Mpaka kufikia Umri huu nimeishi kwa shida sana ndugu zangu, moyo wa mtu umebeba mengi sana

Bill Lugano

JF-Expert Member
Aug 20, 2018
1,186
6,402
Nakumbuka jinsi ambavyo mama alikuwa anatulazimisha kula vyakula mbalimbali na matunda kila wakati. Nilikuwa naona kero sana. asubuhi tu unaangalia menu ya breakfast imejaa hujui ule nini uache nini, ni buffet. Mimi kwa kweli nilikuwa naona kero. natamani kuishi maisha ya watu wengine unakuta labda bfast anakunywa maziwa, cake/mkate,mayai na matunda. Sisi ilikuwa issue home.

tunakereka meza imejaa ma vyakula mengi hatujui tuache nini tule nini. Basi kwa kulazimishwa sana tunasogea mezani na wadogo zangu. Sasa tunamwambia mama tule nini maana kuna kipindi kuna vyakula hata majina tumevisahau. wale watoto wa kizungu wa kitajiri walikuwa wakija home wanauliza "dya have a party today? "nawaambia hapana ndo maisha ya kila siku wanashangaa sometimes mpaka unawashtua akili yao irudi sawa maana ni kama wanapigwa ganzi hivi.

Hapo mama anamwita mpishi na daktari waje watuelezee. mpishi anaelezea jina la chakula na jinsi alivyo pika na daktari anatuelezea faida ya kula hivyo vyakula mwilini na kwenye akili, basi hapo ndo kwa shingo upande tunaenda kula, yaani tumeishi katika mazingira magumu sana.

Shuleni unatamani uende upande school bus kama wenzio yeye mzee anawatuma madereva watupeleke na kutusubiria, kila mtu na dereva wake, mimi nilikuwa naona kero kusubiriwa na dereva so nampa usd 500 akatembee tembee huko then arudi muda wa kutoka. maana mtu unasoma kwa wasiwasi ukijua kuna dereva anakusubiri. sikuwa napenda maisha hayo.

Mzee alikuwa na tabia kila mwezi anamwambia daktari atupime magonjwa yote mwilini. na daktari wa familia alikuwa anakaa hapo hapo kwenye compound ya home maana mzee alifanikiwa kupata kakiwanjaka hekari 200 akajenga humo na nyumba za wafanyakazi wake. nlishawahi waambia hili huko nyuma kipindi kile mnasema eti nyumba aliyojenga Mengi ilikuwa nzuri.nliwashangaa sana.

Ile nyumba ilikuwa ya kawaida kabisa haikuwa na jambo lolote la ajabu ni kama nyumba aliyokuwa anaishi msimamizi wetu wa mifugo dr. lobstain. huyu ni mtalaamu wa mifugo anayeheshimika sana netherlands na nchi nyingi za scandanavia.

Basi maisha yetu yalikuwa magumu sana. mtu unaambiwa kwa siku angalau ule si chini ya mara 6 vyakula na matunda mbalimbali upendayo. Halafu jioni unaambiwa ukakae bustanini uvute harufu ya maua na kusikiliza sauti za ndege. tena hivyo vyakula kwanza mpaka viangaliwe faida zake mwilini ni nini, nikawa natamani watoto wengine wanakula chochote tu watakacho tena wala hawajali wamekula mara 4 au ngapi.

Sisi tumelelewa katika mazingira ambayo ilikuwa inakwaza sana. yaani ukitaka chochote kile unapewa, nikawa nawaza lini nami ntaomba kitu kwa mzee kama wengine kwa wazazi wao akanambia sina. Inaumiza sana unatamani uishi maisha ya wengi lakini maisha yenyewe yanakukatalia. yanataka uishi kama mtu special. mimi nimehangaika sana katika hii dunia kutafuta shida/taabu. Nimeshindwa. kila mara nikawa nawauliza wenzangu au haya maisha ninayoishi ndo shida zenyewe. wakawa wananikatalia kwa kunitia moyo kuwa siyo.

Mimi niliona shida sana. Pale home kila gari la thamani lipo, najiuliza haya maisha mpaka lini? mzee anatumia gari miaka 3 anarudisha kiwandani anasema lime expire. hapo unakuta limetembea kms 2000-5000 tu. anasema basi lirudishwe huko aongezee pesa anunue model mpya. mpaka wakawa wanamfahamu mzee wakitoa model mpya ya gari wanampigia na sometime wakati wanawaza model mpya wanampigia awaelezee angependa hiyo gari iwe na vitu gani. Mzee alikuwa naona usumbufu sana. ndo akawa anawaza kuwa angependa kwenda kuishi mwezini hata miezi miwili tu apumzike na usumbufu wa duniani hapa.

Then arudi kuendelea na maisha mengine. Hapo tukawa tunaona mzee asije akataka familia yake nzima iende huko maana kipindi hicho ndo kuna binti mmoja mzuri sana alikuwa nafanya juhudi ya kuwa na mimi. Baba yake alikuwa Rais wa marekani alinipenda sana yule binti. Nikaona kwanza kabla sijamkubalia nimweleze mzee ili wamchunguze vizuri yule binti akili zake, uelewa wa mambo,afya na sehemu zake nyeti kama zipo salama, zinaendana na mimi kwa size au vipi.

Maana daktari alinambia nisije chukua msichana ambaye ana sehemu kubwa sana nitakosa ku enjoy tendo lenyewe. so mzee alipoanza hizo stories za kuwa amechoka kuishi duniani nikaona asije akasema nimsindikize huko mwezini.na wakati huo nami ni teenager damu inachemka mabinti wananigombania ile mbaya.

Kila napokumbuka maisha haya ya mateso nawaza nasema daaah.. afadhali sasa naishi peke yangu na magari yangu mimi angalau sitaki yafike idadi kama ya mzee mimi napenda kuwa na magari yasiyopungua 5 makali sana na yasiyozidi 10. Ila mzee nachomlaumu kingine alinijengea mentality mbaya sana. kutoyaamini magari na usafiri wa mjapani.

Hivi nawaza nije ninunue angalau V8 moja nione ikoje? Maana naona hata Rais anatumia hayo magari but mzee huwa anasema magari mengi ya mjapan siyo safe sana. Anyway, sijui maybe mwaka huu nami nichunguze hilo maana naona kama bado naishi chini ya mzee ingawa nipo kwangu. sababu ya mawazo yake kwetu, leo hii nipo huru naenda nchi yoyote ninayotaka duniani. nimeshazunguka nchi nyingi sana bad kufika mbinguni tu.natamani nako siku za uzeeni nikatembelee huko.
 
Duuuuh shida ulizopitia zimenifanya nishindwe kujua nikuonee huruma au, nimejikuta nacheka kwa sauti kubwa ofisini mpaka wenzangu wamekuja kuniangalia kuna nini maana si kawaida.

leo siku yangu imeanza kwa kicheko kikubwa sijawahi kuwa nacho. jamaaaa umewaza nini? maana najaribu kujenga picha unavyosimulia kwa huzuni sana ila unayoyasimulia, nyie watu wengine ni genius basi tu 🤣🤣

🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣
 
Nimemkumbuka GuDume sijui yuko wapi siku hizi.

Huyo bint w Rais wa Marekani siyo Malia kweli mnamgombania na Mtemi Don Namilson?
 
Back
Top Bottom