Mpambano: Bulembo vs Fatma Karume Kuhusu Uchaguzi Zanzibar

Mpambano: Bulembo vs Fatma Karume Kuhusu Uchaguzi Zanzibar

Ndo maana mtoto wake BULEMBO amepewa ubunge akisoma kidato bha tatu,ukisitaajabu ya musa utayaona ya BULEMBO.

Graduation za form three siku hizi zinapendeza
 

Attachments

  • 1452413778594.jpg
    1452413778594.jpg
    106.2 KB · Views: 50
Kwani Karume ni mpemba? Mbona historia inaonyesha alikuwa na asili ya Nyasa? Halafu ukisema mchanganyiko wa kiarabu mbona mke wa Karume Sr (mama Karume) ambaye ndiye anaonyesha kuwa na asili ya kiarabu ni CCM kindakindaki? Tuijadili hoja tuache ubaguzi kama chaka la kuficha udhaifu.

Unapoteza muda wako,hao CCM ndiyo wa kwanza kuendeleza ubaguzi wajinga kweli hawa.Hawajui issue ya Z'bar iko sensitive mno
 
Matatizo ya Zanzibar yana rangi za uweupe na uweusi. Uchaguzi mkuu wa mwaka 1995, mgombea fulani alijiona ana nafasi ya kushinda hiyo akapagawa na kusema 'bado siku nne tukomeshe utawala wa mtu mweusi Zanzibar'. Ndipo watu wakashtuka..! Kumbe kuna uzanzibari na uzanzibara! Bahati nzuri hakushinda, hiyo utawala wa mtu mweusi ukaendelea!
Thibitisha kwa vielelezo please
 
Sasa huku bara huwa mnafata nini mkishagombana?2001 mmeuana na wengine wakawa wakimbizi,si mliyamaliza sasa imekuaje?tangu siasa za vyama vingi zianze Zenj haijawah kutulia,kuanzia kwa Salmin Amour mpaka kwa Shein,kuna shida huko visiwani
Tena shida kubwa sana ila naona safari hii ngoma imewakalia kooni
 
Last edited:
Ha ha ha! Ndio hapo unaponikumbusha kile kisa cha ndugu zangu WAHA, eti Muha mmoja anaweza kubishana na behewa zima la 3rd class toka Tabora mpaka Kigoma bila kuchoka. Kumbuka hapo ubishi wake hauna point mradi anabisha tuu.
Duuuu umenikumbusha ubishi wa ndugu yetu humu jf anaitwa MOTOCHINI na mcubic
 
Hili suala la Zanzibar ni dogo sana kama akili kubwa zitapewa nafasi zilishughulikie lakini tukiliachia watoto kina bulembo we are in trouble
 
Bulembo is a jack of all trades; kajaribu mpira; kapa! Kajaribu biashara; hoi! Sasa anadhani kwenye siasa kafika; mpaka amekuwa kampeni meneja wa mgombea Urais! Kwa hiyo maoni yake ni ya kisiasa zaidi ili kutetea ugali, mueleweni!
Tatizo la Bulembo ni elimu hana kabisa hata ya vipande
 
wewe bulembo usimlinganishe na mwana sheria kama fatuma karume huyo elimu yake ni darasa la saba
Bulembo ni shida sana na popote pale ukisha muona mtu anayependa kujipendekeza kwa watawala basi ujue huyo ni sheeda kama yule mwenye ulimi mrefu kama nyoka
 
Duuuu umenikumbusha ubishi wa ndugu yetu humu jf anaitwa MOTOCHINI na mcubic
Acha kuwachokoza nyuki waliolala mkuu. Hapo ni sawa na kuukojolea mzinga wa nyuki wakichomoka hapo wanauma sio wewe tuu uliyewakojolea bali hata wapita njia wengine.
 
Aliwahi kuwa kiongozi Wa FAT Mara enzi ya kina Rage hakuna la maana alilofanya zaidi ya migogoro
hawa ndio wale wazee WA fitina,majungu na uchawi Enzi hizo. Walikuwa miungu watu ndani ya FAT, eti ndio hazina ya ccm kwenye uongozi na ndio maana ccm imekosa weledi na majungu, mipasho na ubabe.
 
Mtu akunyime chakula sio shule fatma yy anaongelea maamuzi ambayo hayakufata utaratibu ya jecha kufuta Matokeo na wala sio mambo ya ccm yy bulembo amekuw lini msemaji wa jecha au zec hapo anafanya watu wazidi kuamini ilikuwa shinikizo kwa jecha kufuta Matokeo baada ya kuona shein kapigwa chini.halafu Mzee shein swala tano hâta nafsi haikusuti ndo maana nasemaga huyo mungu wa waislamu sijui ni mungu gani
 
Acha kuwachokoza nyuki waliolala mkuu. Hapo ni sawa na kuukojolea mzinga wa nyuki wakichomoka hapo wanauma sio wewe tuu uliyewakojolea bali hata wapita njia wengine.
Mkuu wacha waje dawa yao ni mafuta ya taa tu toka kwa Mmawia
 
Back
Top Bottom