Mpaka wa Namanga wafungwa kwa muda na raia wa Kenya

sumu-ya-panya

JF-Expert Member
Aug 6, 2016
628
570
Wananchi wa Kenya wenye asili ya Somalia leo asubuhi wamefunga mpaka kwa kuchoma Matairi na kuweka vizuizi katika barabara inayoingia Tanzania na Iinayoingia Kenya Baada ya Watu wasiojulikana kumteka mtoto wa mfanyabiashara mkubwa NAMANGA na kutokomea nae kusikojulikana usiku wa kuamkia Leo, Raia Hao wenye asili ya somalia na wengine wanaishinikiza Serikali zote mbili kupatikanakwa mtoto huyo haraka.

Inadhaniwa baada ya tukio hilo watu wasiojulikana walielekea Tanzania.

Taarifa zaidi zitawajia hivi punde

Update

Moto umeongezwa zaidi moshi mweusi
Sauti ya makopo ya gas kulipuka katika moto inasikika

Mtoto anaedhaniwa kutekwa ni mrithi wa mali za familia kwa maana ye ndie tajiri.

Anamiliki magari ya Gas nchini Kenya.

index1.jpg
index2.jpg
index3.jpg
 
Sasa mtoto katekwa kenya, wao wanafunga mpaka unaoihusu Tanzania pia.! Vyombo vya ulinzi vya Tz vinahusika vipi.?????

Na pia wakiendelea kufunga huo mpaka huyo mtoto atarudi kupitia anga au.?

Moja kati ya laana ambayo kenya wamepewa ni kuingiliana na jamii ya kisomali..

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Msafwa pekee aliyesoma, hata hivyo uelewa wako hafifu. Hawa hawajaingia Tanzania ila wamefunga barabara baada ya mpaka yaani ofisi za uhamiaji ukitokea Tanzania.
 
Mtoto wa Tajiri kutekwa na maharamia inahusiana vipi na mpaka, hao matajiri wanamambo mengi usikute hata waliomteka mwanae anawajua

Huyo Tajiri alikuwa anaishi upande upi na raia wa wapi, au Namanga ipo pande zote mbili.
Hili Suala nila serikali mbili mjadala wa wasiojulikana
 
Baada ya watu wasiojulikana kwenda upande wa kenya mpakani Namanga na kumteka kijana raia wa kenya,wananchi wa kenya wamefunga mpaka wa kenya hadi Tanzania itakapo mrudisha kijana wao,vijana hao wanadai gari aina ya landcruser ilifika dukani kwa huyo mwenye duka na kumtishia kwa bastola na wananchi walivyo jaribu kuzuia walipiga risasi juu na kuelekea nae upande wa Tanzania.

IMG-20190327-WA0001.jpg
 
Duh, diplomasia ichukue nafasi yake. East Africa inakwenda wapi sasa? Kwa maana unaona huku Rwanda na Uganda kuna chemka, Burundi nako na jirani yake ndo hivyo. Sasa Tanzania na Kenya? Tunaenda wapi? Hope litashughulikiwa na litakwisha ili maisha yaendelee kama kawaida.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
watu wasiojulikana wanavuka mpaka border hii ni noma...hii nchi sasa ni too much...jamaa ni peace sana ule inauma sana
#BringBackMohaWetu
 
Back
Top Bottom