<br /><br />
<br /><br />
Mkuu nilikuwa naheshimu sana comments zako, kumbe sikujua kama kulikuwa na kaupumbavu kanakusumbua. CHADEMA hawakuwafukuza madiwani ili washinde umeya, wala kushinda viti vya udiwani tena. CHADEMA wamewafukuza madiwani kwakukiuka maamuzi halali ya kamati kuu kwa makusudi. Kwa sababu hiyo, ni heri wamewafukuza ili nidhamu ikabaki kwenye chama. Suala kushinda lipo kwa wapiga kura. Kufungua kesi mahakamani ni haki yao kama wanaona wameonewa, la msingi ni kwamba tumewafukuza kwenye chama makini. Hata hivyo itakuwa ngumu kushinda kesi, kwani hawakufukuzwa kwa kuingia muafaka, bali kukiuka kanuni. Hatuna haja ya umeya, tuna haja ya haki na usawa.