If y'all know why they call me TECH WIZ well today i'mma give y'all a piece of HINT.You know what!!??Nimeielewa hii story ya Mtoi kinyume chake.Mbowe ana kashfa ya kupokea fedha kutoka kwa wanaotuhumiwa na makosa ya UFISADI so hii inamaanisha kwamba Mbowe ana mahusiano ya karibu na Mafisadi wa CCM kinyume na anavyojaribu kutuaminisha kwenye majukwaa ya kisiasa.Mafisadi wanatamani kuiona CCM ikirudi madarakani 2015 lakini Dr Slaa anaonekana kuwa kikwazo kwao,Wafanyaje?So suluhu ni kumtumia Mwenyekiti na ndio hayo mambo tunayoyasikia leo mara kapewa na Mkono shilingi milioni 20 (2008) na baadaye shilingi milioni 200 (2010) hapa tusifanye makosa kuna malipo yatakuja huko mbele kwa gharama za Chama.Sasa haya mambo ya kutekwa na kuumizwa kwa Bw Yona mimi ninahisi ni mpango wa akina Mbowe wakishirikiana na Mafisadi wa CCM wameandaa hii filamu mpya ili kutusahaulisha juu ya SIRI iliyofichuka ya USHIRIKA wa Mbowe na Mafisadi katika kuhujumu harakati za Chadema.Pia wanataka tuendelee kuwaamini akina Mbowe.