Mpaka wa Tanganyika na Zanzibar Upo Wapi?

Head teacher

JF-Expert Member
Mar 10, 2012
1,796
411
Ni vyema kabla ya muungano kuvunjika tufahamishane mipaka ya baharini kati ya Tanganyika na Zanzibar mapema wakati huu bado tunaelewana. Maana hawa wazenji wasije wakaleta kama za Malawi tukawachapa.

Kuna muda furahi UAMSHO walidai kuwa eneo la Dar es Salaam, kilometa 10 kutoka ufukwe wa bahari lipo Zanzibar.

Je kuna yeyote anayefahamu mipaka sahihi ya Jamhuri ya Tanganyika na Jamhuri ya Watu wa Zanzibar atujuze mapema. Maana kama kujiandaa kwa LIWALO NA LIWE basi iwe mapema
 
Ninaamini Muungano ukivunjika Wazenj watataka ku-nullify Heligoland Treaty ya 1890 ili ukanda wa Pwani uwe wao. Hoja yao kubwa ni kwamba Mwingereza hakuwa na legal capacity ya kuingia mkataba unaohusu ardhi ya Zanzibar bali Sultan (Zanzibar ilikuwa protectorate chini ya Uingereza).
Mipaka ina utata!!!!
 
Mkuu hizo km 10 ndani ya Tanganyika ni kweli kwa mujibu wa mkataba wa sultani na mjerumani. Sultan alikuwa akitawala uarabuni, visiwa vya unguja na pemba pamoja na km 10 pwani ya afrika mashariki yaani dar hadi huko mombasa.

UAMSHO ni kama MRC ya Kenya ambayo inasema pwani si Kenya. Hapo kuna shida heri kweli tuelewane mapema kabisa. Lakini ikumbukwe pia kwamba baad ya waingereza kupewa Tanganyika waliondoa huo mkataba na kuitawala Tanganyika yote na zile km 10
 
nadhani Buguruni itakuwa sehemu ya jamhuri ya watu wa zanzibar!maana wale wapemba pale buguruni ukiwambia eti hiyo siyo zanzibar patakuwa hapatoshi!
 
Kusema kweli it may sound odd lkn kama mikoa inapimwa ni bora kigezo hichohicho kikatumika znz. Inawezekana kabisa muungano hautenganishiki hasa kutokana na swali hili. If that is the case basi tujipange Znz iwe mikoa ya nchi moja else huu muungano lzm ubaki kama ulivyo ila tujitahidi kumaliza kero za muungano.
 
Kwa mujibu wa mkataba kati ya Germany East Africa (Tanganyika enzi hizo) na Sultan wa Zanzibar, Sultan alipewa kutawala hadi maili 10 ya pwani ya Tanganyika.

Pia Sultani alipewa kutawala hadi Mombasa na Waingereza.

Kwa kuwa Sultani anarudi kutawala, maili 10 ndani ya Dar, Tanga, na Bagamoyo itakuwa sehemu ya Zanzibar, pia Mombasa nayo.
 
Wimana

Kwani wakati wa uhuru wa Tanganyika mwaka 1961, Pwani ilikuwa Zanzibar
 
Last edited by a moderator:
Rahisi sana;
Zanzibar kufanywa rasmi kuwa sehemu ya mkoa wa Dar: yaani visiwa kuitwa rasmi wilaya za Uguja na Pemba. Hapo mipaka ya wilaya hizo nadhani haitakuwa na tatizo. Hii itamaliza kelele zote.
 
Hili ni swali la muhimu sana,mpaka utakuwa wapi muungano ukivunjika?Maana kweli haya ya Malawi yamezua mambo.
 
Back
Top Bottom