Dr leader
JF-Expert Member
- Jun 28, 2016
- 1,080
- 1,448
MOYO UNA MENGI.
Kiukweli ni mapito haya napitia
Moyo umeshindwa hauwezi kutulia
Mbona kutamka nafusi yanizuia
Nimeyabeba mengi ya huzuni moyoni.
Natamani kusema na kuyasimulia
Lakini sijui nani nitamuambia
Ayaweke moyoni nayo akatulia
Nimeyabeba mengi ya huzuni moyoni
Kitu nilichojifunza kwenye kwa dunia
Upige mkelele nani atasikia
Hakuna mtu atakaye kuhurumia
Nimeyabeba mengi ya huzuni moyoni.
Watasema tulisema na kumuambia
Na tulimkanya kisha tukamuusia
Mwacheni aumie kesho hatorudia
Nimeyabeba mengi ya huzuni moyoni.
Acha nijikaze na pia kuvumilia
Na niwaeleze muende kuhadithia
igeuke fimbo kwangu ya kunichapia
Nimeyabeba mengi ya huzuni moyoni.
Mtanicheka na sio kunisaidia
Na msonipenda mzidi kufurahia
Kisha ninao wapenda watanikimbia
Nimeyabeba mengi ya huzuni moyoni.
[emoji2398]ibn kimweri.
0746624003
Kiukweli ni mapito haya napitia
Moyo umeshindwa hauwezi kutulia
Mbona kutamka nafusi yanizuia
Nimeyabeba mengi ya huzuni moyoni.
Natamani kusema na kuyasimulia
Lakini sijui nani nitamuambia
Ayaweke moyoni nayo akatulia
Nimeyabeba mengi ya huzuni moyoni
Kitu nilichojifunza kwenye kwa dunia
Upige mkelele nani atasikia
Hakuna mtu atakaye kuhurumia
Nimeyabeba mengi ya huzuni moyoni.
Watasema tulisema na kumuambia
Na tulimkanya kisha tukamuusia
Mwacheni aumie kesho hatorudia
Nimeyabeba mengi ya huzuni moyoni.
Acha nijikaze na pia kuvumilia
Na niwaeleze muende kuhadithia
igeuke fimbo kwangu ya kunichapia
Nimeyabeba mengi ya huzuni moyoni.
Mtanicheka na sio kunisaidia
Na msonipenda mzidi kufurahia
Kisha ninao wapenda watanikimbia
Nimeyabeba mengi ya huzuni moyoni.
[emoji2398]ibn kimweri.
0746624003