Mpambano: Bulembo vs Fatma Karume Kuhusu Uchaguzi Zanzibar

Mpambano: Bulembo vs Fatma Karume Kuhusu Uchaguzi Zanzibar

Labda Jecha alitangaza kufuta matokeo baada ya mzee Seif kujitangazia matokeo ya awali wakati tume ndiyo yenye wajibu ya kutangaza matokeo kadri yanavyopatikana. Labda kuna rafu ambayo CUF walitaka kuicheza ambayo inafanana na ile ambayo UKAWA walitaka kuicheza huku bara halafu usalama wa nchi ukawashtukia na kuharibu kila lililokuwa limepangwa, natumia neno labda kwa sababu ni maoni yangu tu.

Sasa CUF itachezaje rafu wakati hakina madaraka?Chama kilichopo madarakani ni CCM.Jaribu kushirikisha ubongo wako kabla ya kujibu hoja.
 
Mkuu Fatma hakinzani na baba yake Rais Mstaafu na ndiye mshauri wake mkuu tokea urais. Ukisikia Fatma anasema moja ujue wameshajadiliana na baba yake. Wote wako pamoja na Mansoor Himid - shemeji yake Karume.
Kama hukujua basi bora uelewe hilo. Fatma siyo independent au objective bali ana maslahi yake. Hili si tatizo ila ni vyema ikijulikana.

Asante kwa ufafanuzi.Nimefurahi Kusikia Rais Karume nae amesimamia haki.
 
Sasa CUF itachezaje rafu wakati hakina madaraka?Chama kilichopo madarakani ni CCM.Jaribu kushirikisha ubongo wako kabla ya kujibu hoja.
Ubongo wangu siku zote naushirikisha kaka, na sio lazima utumie matusi ili hoja yako ifike. CDM waliajiri mpaka wakorea kwa ajili ya kufanya hujuma ingawa hawakuwa na dola, CUF kutokuwa na madaraka haimaanishi kuwa hawawezi kufanya mambo ya rafu kwenye siasa, kwanini seif akimbilie kutangaza matokeo ya uchaguzi wakati yeye sio muajiriwa wa tume, ni mgombea urais kama alivyokuwa Dr. Shein na wengine?.
 
Hivi sababu ya kuwapa wagombea matokeo ya kila kituo kila mgombea ni nini? Kuna kosa gani mgombea akisema matokeo yangu ya vituo A,B,C ni 2+3+4 =9 ???
Au calculator ya kujumlisha matokeo iko tume tuu? Mie nadhani angehojiwa au kulaumiwa kama kwa hesabu niliyotaja hapo juu akasema jumla ni 13
 
Back
Top Bottom