Mozambique = Msumbiji?

MaxShimba

JF-Expert Member
Apr 11, 2008
35,772
4,054
Hivi hii tafsir ya Mozambique ilitoka wapi na kuwa Msumbiji?

Sasa Kenya itakuwa nini kwa kidhungu?

Au neno Zanzibar ni kiswahili kweli?

Walau Mozambique inafanana fanana kidogo na Msumbiji,

Na hii je?!....

Portugal = Ureno!!

Nadhani magwiji na waasisi wetu wa lugha hawakuipenda nchi hii na wakoloni wake!! lol

Ila kiswahili kiko perfect na italia.....

Ndivyo wenyewe wanavyojiita...na sio italy...

Mnanikumbusha darasa la nne, naangalia ramani halafu Mozambique inanizingua kichizi. Hivi hii nchi ya Afrika au vipi?

Ila kiswahili kiko perfect na italia.....

Ndivyo wenyewe wanavyojiita...na sio italy...

-ia ni perfect ending ya majina ya nchi nyingi, na ina latin roots - not surprisingly, latin having origins in the modern day Italy, or the other way around- kwa maana ya "sehemu ya" which is natural kwa jina la nchi under that rule.Jina la kweli katika Kiswahili linaanza na U-, as in Ureno kama ilivyosemwa hapo juu, Uingereza, Ujerumani, Uchina, Unyamwezi, Ukaguru, Usukuma, Uzaramo, Usukuma etc. -ia ni kutohoa kutoka kilatini zaidi ya kiswahili cha kweli.

Kuanzia non state place names kama Patagonia, Manchuria, Transylvania, Pennsilvania, Bavaria, Bohemia, Azania, Brittannia etc mpaka states kama Mauritania, Somalia, Nigeria, Liberia, Yugoslavia, Bolivia etc.

Kuanzia "Australia" (latin "australis", southern, hence australia, land of the south) mpaka countless of other ia ending place names, including "Tanzania" which would mean land of Tan and Zan, as in Tanganyika and Zanzibar, by the same token ( although some tie Azania, the ancient name for Sub Saharan Africa with that name, no reason why it shouldn't be both IMHO ).

Hapo Kiswahili kimetohoa kutoka kilatini tu.

Kuna kipande cha audio niliki-record miaka kama mitatu iliyopita kutoka Radio Mlimani (fm), kiliongelea swala hili. Mtaalam mmoja wa lugha ya Kiswahili toka UDSM alikuwa anaelezea vina na mizizi ya maneno katika Kiswahili. Na moja ya jambo alilogusia ni majina ya nchi. With time nitajitahidi kuchimbua kwenye archive yangu na ku-upload hapa kwa manufaa ya wengi.

walau mozambique inafanana fanana kidogo na msumbiji,

na hii je?!....

Portugal = ureno!!

Nadhani magwiji na waasisi wetu wa lugha hawakuipenda nchi hii na wakoloni wake!! Lol

na ulaya je?????walitoa wapi hii ulaya??????

Walau Mozambique inafanana fanana kidogo na Msumbiji,

Na hii je?!....

Portugal = Ureno!!

Nadhani magwiji na waasisi wetu wa lugha hawakuipenda nchi hii na wakoloni wake!! lol
Moreno=dark skinned,dark haired.
Wareno=wazungu dark.
Au wao walivyotuita watu wa pwani ya mashariki na sisi tukawageuzia kibao.
Egypt=misri(the right way)

Ulaya kama sikosei inatokana na Milima ya Urals inayotenganisha Bara la Uropa na la Asia

sisi wataalamu wa vishazi tunafahamu sana kuwa language ( lugha) is arbitrary. ie. hakuna uhusiano wa neno na tafsiri yake haka kama kimatamshi linafanana fanafa. hapo hatukutafsiri majina hayo ya nchi bali tumetunga yetu ya kisw. na hakuna kuhoji. ni sawa na mchanga ( sand) kuitwa mchanga hakuna uhusiano wowote!!

Hivi hii tafsir ya Mozambique ilitoka wapi na kuwa Msumbiji?

Sasa Kenya itakuwa nini kwa kidhungu?

Au neno Zanzibar ni kiswahili kweli?

Na neno "kidhungu" maana yake nini? Ni kiswahili kweli au uhuni tu? Mimi nimekutana nalo hapa JF, sijawahi kulisikia au kulisoma mahali pengine. Mwanzoni nilifikiri ni typing error lakini naona linajirudia.

Wamakonde asilia wanatamka "msambiki" labda ndiyo huko jina la msumbiji lilikotokea!

sisi wataalamu wa vishazi tunafahamu sana kuwa language ( lugha) is arbitrary. ie. hakuna uhusiano wa neno na tafsiri yake haka kama kimatamshi linafanana fanafa. hapo hatukutafsiri majina hayo ya nchi bali tumetunga yetu ya kisw. na hakuna kuhoji. ni sawa na mchanga ( sand) kuitwa mchanga hakuna uhusiano wowote!!

Granted kuna majina kama Ureno na Portugal ambayo hayana uhusiano (ningependa kujua historia yake, najua ipo).

Lakini utakataa kwamba Marenani na America hamna uhusiano? Ufaransa na France hamna uhusiano? Ujerumani na Germany hamna uhusiano?

1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom