Nipa Neema Wadudi
1 Umenishika utungu, Matozi ndani ya maji
Menichoma nungunungu, ninakosa mfariji
Sijui ni lepi fungu, wala sinalo taraji
2 Yanisakama mawazo, usiku kesha silali
Kila yaumi vikwazo, mwisho ungali umbali
Lini nipate tulizo, hakunapo afadhali
3 Ati kukua ni huku, dunia mejaa tabu
Nakula kwa chukuchuku, ambwa natiwa adabu
Napeza kula makuku, ninenepe kama dubu
4 Naenda huku na kule, ila bado yale yale
Amara hii na ile, halitoshi lake bale
Sipati japo uwele, nifurahi nami nile
5 Madeni tele yan'zidi, ulimwengu masumbuko
Nipa neema Wadudi, fuadini machubuko
Mola sijamkaidi, ingali ni sokomoko
[emoji2399]Abuuabdillah[emoji3578]
0744883353