanga wa matukio haya ya ugaidi ya kuteswa na kya CCM.

Kitu ambacho sielewi leo anakuwa msatari wa mbele kushadadia huu ugaidi wa CCM!!.. Asifikiri kwamba CCM wamemusahau, wanaweza kumrudia na kumung'oa hilo jicho la pili walilombakishia, labda ndiyo atajifunza. Maana watu wengine wana vichwa vigumu vya kujifunza kama nazi.

Wait and see the filamu has began.
 
Mtoi, hivi unafikri Buku saba Project wanaweza kukukubali ukweli? hata ungewatafunia na kuwamezesha bado wangejitapisha tu, ukweli uko hapo facts zipo wazi, it is up to them to agree or disagree. The later is better for them kwa kuwa they will be paid ........

lol Elli najua buku7 nao ni binadamu nafikiri ukweli wanaukubali rohoni, ila akili zao zinakataa ukweli kwa ajili ya pesa. Ni jambo liliowazi kabisa kuwa hii movi walitengeneza, na waliotengeneza waliacha makosa mengi hasa kwenye picha. We uliona wapi mtu kula kichapo kile na damu kuchuruzika kiasi kile lakini cha ajabu si shati wala alipokuwa amelala yaani kwenye box kuna hata tone la damu.
 
Siasa za Tanzania zimejaa maji taka tu. Ndio maana umaskini unaongezeka maana tunatumia nguvu nyingi kwenye mambo yasoyo na tija tunasahau yenye tija kama hayapo vile

safi sana short and clear,, kaka tuliowengi tunatumia nguvu nyingi kusaidia wanasiasa kwenda IKULU, halafu baadaye wanatutupa kule... tunasahau kuwa tunatakiwa tupush hawa watawala kwa nguvu wafanye yale yenye manufaa kwetu!!
 
Back
Top Bottom