Mpango mzima wa kuihusisha CHADEMA na ugaidi mpya huu hapa

Mpango mzima wa kuihusisha CHADEMA na ugaidi mpya huu hapa

Mohamedi Mtoi wewe kweli tambara la deki, ninguwa Mod ninge kupiga Ban, na upuuzi wako, Yaani hili nalo utummwa na mabwana zako au ndio kujipendekeza tu kwa Mtei.wewe tulia tu kifaranga, tuwashughulikie hawa MAGAIDI.
 
Last edited by a moderator:
Kova nae jana nimemsikia kwe vyombo vya habar anaongea kama alikuepo kwenye tukion..yaani anahadithia kama alishuhudia na sikwamba anatoa taarifa walipokea Polisi.
Lakini kikubwa nilichojiuliza ni pale Kova aliposema (mana si kwamba alikua anawasilisha kilichosemwa) kua mwenyekiti wa CDM Temeke alipopanda gari aliona mmoja wa waliomteka anamfahamu kabisa na hua anafanya nae kazi ndipo akamwambia;"wewe si 'fulani' nakufahamu hua tunafanya wote kazi kila siku..."?? ndipo hao jamaa wakamfunga kitambaa usoni ili asiendelee kuwaona. Kah..yaani mtu unajua kabisa unaeenda kumteka anakufahama vizuri na mnafanya wote kazi kila siku then unaenda nakujitambulisha kama polisi..alaf baada ya kukugundua ndio umfunike macho asikuone?hizi hadithi za Kova hizi.
Nashauri jeshi la Polisi mnapoandaa filamu kama hizi msimpe Kova wajibu wa kuongea na vyombo vya habar unless kama yeye ndie kichwa kuliko wote mliobaki.
 
Kova tunamjua siku nyingi.......anatafuta kuingia bongo movie baada ya kustaafu. Ila tatizo lake si mwerevu wa mambo kwani akiwa anatangaza sinema zake hujisahau kwani hata mtoto mdogo huuona ni uigizaji. Kova pole sana kwani hata fadhila unazotaka toka CCM hautazifaidi kwani soon unastaafu na ujue ukishavua magwanda hata ubalozi wa nyumba kumi hupati
 
Mtoi, nina maangalizo kadhaa kutokana na maelezo yako yanayojikanganya,

1. Chanzo -CDM Diaspora unategemea nini kama sio habari za upande mmoja...kwa sasa ni vema kumsikiliza bwana Yona kwanndiye mtekwaji na pia kwani kila Mbowe na Slaa wanapowasiliana na viongozi lazima wakushirkishe? kuna ukweli alionywa na uongozi kwamba aache mahusiano naZitto kwani hata sasa uongozi wa CDM umeagiza viongozi na wanachama kutoshirikiana na Zitto , Hili lina ukweli

2. Zitto na wenzake wamefukuwa kutokana na waraka wa kutwaa madaraka kinnyume na Katiba......Wewe unatueleza kwamba Mwakembe katangaza kugombea uenyekiti Temeke, je sio uhaini? Kileo kajhalalisha kwamba yeye ndiye mgombea mteule wa Ubunge Mwanga bila kufuata katiba....je nikweli hamna wana CDM wengine wenye nia....kama ambavyo mnasisitiza siku zote kwamba wagombea wafuate utaratibu uliopo kwenye katiba, au kuna wanaoruhusiwa kwenda kinyume?

3. Ni ngumu kutenganisha utesaji wa Yona na CDM,kama ilivyo ngumu kutenganisha utesaji wa Ulimboka na Serikali!


Pagija,

Katika watu ambao ni majuha,mazezeta na wapuuzi wewe ni nambari wahedi. Sijui ulisoma shule gani ambayo haikuweza kukuelimisha ili uweze kuutumia ubongo wako kufikiri tena kwa makini(to think critically). Kwa watu makini wenye fikira pevu watakubaliana na kile alichosema Mhe. Mtoi. Huo ndio ukweli wenyewe!

Ni watu wapumbavu tu kama Kova pamoja na wewe mnaweza kufikiri kuwadanganya Watz waliokwenda shule kwa propaganda na porojo kama hizi za kina Abhu Sayaf(propangadist wa Marehemu Saadam Hussein). Kwa watu wenye akili timamu hawawezi kukubaliana na upuuzi huu mnaotaka kuutetea ati CDM inahusika na kumteka huyu Bwana Yona. No body can beleive this rubbish and non-sense materials zinazoandikwa na Magazeti ya Watu wa CCM ili kuivuruga CHADEMA!!

Kwa simple reasoning akili tu inakuambia huyu jamaa Yona wala hakutkwe na yoyote. Haiewezekani wewe watu wajifanye polisi waje wakukute ati unakunywa kwenye klabu ya pombe saa 5.00 usiku wakukamate kwa madai ya kuupeleka Kituo cha Central. Polisi siku zote lazima wawe na sare na Vitambulisho na lazima wajitambulishe kabla ya kukukamata na kwanini wanakukamta.Polisi wenye kufuata maadili ya kazi lazima wajitambulishe kwa majina na ID zao na kama uko klabuni lazima au nyumbani kwako lazima wonyeshe warrant of arrest au search warrant kama wanatafuta kitu cha wizi au madawa ya kulevya n.k.

Kwa akili ya kawaida maelezo yote ya Yona ni urongo mtupu. Kitu kinachosikitisha ni kwamba kuna media zinatumiwa na wanasiasa hasa CCM kuwachafua wapinzani lakini pia hata mahasimu wao kisiasa ndani ya hiyohiyo CCM. Mtoi alivyodadavua habari ya Mtanzania kuhusiana na tukio fake la kutekwa ni ukweli mtupu kuwa Mhariri wa gazeti hili ametumika. Hivi ni mwandishi gani unawezaa kuandika habari inayohusisha pande pili zinazogombana hata kushirikiana kwakuongea na upande mmoja tu bila kuhoji maoni ya upande wa pili???Huu utakuwa ni ukanjanja wa kutupwa!!!


wandishi wa Mtanzania amedai kuongea na Yona baadaye akaongea na Zitto kuhusu utekaji huo huku akiwaacha viongozi waandamizi wa CDM ambao Yona anawatuhumu kuwa walimwita na kumtishia ajiondoe kwenye chama.Hiki ni kituko! Hawa viongozi wana simu zao zinajulikna kwanini hajawapigia kuwauliza kuhusiana na tuhuma hizo kama zina ukweli wowote?Yaani mwenyekiti wa mtaa aitwe na Katibu Mkuu wa chama au M/Kiti wa Taifa kwa jambo la kipuuzi kama hili hata kama lingekuwa na ukweli??? No way,siyo CDM.

Hata huyu Kova ni kibuyu tu. Nafikri kuna haja ya Watanzania kupiga kelele kuhusu huyu Afande Kova. Tumesikia kuhusu MIZIGO YA MAWAZIRI lakini pia kuna MIZIGO YA MAPOLISI aina ya kina Kova. Kova ni mzigo katika Jeshi la Polisi. Ninaomba kama IGP mpya Afande Mangu amfuatilie huyu Kova na Mapolisi wengine Mizigo ambao wananedelea kulidhalilisha Jeshi la Polisi. Kova mpaka leo hii hajakamata watesaji wa Dr. Ulimboka wala wa Absolom Kibanda pamoja na ushaidi na vielelezo toka kwa waathirika wenyewe yaani Ulimboka na Kibanda ukiacha vyanzo mbalimbali vya habari vilivo onyesha kuwa kuna watu toka Serikalini tena Ikulu, Usalama wa Taifa waliohusishwa na matukio haya lakini mpaka leo hakuna kitu.

Kuna tukio la Mkurugenza wa Usalama wa CHADEMA ndugu la Lwakatare kuhusishwa na UGAIDI wa kutengeneza kumteka ati kibanda mpaka leo kesi imedoda maana imekuja kubainika kuwa Kova alikuwa ameandaa Filamu ya maigizo kuwafurahisha wazee wake wa CCM!

Mimi namwuliza IGP Mangu hivi sheria ya Polisi katika ajira inazungumziaje kuhusu ajira ya watu wenye MAKENGEZA kama Kova kuajiriwa na Jeshi la Polisi???Sina hakika kama Kova anaona na kufikiri sawasawa na kama kwenye somo la KULENGA SHABAHA alipiga riasai ngapi kwenye 'BULL' au target!!!!Kova hafai hata kulinda kuku, hana sifa za uaskari polisi hata chembe. Kama IGP Mangu hataweza kumwondoa Kova Mzigo basi Wabunge wa CHADEMA wapeleke hoja Bungeni ya kutaka kuondolewa kwa Maafande Mizigo akiwemo aliekuwa RPC wa Iringa Michael Kamuhanda, RPC wa Arusha, RPC Morogoro na wengine mizigo ambao wameshindwa kusimamia Jeshi la Polisi kulinda Usalama wa Raia na badala yake Polisi ndiyo wamekuwa wauaji wakubwa. Hii lazima ihusishe na wale ma-RPC ambao wamesababisha Mawaziri 4 wa Kiwete kufutwa kazi kwa uzembe uliosababisha mpaka Wananchi na Mifugo wasio na hatia kuuawa kinyama.

Kazi kwako IGP Mangu.
 
Binafsi ninachofurahi ni kuwa MUNGU hamfichi mwongo au mfitini!siku moja haya yote yatajulikana na ukweli kuonekana wazi mbele ya macho ya watu wote. Baba Mungu twakukabidhi yote haya utuonyeshe UKWELI uko wpi.
 
Jamaa alijitaidi kukosa usingizi ili apost hii topic nathani alifikiri kuandika maneno mengi ndo ustadi bali ukweli oko pale pale, si Chama Bali viongozi wa Chama ndo waliandaa ughaidi dhidi ya kiongozi mwenzao, kisa anamkubali Zitto.
 
Ninachokiona sasa hivi ,Tanzania inaenda kuingia kwenye vita mbaya kuliko hata vita iliyowahi kutokea nchini Rwanda,hii yote inasababishwa na Rais tulienae kuwa na uwezo mdogo wa kutawala.Hana uwezo wa kukemea mawaziri wake pindi wanapofanya uharifu wa makusudi,mfano kwenye mauaji ya mwandishi wa habari wa chanel ten,wahusika ni askari wake,kama Rais amewachukulia hatua gani?hasa waziri husika;Kumekuwa na matukio mengi yanayofanana na hayo lakini Rais amekuwa kimya kana kwamba yeye ndiye anaewatuma wauaji ama waharifu.Hata mahakama zimekuwa zikitenda kazi chini ya kiwango ama kutokutenda haki ni kwa sababu ya udhaifu wa Rais alieko madarakani,ikiwa haki haitendeki kwa wsiokuwa upande wa Rais,ujue siku wakisema inatosha, si polisi wala jeshi litakalosimama na umma.Tuombe Mungu atunusuru ili huyu Rais amalize muda wake kabla ya wale wanaonyimwa haki yao hawajafika mwisho wa kuvumilia,na tuombe tupate Rais atakaeiongoza nchi bila kuangalia matabaka,mwenye kusimamia haki sawa kwa watu wote bila kujali cheo cha mtu ama wadhifa alionao saerikalini au kwenye jamii inayomzunguka.MUNGU IBARIKI TANZANIA NA WATU WAKE.
 
Watashindwa tu hao magaidi wa ccm,walianza kitambo lakn wakashindwa kwa aibu! MUNGU YU PAMOJA NA CDM!
 
SIRI YAFICHUKA SOMA HAPA A - Z KUTEKWA, KUTESWA KWA MWENYEKITI CHADEMA

Makongoro Oging na Haruni Sanchawa
MWENYEKITI wa Chadema wilayani Temeke, jijini Dar Joseph Yona,33, ameeleza A-Z sakata la kutekwa, kuteswa kwake na vijana sita wakati akienda nyumbani kwake Mtoni kwa Azizi Ally.
Mwenyekiti wa Chadema wilaya ya Temeke na Mjumbe wa Kamati Kuu ya chama hicho, Joseph Yona akipelekwa Kitengo cha Mifupa Muhimbili (MOI) kutoka wodini.
Akisimulia mkasa huo kwa mwandishi wa gazeti hili juzi Jumanne akiwa Hospitali ya Taifa, Muhimbili, Yona ambaye pia ni Mjumbe wa Baraza Kuu, Taifa Chadema alikuwa na haya ya kusema: “ Majira ya usiku nikiwa na baadhi ya vijana wa Chadema Tawi la Ukombozi lililopo karibu na kwangu maeneo ya Benki Klabu, Mtoni kwa Azizi Ally tulikuwa tukiongea.
“Ilipofika saa sita tukatawanjika mimi nikawa naelekea nyumbani, kabla sijafika mbali nikashitukia vijana sita wakinivamia na kunikaba kisha kunivua tisheti na kunifunga usoni, wakaniingiza katika gari ambalo walikuwa wamepaki pembeni.
“Nilipowauliza mnanipeleka wapi? Wakawa wanajifanya ni askari kwani walikuwa wanasema, ‘tumeshamkamata, tunamleta huko kituoni afande’, tukiwa njiani waliniambia niseme Zitto ni msaliti badala yake nikawaambia kuwa hilo waulizeni viongozi wa juu.


“Baada ya kuona tumesafiri kwa muda mrefu niliwauliza mbona hatufiki kituoni? Wakasema wewe ndiye tulikuwa tunakutafuta, utakiona cha moto, usipokufa utawasimulia wenzako. Walinipeleka mpaka kwenye msitu, baadaye ikafahamika kuwa ni Ununio, Tegeta wilayani Kinondoni. Huko walinipiga sana kisha kunitelekeza katika pori hilo nikiwa nimezimia.
“Baadaye nilipata fahamu nikajikokota kwa taabu hadi kwenye nyumba moja, nikagonga lakini hawakunifungulia. Nikaenda nyumba ya pili kugonga napo hawakunifungulia. Nyumba ya tatu nilipoigonga wakanifungulia. Walinishangaa na kuniuliza kulikoni umelowa damu? Nikawaeleza kilichonipata.
“Watu hao waliwasiliana na polisi ambao walikuja na kunichukua mpaka hapa Muhimbili nilipofanyiwa uchunguzi nikahamishiwa Taasisi ya Mifupa na Mishipa ya Fahamu (Moi). Lakini kule porini wale watekaji walichukua vitu vyangu kama vile simu mbili na pochi yenye fedha na waliondoka nazo.”
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi wa Temeke, SACP Engelbert Kiondo akiongea na mwandishi wetu ofisini kwake alikiri kutokea kwa tukio hilo. “Msako mkali unaendelea ili kuwabaini na kuwakamata wale waliohusika na unyama huo ili wafikishwe mahakamani,” alisema Kiondo
Kova alishaianza hii movie,peleka pale central mka-edit..
 
jamaa mjinga anataka kutufanya wajinga, jipendekeze lakini wachaga hawatakupa cheo
 
Simpendi zitto pamoja na wafuasi wanafki wa CCM,subirini,mtatoa hesabu za matendo yenu maovu mbele ya KITI CHA ENZI.
Mungu ibariki Chadema.
 
naona alipeleka kule ----------- forum akakosa mashabiki
 
Nimekuuliza wewe na aliyeshambuliwa nani anasema kweli?nashangaa unanipa hekaya zile zile tulizozizoea hapa,mlituletea hekaya kama hizi kwenye bomu la Arusha lakini mpaka sasa mmeshindwa kuthibitisha lolote,halafu akili zenu za kulamba viatu mnadhani kila mtu anaepingana na mawazo yenu basi ni ccm akili za panya hizo,

unapo andika weka ushabiki pembeni theni tumia akili chawa wewe,swala la arusha nani kashindwa kutekeleza wajibu wake?raisi wako angeunda tume ya majaji si mngesha pata jibu zamani san unafikiri kwa nini raisi wako aliogopa kuunda hiyo tume?? Mlishaambiwa ushahidi upo hata leo mkiutaka upo mshauri raisi wako ainde tume aliyo ambiwa uone kama ccm hamjainamisha vichwa chini,achakujibu hoja nzito kwa majibu ya kubuni mamba wewe tumia akili,, mbinu zenu ccm hakuna ambazo zitafanikiwa bila kugundulika mijusi nyie.
 
Niuchambuzi wakina na wenye mantiki ukiachilia mbali kuwa umetolewa na chadema diaspora. Unganisha matukio na chambua kwa pande tatu kiaakili, nadharia na dhana. Haiwezekani wana M4C kumpiga mtu huku wakimwambia kwanini anamuunga mkono zito alafu wamwachia, je unataka niambia kuwa ni kosa kubwa waliodhamiria kulifanya ili iwe ujumbe kwa wote wanaomuunga mkono zito?Asante Mohamedi Mtoi kwa kuliona hili, wenye kutambua mchele na chuya tayari tumeisha tambua nini kinachoendelea.
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom