Mpango mzima wa kuihusisha CHADEMA na ugaidi mpya huu hapa

Mpango mzima wa kuihusisha CHADEMA na ugaidi mpya huu hapa

chadema mkubali kuwajibika katika hili acheni kutafuta njia ya kuhalalisha maovu kwa kutunga mambo
 
Chadema ni magaidi wanatafuta dola kwa nguvu na hawato pata,nawashanga vijana mmegeuka al sahaf wakati ukweli unajulikana au ndo maisha bila unafiki hayaendi?ukiona mwenzio ananyolewa nawe tia maji.hao majasusi mnao wafuga ni wakazi gani?.




Namtaka Mama Wa Kifaranga.:yell:
 
Kutekwa na kuteswa Mwenyekiti wa Temeke; Mpango mzima wa kuihusisha CHADEMA huu hapa;

Jana majira ya saa 3.30 asubuhi, watu wapatao watano ambao ni wanachama wa CHADEMA mamluki wa Timu ya Zitto na CCM, wakiwa eneo moja la ofisi ya umma wakisubiri huduma ya muhimu sana, walipokea simu ya taarifa kuwa Mwenyekiti wao wa chama wilaya ya Temeke, Josephat Yona Patrick alikuwa amekutwa mahali fulani Dar es Salaam baada ya kutekwa, kuteswa na kuumizwa na watu wasiojulikana.

Wale watu mara tu baada ya kupokea habari hizo, wakamtafuta mtu waliyekuwa wakimwita kwenye simu jina la Mchange (wala si mwingine ni Mhange huyo huyo anayefahamika katika masuala hayaya circles za usaliti dhidi ya CHADEMA).

Wakamwambia habari hiyo (inavyoonekana yeye alikuwa tayari anaijua na alikuwa mahali fulani kwa mwanasheria). Akawauliza wanaweza kumtaja mtu (a watu) yeyote wanayetaka ahusishwe kwenye tukio hilo kisha afunguliwe kesi. Mtu ambaye akihusishwa itakuwa rahisi kwa viongozi wakuu wa chama na hatimaye chama kizima kuhusishwa kwenye tukio hilo.

Wale watu wakamwambia ili kumalizana na ‘biashara’ ya CHADEMA kabisa kwa kuwahusisha viongozi na hatimaye chama kizima katika tukio hilo ambalo linaweza kukuzwa na kuoneshwa kuwa ni UGAIDI, wako tayari kumtajia majina ya watu wawili ambao wamekuwa wakikihami na kukitetea sana CHADEMA Temeke, hivyo ni kikwazo kwa mikakati yao ya kukihujumu CHADEMA katika eneo hilo.

Kama inavyojulikana kwa upande wa Dar es Salaam, mikakati ya kuihujumu CHADEMA imekuwa ikifanyika kwa kiasi kikubwa sana Temeke.

Wale watu wakamtajia huyo mtu waliyekuwa wakimtaja kwa jina la Mchange, majina ya watu wawili, Mzee Salum Zinga na Bernard Mwakyembe. Wote hawa ni makamanda kweli kweli hapo Temeke, kiasi kwamba Mwenyekiti wa sasa wa CHADEMA Wilaya ya Temeke amekuwa akimhofia sana Mwakyembe kwamba anaweza kuchukua nafasi yake wakati wa uchaguzi ujao wa ndani ya chama hicho.

Baada ya kumtajia majina hayo, wakamwambia wanapitia ofisi ya wilaya ya chama hicho mara moja, kisha wakutane kituo cha polisi ili wakafungue malalamiko dhidi ya watu hao wawili kuwa wamehusika na tukio la kutekwa, kuteswa na kuumizwa kwa mwenyekiti huyo. Mpango mzima ukawa umekamilika na ukatekelezwa.

Tunavyozungumza hapa sasa tayari Mzee Salum Zinga ambaye ni Mwenyekiti wa Wazee Jimbo la Temeke ameshakamatwa na polisi na sasa jeshi hilo linamtafuta Mwakyembe. Lakini kwa namna ambavyo mpango huo umepangwa na utakavyotekelezwa, lengo ni kuwafikia viongozi wa juu.

Mpango huo uliozungumzwa na watu hao watano pale Temeke kwa kuwasiliana na Mchange ndiyo msingi wa kauli za Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Suleman Kova, kutamka kwa kuihusisha CHADEMA huku akijigamba kuwa watamkamata mtu yeyote bila kujali cheo chake. Akilenga viongozi wakubwa wa chama hicho.

Huyo Kova ambaye kwa sababu ameshajitambulisha kuwa ni bingwa wa kugeuza matukio haya ya ukatili kuwa ni ‘filamu’ ya kuficha ukweli na kuanza kusaka uongo, hatuna haja ya kumjadili zaidi ya hapo. Ila ajue tu kuwa mpango mzima unajulikana.

Ndiyo maana sehemu ya mpango huo ni kumlazimisha Yona arudi na kulazwa Moi ambako alikuwa ameagwa jana hiyo hiyo baada ya kubainika hana majeraha makubwa na angetakiwa kurudi baada ya wiki mbili. Hiyo ilikuwa ni baada ya CHADEMA kuwa wamesimamia matibabu yake, ikiwemo kumlipia gharama za hospitali na usafiri kumpeleka nyumbani.

Akiwa hapo hospitalini amezungumza na vyombo vya habari kwa namna tofauti tofauti, kwa mtazamo wa kila chombo na kadri ya maelekezo…

Mpango mzima unaandaliwa pia kupitia vyombo vya habari;

Angalia kutoka magazetini

Kama mlivyoona leo kwenye kurasa za mbele za magazeti yote yaliyotoka leo, habari hii imepewa uzito mkubwa, ingawa kwa namna tofauti tofauti, kulingana na uwezo, sera za vyombo vya habari na MALENGO ya chombo husika, hasa katika kufanya kazi za watawala dhidi ya CHADEMA.

Lengo lingine ni kubeba agenda za makundi ya kuwania urais ndani ya CCM, ambayo CHADEMA ndiyo tishio pekee la wao kufanikiwa kwenda ikulu, hivyo yanafanya kila jitihada kukiumiza chama hicho kwa propaganda nyepesi kama ya tukio hilo.

Kwa upande wako fanyia kazi PICHA zilizotumika leo katika magazeti yote. Zimepigwa wakati gani? Eneo gani? Saa ngapi huyo mpiga picha maalum alikuwa ameandaliwa kwa ajili ya kupiga hizo picha zinazooenakaana kupigwa kwa ustadi na kifaa kizuri? Kuna maswali mengi sana ukizingatia kuwa picha zilizotumika katika habari hiyo ni za aina moja! Nani kazipiga?

Hapa tunaweza kujadili habari kutoka katika magazeti kadhaa;

Mtanzania

Gazeti hili limeipatia habari hii kichwa kisemacho INATISHA. Ndani ya habari gazeti hilo kwa malengo linalojua yenyewe, labda likiongozwa na kile kinachoweza kuitwa aina ya weledi wa aina yake wa taaluma ya habari, sera za chombo hicho na malengo ya wamiliki, limewahusisha viongozi wa CHADEMA katika tukio hilo kwa hali ambayo inaacha maswali mengi sana.

Mathalani kwenye moja ya nukuu zake, wamemnukuu Yona akisema

“Bernard na Mwakyembe walinisalimia na kuondoka, baada ya hapo, wakaja watu wengine wane ambao siwajui, wakajitambulisha kwangu kuwa ni polisi wanatoka kituo cha kati, hivyo basi wananihitaji kwa ajili ya mahojiano.”

Waandishi wa gazeti hili wangekuwa na nia ya kufanya uandishi unaowajibika kwa jamii, wangefanya kazi yao kidogo tu wangebaini kuwa Yona katika hilo alikuwa amewadanganya au amewaambia kitu ambacho kinahitaji kufanyiwa kazi zaidi.

Kwa sababu kama umefuatilia mtiririko wa taarifa hii, kuna mtu anaitwa Bernard Mwakyembe (mtu mmoja), lakini hapa Yona ametaja kwamba hao ni watu wawili tofauti. Gazeti lilipaswa kufanya kazi yake badala ya kutumika kuwa karatasi ya kufanyia propaganda za CCM dhidi ya CHADEMA.

Katika aya mbili zinazofuata ndiyo zinaliacha gazeti hilo uchi kabisa kwamba limeamua kutumika kwenye mkakati unaoandaliwa na CCM kupitia vyombo vya dola. Limeandika hivi;

“Tulibishana sana tena ni muda mrefu, mwisho nikawaambia wanionyeshe kibali cha kunikamata lakini walinijibu kuwa wao ni polisi, napaswa kutii amri kama kuna mahojiano zaidi yatafanyika kituoni, nikapanda gari lao na kuondoka,” alisema Patrick.

Soma na aya inayofuata ambayo gazeti hilo limeandika kama vile lilikuwepo wakati tukio linatokea. Kwa sababu lilipaswa kuandika maneno ya Yona ni madai…allegations.

“Alipohoji sababu ya watu hao kujitambulisha ni polisi wakati anawajua kuwa si wanausalama, walianza kumshurutisha kuingia ndani ya gari alipogoma walimsukuma kwa nguvu ndani ya gari hilo na kumwambia kuwa wanampeleka kituo cha kati.”

Aya hizo mbili zilitosha kabisa kuwashtua waandishi au wahariri makini kuwa chanzo cha habari wanachozungumza nacho si cha kuaminika au kinazua maswali mengi mno.

Mtu aliyesema dakika kadhaa tu zilizopita kuwa walikuja watu wengine wanne hawajui, wanajitambulisha kuwa ni polisi, akawahoji vitambulisho, wakashindwa kutoa, akabishana nao sana maeneo ya baa (hakuna mtu aliyesikia?), cha ajabu akakubali kuondoka nao wakati yeye hawajui ni akina nani, ghafla tena anasema kuwa anawajua kuwa si wanausalama. Kuna maswali mengi sana?!

Kwa ujumla habari nzima ya Mtanzania kuhusu tukio hili, ilistahili kuandikwa na yale magazeti ‘crap’ ya ajabu ajabu yaliyoko mtaani, chini ya waandishi na wahariri ambao hawajui wala hawathamini chembe hata moja ya maadili achilia mbali weledi wa kitaaluma.

Wameandika habari ile badala ya kutumia madai ya nafsi ya tatu umoja, wao wameandika kama vile walikuwepo hatua kwa hatua na mlalamikaji Yona, lengo zima ikiwa ni kuwahusisha viongozi wa CHADEMA na chama hicho katika sakata zima. Je Mtanzania maslahi yao katika hili ni yapi? Bila shaka ni makubwa sana.

Angalia aya hizi zilivyoandikwa kwa makusudi, kimkakati;

Patrick ambaye ni rafiki wa karibu na aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu wa CHADEMA, Zitto alisema kuwa mgogoro wake na viongozi wakuu wa chama hicho ulianza tangu alipoitisha mkutano na waandishi wa habari wa kuitaka Kamati Kuu ya chama hicho kuitisha mkutano wa kujadili suala la kina Zitto, Samson Mwigamba na Dk. Kitila Mkumbo.

“Niliitisha mkutano ule ili kuwaambia viongozi wa CHADEMA kujadili suala la kina Zitto, Kitila na Mwigamba ndani ya chama na si kuwavua uanachama kama ilivyojitokeza jambo ambalo lilipingwa na viongozi wa chama hicho,” alisema Patrick.

Alisema, kutokana na hali hiyo viongozi wa chama hicho akiwemo Mwenyekiti wake Freeman Mbowe na Katibu Mkuu, Dk. Willibrod Slaa alimwita na kumuambia aache urafiki na Zitto la sivyo watamfukuza uanachama. (Walimwita lini, wapi kwa namna gani, hivi kweli viongozi wa juu namna hiyo wanaweza kumwita kiongozi wa wilaya hivi hivi tu, hicho chama si CHADEMA labda CHAUMA na viongozi hao hawawezi kuwa Mbowe wala Slaa, lakini kibaya kabisa, gazeti wala halikuwatafuta kutaka kujua upande wao na kupata hata ukweli. Uandishi wa hatari sana huu)

“Waliniita na kuniambia niachane na Zitto, nilipinga ndipo waliponiambia nijiondoe ndani ya chama hicho, niliendelea kupinga,” alisema.

Alisema kutokana na hali hiyo, viongozi hao walimwambia aitishe mkutano wa Kamati ya Utendaji ya Wilaya na kuwaambia wajumbe wa kamati kuwa yeye si rafiki wa Zitto na kwamba hawezi kumuunga mkono kwenye harakati zake, lakini aliendelea kukataa suala hilo. (Hivi gazeti makini linaweza kunukuu uongo kama huu na kusema limeandika habari kwa ajili ya watu kusoma. Kuna tofauti gani na magazeti ya Yule jamaa mtunga hadithi).

“Tangu nilipoitisha mkutano wa waandishi wa habari wa kupinga uamuzi wa kuwavua uanachama akina Zitto, Mwigamba na Kitila, nimekuwa kwenye mvutano mkubwa na viongozi wangu wa juu, nimepokea vitisho vingi ambavyo nilivirekodi kwenye simu yangu ya mkononi waliyoichukua,” alisema Patrick.

(Kwa trend ambayo chanzo hicho kimeonesha tanguy huko juu, huna haja ya kwenda hata darasa moja kujua kuwa huu ni uongo mkubwa unaosemwa na mtu anayejifunza kuzalisha fitna na majungu, lakini pia mwanafunzi wa kutengeneza mgogoro, lakini kikubwa kupika kesi. Mathalani mhariri makini hawezi kupitisha uchafu kama huu uwe habari, angeuliza tu, huyo Yona alifanya huo mkutano lini?, Ulihusu nini? Je ni kweli ulihusu kupinga kuwavua uanachama watu hao? Kwa nini kutumika kuandika uongo?).

Aliongeza, suala hilo liliendelea hadi Dk. Slaa na Mbowe walipomwita na kumlazimisha aitishe tena kikao kingine cha kamati tendaji ili atangaze kujiuzulu mwenyewe nafasi yake kabla ya kumfukuza uanachama, jambo ambalo alilipinga tena. (Umakini wa waandishi na wahariri wa gazeti hilo haukuwatuma kuona umuhimu wa kuwatafuta viongozi hao walau wahalalishe huo uchafu walioamua kuuita ni habari ya kuwapelekea Watanzania. Hii ni hatari sana.)

“Dk. Slaa aliniandikia barua ya kunitaka niitishe mkutano nilipoona kelele zinazidi nikaamua kuitisha lakini wajumbe wa kikao nilichoitisha kwa pamoja wakaniunga mkono na kusema wana imani na mimi, hivyo basi hawataki niondoke.

“Baada ya hapo, Dk. Slaa akaniandikia barua na kuniambia kuwa kikao nilichoitisha ni batili na kwamba wanatakiwa kuitisha kuitisha kikao kingine Januari 10 mwaka huu.”

Kwa ujumla habari nzima ya Mtanzania ni ----. Na kuonesha dhahiri malengo na nia ovu waliyonayo dhidi ya CHADEMA kupitia tukio hilo la kusikitisha la kutekwa na kuteswa kwa Yona, gazeti hili ambalo limeandika mengi sana ya KUUMIZA, yanayokiuka maadili na weledi wa uandishi, likimnukuu mwenyekiti huyo akisema uongo dhidi ya Mbowe na Dk. Slaa, halikuwatafuta viongozi hao, lakini likamtafuta Zitto Kabwe.

Wanaandika hivi;

“Nikiangalia tukio langu na mgogoro uliopo ndani ya chama najua nimeumizwa kwa ajili ya kumtetea Zitto, kwa sababu nimekuwa nikipokea vitisho kutoka kwa viongozi wa juu wa chama na M4C,” alisema.

Kukamilisha mpango huo wa spinning ya kuwahusisha viongozi wa CHADEMA na hatimaye chama kizima katika sakata hilo, Zitto akatafutwa na akasema hivi;

Akizungumzia tukio hilo, Zitto amesema vurugu kamwe siyo suluhu ya siasa nchini na kwamba ni kitendo kinacholenga kuwaingiza watu katika woga na kuwatisha.

“Haya ni matendo ya kikatili na ya kumuogopesha kutokana na kupinga baadhi ya mapendekezo ya upande wa baadhi ya viongozi Kamati Kuu ya chama.

“Natoa changamoto kwa viongozi zote wa Chadema kwamba sasa wakanushe kuwa vurugu siyo silaha yao katika siasa,” alihitimisha Zitto.

Huyu mtu tayari alishajua na kuhitimisha kuwa viongozi na chama chake kinahusika na tukio hilo? Kwa nini anawahi kuhitimisha kuwasukumia tukio zito kama hilo ambalo linaweza kuharibu kabisa chama chake ambacho eti anataka kuwa mbunge na kiongozi wake. Au ni mwendelezo wa mkakati ule ule, wakakutanishwa kwenye kipindi cha Star tv asubuhi yeye na Mwigulu, Mwigulu Nchemba akajifanya anatoa habari ya ugaidi wa CHADEMA?

Habari za kiuchambuzi juu ya mkakati huu wa kutaka kurudisha taswira ya ugaidi na kuihusisha CHADEMA na matukio ya vurugu yanayohusisha umwagaji wa damu ikipangwa kwa ustadi na wale wale, kwa mtindo ule ule, kwa malengo yale yale, zitaongezwa baadae katika andiko hili;

Chanzo:Chadema diaspora.

Dj baba freelady TEAM at work
 
LOWASA Vs ZITTO KABWE NDANI YA VYAMA VYAO VYA SIASA
Watu Wanamfananisha Lowasa na Zitto, Wanasema Kama Lowasa Akihama CCM au Asipoteuliwa kuwa Mgombea Uraisi 2015 kwa Ticket ya CCM Basi CCM Itapasuka Vipandevipande na Wengine Kusema Itakufa Kabisa Kama Inavyopasuka Chadema na Kuelekea KIFO kwa sasa. Ifahamike ya Kwamba Vijana wa CCM na Wana CCM kwa Ujumla ni Tofauti Kabisa na Vijana wa Chadema na Wanachadema kwa Ujumla.Vijana wengi wa Chadema Walijiunga na Chadema Kwa Sababu ya Kuvutiwa na Zitto Kabwe, Uwezo na Umahiri Mkubwa Aliokuwa nao Katika Kujenga Hoja na Kuibua Kashfa,Siri Nyingi za Mafisadi.Hawakuwa na Malengo Binafsi ndani ya Chama na Siasa kwa Ujumla
Vijana wengi wa Chadema na Wanachadema kwa Ujumla Walijiunga na Chadema kwa sababu Kuu Zifuatazo
1. Walivutiwa na ZITTO KABWE, Dr Willbroad Slaa,Tundu Lissu au John Mnyika
2. Wanahasira na Serikali juu ya Kushindwa Kutatua Maslahi yao Binafsi
3. Walivutiwa na Chadema kwa Kuibua Kashifa za MAFISADI ie EPA, MELEMETA….
4. Waliongopewa ya Kwamba Chadema Inawapenda Sana Vijana na ni Mkombozi wa Taifa
5. Ndio Chama cha Upinzani Kilichokuwa na Nguvu Miaka ya 2009-2010…,Hivyo watu wanaopenda Upinzani Wakajikuta wamejiunga na Chadema
6. Wengine wamejiunga na Chadema kwa Sababu tu wao ni WACHAGA,Wanaamini Chadema ni Chama Chao
Vijana wengi wa CCM na WanaCCM kwa Ujumla Wamejiunga na CCM kwa Sababu Kuu Zifuatazo
1. Mapenzi yao ya Dhati na CCM,
2. Wana Malengo ya Kuwa Viongozi wa Kisiasa na Serikali wa Sasa na Badae
3. Nguvu ya Kisiasa na Kimtandao ya CCM ndani ya CCM na Serikali
4. Nafasi za Kiungozi ndani ya CCM ni Nyingi sana Ukilinganisha na Vyama Vingine vya Siasa
5. Nafasi ya CCM Kushinda Uchaguzi Mkuu na Kuunda Serikali ni Kubwa Kuliko Vyama vya Upinzani,Hivyo wana Matumaini ya Kuwa Sehemu ya Serikali
Ukitazama Sana Sababu Hizo Hapo Juu Utagundua ya kwamba Hata Lowasa Akihama CCM Basi Atahama yeye na Familia Yake na Hakuna MwanaCCM Atakaemfuata.Lowasa Atakuwa Raisi wa Tanzania Kama Kamati Kuu ya CCM na NEC Wakipendekeza Jina Lake na Kushinda Katika Kura za Maoni na Si Vinginevyo.Hata Kama Lowasa Hatashinda kwenye Kura za Maoni au Akakatwa Jina Lake Hata HAMA CCM, Atabaki CCM na Kuendelea Kuwa Mwanachama na Kiongozi wa CCM.
Vijana wa CCM na Wana CCM kwa Ujumla Wanakipenda Chama na Si Mtu Ndani ya Chama,Mimi Nawapenda Sana Viongozi wa CCM Wazalendo,Wanaowajali na Kupigania Maslahi ya Watanzania Lakini Wakihama CCM SINTOWAFUATA WAENDAKO,Nitabaki kuwa LOYAL na CCM Maana Kila Mtu Anamalengo yake ndani ya Chama cha Siasa,Kama Unamfuata Mtu Huwezi kuwa Stable Maana Umejenga Imani yako kwa Mtu na Si Chama.
FAHAMU
CCM Imejengwa Juu ya Mwamba,Ni Imara sana,Mizizi yake ni Mirefu na Imara Mno
CCM Inatawala Leo, Itatawala Kesho na Kuendelea Kutawala Mpaka Kitakapopatikana Chama sahihi Ambacho ni Mbadala wa CCM Lakini Sio Hivi Vyama vya KIKABILA…
CCM Inawajali Wazee na Vijana Hivyo Inapata Baraka za Pande Zote Tofauti na Vyama Vingine vilivyo Watenga Wazee na Kuona ni Watu waliopitwa na Wakati.

KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI…
 
Chadema ni magaidi wanatafuta dola kwa nguvu na hawato pata,nawashanga vijana mmegeuka al sahaf wakati ukweli unajulikana au ndo maisha bila unafiki hayaendi?ukiona mwenzio ananyolewa nawe tia maji.hao majasusi mnao wafuga ni wakazi gani?.




Namtaka Mama Wa Kifaranga.:yell:

wewe ndiyo umeandika madudu gani ?
 
CCM na CDM mtaua waTz .Hivyo vita vyenu zinazoumia ni nyasi.Mungu awachunguze na awafatilie.
 
Haya yote yanatokea kutokana na udhaifu wa chadema katika kulisolve swala hili.
Wapinzani wa chadema wanatumia weakness za chadema kuzidi kuisambaratisha.
 
Katika vitu ambavyo serikali ya CCM imefanikiwa ni kuharibu mfumo wa elimu yetu, wengi wamekuwa na ubutu wa kufikiri na maskini ya Mungu hata kuunganisha nukta.

1. habari iko wazi hapo juu, mwishoni nimeweka chanzo. taarifa au habari yoyote ikiwa na chanzo chini maana yake sio ya mletaji bali mletaji amekuwa mjumbe tu aliye beba ujumbe baada ya kuona mantiki.

2. Umeshindwa hata kuunganisha nukta walau kwa kurejea kwenye kesi ambazo CHADEMA ilishaingizwa kwenye ugaidi na baadaye kushinda. Hukumbuki ulioitwa ugaidi wa Lwekatare na Kileo?! kesi ziliiishaje na kwa nini ziliitwa za ugaidi? Je hii nayo haiwezi kuitwa ya ugaidi kama zile nyingine ili kuhusisha viongozi wa juu wa chama na ugaidi kama walivyo fanya awali?

3. Umeshindwa hata kukakavua na kudadavua bongo lako na kujiuliza kwa nini baadhi ya magazeti kwenye uchambuzi wa hii kilicho itwa mpango wa kuihusisha CHADEMA na ugaidi yamejichanga kwenye maelezo ya mhanga (Au maskini ya Mungu ume comment bila kusoma kama wale jamaa zako (B7FC?)

4. Kwa nini Kovo amekimbilia kuihusisha CHADEMA bila hata kufanya uchunguzi wa kitaalamu nawa kina?!, Je Kovo akisimama na kuanza hekaya za ugaidi dhidi ya CHADEMA umepa Moral integrity kwa kiasi gani? (Rejea kwenye tukio la Ullymboka na ile filamu yake)

5. Je, haya matukio yanayotokea ya watu kutekwa niya kigaidi?! Kama jibu ndio kwa nini serikali inaruhusu ugaidi utokee halafu kuna kuwa na nguvu ya soda ya kukihusisha CHADEMA badala ya kufanya uchunguzi wa weledi kupata majibu?, na je matukio haya yanafanana na ile Operation Tokomeza?! Je, Kovo alitumia nguvu hii hii anayoitumia kwa CHADEMA kuwakemea wale askari walio mlazimisha mwanaume mwenzetu kufanya mapenzi na mti na kwa kasi na nguvu hii ya kuihusha CHADEMA?
chanzo cha habari''CHADEMA DIASPORA''
SIJUI ILITEGEMEA NINI kama chanzo chenyewe ndio hicho.... ujinga uliopitiliza wa nyie chadema pro-chagaz ni kutunga uongo,kuusambaza, kuupamba,kuuvumisha na hatimaye ninyi wenyewe mlioutunga kuanza kuuamini.
at least somebody is injured(chairperson of your party who is opposing pro-chagaz block)
at least there is plenty of evidence on your violence acts in your part(mwigamba was beatten,sugu attacked police inside bunge area,video of RWAX planning some deadly attacks on some innocent citizens,confrontation with police in different places in this country..............etc.......etc.......etc.......etc)
hizi hekaya toka kwenu vifaranga hazitaweza kumponya mama yenu. you are swimming agaist the strongest political current in morden politics(ZZK).
MTAJUTA NAWAAMBIA
na nina hakika wenye akili miongoni mwenu (ingawa wako wachache sana) wameshaisoma na wameamua kukaa kimya.
wakati ZZK ana deal na mama zenu... we are here to deal with YOU(VIFARANGA). we wont stop till you get enough and perish
 
Hata chanzo kingekuwa wapi mkanda mzima wa utekajii ni washirika wa Zito polisi na Ccm.Chadema wako smart na hamna mwanachadema mwenye unyama huo zaidi ya mapandikizi ya kina Zito.

Mtoi, nina maangalizo kadhaa kutokana na maelezo yako yanayojikanganya,

1. Chanzo -CDM Diaspora unategemea nini kama sio habari za upande mmoja...kwa sasa ni vema kumsikiliza bwana Yona kwanndiye mtekwaji na pia kwani kila Mbowe na Slaa wanapowasiliana na viongozi lazima wakushirkishe? kuna ukweli alionywa na uongozi kwamba aache mahusiano naZitto kwani hata sasa uongozi wa CDM umeagiza viongozi na wanachama kutoshirikiana na Zitto , Hili lina ukweli

2. Zitto na wenzake wamefukuwa kutokana na waraka wa kutwaa madaraka kinnyume na Katiba......Wewe unatueleza kwamba Mwakembe katangaza kugombea uenyekiti Temeke, je sio uhaini? Kileo kajhalalisha kwamba yeye ndiye mgombea mteule wa Ubunge Mwanga bila kufuata katiba....je nikweli hamna wana CDM wengine wenye nia....kama ambavyo mnasisitiza siku zote kwamba wagombea wafuate utaratibu uliopo kwenye katiba, au kuna wanaoruhusiwa kwenda kinyume?

3. Ni ngumu kutenganisha utesaji wa Yona na CDM,kama ilivyo ngumu kutenganisha utesaji wa Ulimboka na Serikali!

3.
 

MMILIKI WA CHADEMA ALONGA INAONEKANA DHAHIRI HAPA CHAMA KINA WATU WA UKANDA WAKE WENYE MASLAHI YAO BINAFSI..!! KWELI WAMEDHAMIRIA KUMCHAFUA..!! UKWELI UTAJULIKANA TUU..!!
Mzee Edwin Mtei amtaka Zitto Kabwe ajiunge na CCM au CUF kwa kuwa ndani ya Chadema kwa sasa hahitajiki

Edwin Mtei amemtaka Zitto aunde chama chake au atafute kingine cha kujiunga nacho kwa kuwa kwa sasa hana nafasi.


Alimtuhumu kwa kuwagonganisha viongozi mbalimbali ndani ya Chadema na hata kuzua mitafaruku ya hapa na pale huku akisema kwamba uamuzi wa Kamati Kuu ndiyo wa mwisho.

Pia ameshauri kuwa kama ana ndoto za kuwania urais ni vizuri akatafute vyama vingine kama CCM au CUF kwa kuwa ndani ya Chadema kwa sasa hahitajiki.

Mtei alisema kuwa kama anataka kubakia na uanachama wa Mahakama wao hawana shida... "Lakini huwezi kuwapeleka viongozi wako kortini na bado ukaendelea kubaki kuwa mwanachama wetu."
SASA KAMA MTU ANAONA HAMUMTENDEI HAKI AENDE WAPI??? WEE MZEE HIVI HATA KWENYE FAMILIA KUGAWANA MALI IKISHINDIKANA LABDA DHULUMA IKAANZA JEE HAUTAKIMBILIA MAHAKAMANI??? HEBU ACHENI SIASA ZA KIAFIDHINA,KIZANDIKI NA KINAFIKI ZILIZOJAA UROHO WA MADARAKA NA UKANDA WAKE..!!
 
Hivi sasa kuna mgogoro unaoendelea katika chama kikuu cha upinzani (cdm) hapa Tz.
Mgogoro huu ccm inasemwa kuhusika zaidi kuhusika kwa asilimia kubwa.

Mgogoro uliopo cdm wamejitakia wenyewe, maana walimuona mtuhumiwa anakengeuka tangu mwaka 2008 na wakabaki wanamuangalia tu bila hata kumuonya?
Ndugu zangu hapa mlikosea, na mnatambua methali isemayo mchelea mwana.....mdharau mwiba.....au ile ya kawaida inayosema SAMAKI MKUNJE ANGALI MBICHI.

CDM imeruhusu ccm kuingilia mgogoro na kuukuza zaidi, cdm imeruhusu adui ccm kucheza mchezo unaochezwa hivi sasa, ccm wala isilaumiwe kwa makosa yaliyofanywa na cc ya cdm.
Msaliti angetoswa/angeonywa tangu alipogundulika anasaliti.

CDM malizeni mgogoro kwa busara.
 
Siasa za Tanzania zimejaa maji taka tu. Ndio maana umaskini unaongezeka maana tunatumia nguvu nyingi kwenye mambo yasoyo na tija tunasahau yenye tija kama hayapo vile
 
LOWASA Vs ZITTO KABWE NDANI YA VYAMA VYAO VYA SIASA
Watu Wanamfananisha Lowasa na Zitto, Wanasema Kama Lowasa Akihama CCM au Asipoteuliwa kuwa Mgombea Uraisi 2015 kwa Ticket ya CCM Basi CCM Itapasuka Vipandevipande na Wengine Kusema Itakufa Kabisa Kama Inavyopasuka Chadema na Kuelekea KIFO kwa sasa. Ifahamike ya Kwamba Vijana wa CCM na Wana CCM kwa Ujumla ni Tofauti Kabisa na Vijana wa Chadema na Wanachadema kwa Ujumla.Vijana wengi wa Chadema Walijiunga na Chadema Kwa Sababu ya Kuvutiwa na Zitto Kabwe, Uwezo na Umahiri Mkubwa Aliokuwa nao Katika Kujenga Hoja na Kuibua Kashfa,Siri Nyingi za Mafisadi.Hawakuwa na Malengo Binafsi ndani ya Chama na Siasa kwa Ujumla
Vijana wengi wa Chadema na Wanachadema kwa Ujumla Walijiunga na Chadema kwa sababu Kuu Zifuatazo
1. Walivutiwa na ZITTO KABWE, Dr Willbroad Slaa,Tundu Lissu au John Mnyika
2. Wanahasira na Serikali juu ya Kushindwa Kutatua Maslahi yao Binafsi
3. Walivutiwa na Chadema kwa Kuibua Kashifa za MAFISADI ie EPA, MELEMETA….
4. Waliongopewa ya Kwamba Chadema Inawapenda Sana Vijana na ni Mkombozi wa Taifa
5. Ndio Chama cha Upinzani Kilichokuwa na Nguvu Miaka ya 2009-2010…,Hivyo watu wanaopenda Upinzani Wakajikuta wamejiunga na Chadema
6. Wengine wamejiunga na Chadema kwa Sababu tu wao ni WACHAGA,Wanaamini Chadema ni Chama Chao
Vijana wengi wa CCM na WanaCCM kwa Ujumla Wamejiunga na CCM kwa Sababu Kuu Zifuatazo
1. Mapenzi yao ya Dhati na CCM,
2. Wana Malengo ya Kuwa Viongozi wa Kisiasa na Serikali wa Sasa na Badae
3. Nguvu ya Kisiasa na Kimtandao ya CCM ndani ya CCM na Serikali
4. Nafasi za Kiungozi ndani ya CCM ni Nyingi sana Ukilinganisha na Vyama Vingine vya Siasa
5. Nafasi ya CCM Kushinda Uchaguzi Mkuu na Kuunda Serikali ni Kubwa Kuliko Vyama vya Upinzani,Hivyo wana Matumaini ya Kuwa Sehemu ya Serikali
Ukitazama Sana Sababu Hizo Hapo Juu Utagundua ya kwamba Hata Lowasa Akihama CCM Basi Atahama yeye na Familia Yake na Hakuna MwanaCCM Atakaemfuata.Lowasa Atakuwa Raisi wa Tanzania Kama Kamati Kuu ya CCM na NEC Wakipendekeza Jina Lake na Kushinda Katika Kura za Maoni na Si Vinginevyo.Hata Kama Lowasa Hatashinda kwenye Kura za Maoni au Akakatwa Jina Lake Hata HAMA CCM, Atabaki CCM na Kuendelea Kuwa Mwanachama na Kiongozi wa CCM.
Vijana wa CCM na Wana CCM kwa Ujumla Wanakipenda Chama na Si Mtu Ndani ya Chama,Mimi Nawapenda Sana Viongozi wa CCM Wazalendo,Wanaowajali na Kupigania Maslahi ya Watanzania Lakini Wakihama CCM SINTOWAFUATA WAENDAKO,Nitabaki kuwa LOYAL na CCM Maana Kila Mtu Anamalengo yake ndani ya Chama cha Siasa,Kama Unamfuata Mtu Huwezi kuwa Stable Maana Umejenga Imani yako kwa Mtu na Si Chama.
FAHAMU
CCM Imejengwa Juu ya Mwamba,Ni Imara sana,Mizizi yake ni Mirefu na Imara Mno
CCM Inatawala Leo, Itatawala Kesho na Kuendelea Kutawala Mpaka Kitakapopatikana Chama sahihi Ambacho ni Mbadala wa CCM Lakini Sio Hivi Vyama vya KIKABILA…
CCM Inawajali Wazee na Vijana Hivyo Inapata Baraka za Pande Zote Tofauti na Vyama Vingine vilivyo Watenga Wazee na Kuona ni Watu waliopitwa na Wakati.

KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI…
pamoja na kwamba mimi sio mpenzi,mfuasi wala mwanachama wa ccm, lakini kamwe siwezi kubishana na ukweli.
sio lowasa tu!! viongozi wote wa ccm hawawezi kuhama ccm kwa sababu huko ndiko iliko salama yao. na kuhusu uwezekano wa ''ETI CHADEMA KUCHUKUA DOLA" hilo kila mwenye akili anajua ni ndoto za mtembea juani.
THIS COUNTRY WILL NEVER BE GIVEN TO DOGS...
Haswa katika kipindi hichi ambacho'' DOGS ARE CHASSING PATRIOTIC MEN/WOMAN TO POSSES THE PART''
 
Huu ni Upuuzi,Jitu zima lina heshima zake linakuja na hadithi Kama za kina Yerico.Huu ni ujinga tatizo mmezoea misukule hua haishtuki lakini hebu kua hata na chembe ya aibu. Haki Huliinua Taifa Ila Dhambi .....?
Mtashindana Lakini Hamtashinda.Mtoi Huu uongo unaotunga kwaajili ya kuwatendea wakandamizaji wa haki utakuback fire very soon.utatumika sana kusafisha watu, poor u.
 
Hawa CDM hawa, wanafanya watu waache kujadili mambo muhimu ya kitaifa, wanataka wajadiliwe wao muda wote tu!!. Spinning nyiiingi mpaka mnaboa!.
 
Kuna umuhimu wa sisi watanzania kuanza kampeni ya kuhakikisha KOva anaondoka kwani kapachikwa pale kwa ajili ya propaganda Alisha retire badala ya kufanya kazi ya wananchi yeye anafanya siasa
Mtanzania sio gazeti la maana kwa sasa wanatumika na MACCM na si ajabu mmliki Rostam na LOwassa ungetegemea nini hao ni KIng makers threat wa hao ni chadema na wala sio CCM watashindwa kama walivyo shindwa message hizi wanatakiwa wananchi wazifahamu tu kwamba tuko kwenye vita na dola,CCM na vyama mamuluki wao, Usalama wa taifa na media power house

kaka hao uliowataja ROSTAM,, inasemekana lakini alishawahi kumpa hela mwenyekiti MBOWE...
 
Mohamed Mtoi,labda utuambie kama kuna kiongozi yeyote wa Chadema makao makuu alieenda kumjulia hali Yona.
 
Back
Top Bottom