Inasikitisha jinsi gali ulivyo haujui sheria na kanuni za kumfanya mtu awe diwani au kiongozi wa nchi.
-kwanza kabisa nchi yetu haitambui mgombea binafsi, ingawa mtikila alijitahidi kulipigania hilo,
kwa maana hiyo hakuna kiongozi yoyote (Diwani, Mbunge na Rais) atakayeendelea kuwa na cheo hicho kama
si mwanachama wa chama chochote cha siasa kinachotambulika kisheria.
-Chadema hawakuwafukuza udiwani (rejea tamko la Mhe: Mbowe), walichofanya ni kuwavua uwanachama wa chama cha Chadema.
kwakuwa sheria za nchi hazitambui mgombea binafsi, basi madiwa wanakuwa wamevuliwa udiwani wao.
-Chadema ilichokifanya kwa mujibu wa kanuni na sheria ni kuandikia mamlaka husika na kuwataarifu kuwa diwani Mallah, Bayo, Ngowi,
Mpanda na Rehema si wanachama wa Chadema.
-Kamati kuu ya Chadema inayo mamlaka yakumvua mwanachama yoyote atakayeenda kinyume na sera za chama.
-Madiwani wote kwa wingi wao wamevuliwa uwanachama na hawawezi kuingia kwenye kikao chochote cha madiwani kwakuwa si wanachama
wa chadema chama ambacho kiliwapa ridhaa ya uongozi.
-Mwisho, Meya hawezi kuchaguliwa kwani sheria zinasema anatakiwa achaguliwe na 2/3 ya madiwani wote, ukitoa madiwani waliofukuzwa
na madiwani waliobaki wa chadema ambao wameazimia kugomea vikao hadi muafaka ufikiwe, madiwani waliobaki hawafikishi idadi inayotakiwa.
Naomba kuwakilisha.