Moyo mpweke

habari ya hapa

JF-Expert Member
Dec 20, 2012
12,791
8,743
Nina tamani walau siku moja moyo wangu upate kutulia, nimpate wa kunienzi, airejeshe furaha yangu ilopotea kwa miaka mingi, authamini moyo wangu, japo kidogo na mie nihisi nipo kwa hii dunia kwenye ulimwengu wa mapendo moyoni mwangu nipate kufarijika, hakika moyo wangu mpweke unahitaji kutulizwa:
 
Hahahahahas pole sana, hakikisha unatafuta wimbo wa Whitney Houston unaitwa THE GREATEST LOVE OF ALL

yasome yale mashairi vizuuuuri sana na ujitahidi kumwelewa! Kumtegemea mtoto wa mwenzio akupe raha utaishia kuishi maisha ya ku pretend ambayo yanaumiza zaidi kuliko kama ungeishi kwa uhalisia wako.
 
Ww mke mume mbona sielewi km mke tuwahi fursa tuanze na mtoko kesho nyama choma.

Ila tafuta tu utafanikiwa usivunjike moyo
 
Asante Elli nitautafuta
 
Ww mke mume mbona sielewi km mke tuwahi fursa tuanze na mtoko kesho nyama choma.

Ila tafuta tu utafanikiwa usivunjike moyo

Kiti moto au mbuzi maana za ng'ombe nimesikia zina shida si Salama sana kwa matumiz ya binadamu
 
Wazee wa fursa wameliona hili nadhan wanalifanyia kazi soon tatizo litatatuliw kwan tatizo lako ni dog tu
 
Hahahahahas pole sana, hakikisha unatafuta wimbo wa Whitney Houston unaitwa THE GREATEST LOVE OF ALL

yasome yale mashairi vizuuuuri sana na ujitahidi kumwelewa! Kumtegemea mtoto wa mwenzio akupe raha utaishia kuishi maisha ya ku pretend ambayo yanaumiza zaidi kuliko kama ungeishi kwa uhalisia wako.
Learning to love yourself,
It is the greatest love of all
 
Unatakiwa kujipenda mwenyewe kwanza, hao wengine wawe nyongeza ya furaha yako na kukusaidia kupiga hatua ktk maisha yako mf mke, mtoto
 
>>Nahisi nipo peponi,nikiona sura yako.
Penzi lako la thamani,hakuna mfano wako.
Napata hamu moyoni,kushika kiganja chako.
Kilichokuwa laini,nalainika mwenzako.
Nikuonapo usoni,ni nyororo ngozi yako.
Sikuachi asilani,milele mimi ni wako.
Wewe ni wangu mwandani,nifanye chaguo lako.
Nitie ndani moyoni,nisije kufa mwenzako.
Kwani kwangu u moyoni,kukuacha mimi mwiko.
Sebuleni na chumbani,kwangu uje kuwa jiko.
Ni shuka langu la ndani,kwako sina hangaiko.
Nitatulia kitini,nije pata pumziko.
Nisemeze sikioni,linitoke sikitiko.
Mrembo hadi gizani,hata hujapakwa piko.
Ungelikuwa angani,malaika peke yako.
Utamu wako mezani,nilizuri pishi lako.
Oho malaika wangu,ipooze roho yangu.
Kwako sipati uchungu,upo kwenye moyo wangu.
Nishike mkono wangu,utazame mboni yangu.
Utajiona mwenzangu,wewe ulo chungu changu.
Ivisha chakula changu,kitamu kiso kichungu.
Zawadi toka kwa mungu,ilofika hapa kwangu.
Naapa haki ya mungu,paka kifo wewe wangu.
Niseme nini mwenzako,nahisi nipo peponi.
Mazuri mahaba yako,yasiyouzwa sokoni.
Mazuri mahaba yako, hayapo hata dukani.
Shairi:NAHISI NIPO PEPONI.
Mtunzi:Idd Ninga wa Tengeru Arusha.
0655519736.
 
Acheni kutudanganya...anahitajika mtu wa kukupenda pia hata kama na wewe unajipenda
Afu una kesi kubwa na mimi ujue ooh lol

"The greatest happiness of existence is to love and to be loved"
But ni afya zaidi kuanza kujipenda wewe mwenyewe kabla ya watu wengine hawajaanza kukupenda. Na sio muda wote watu watakupa furaha unayoitaka, so it's better ukajifunza kujipa furaha wewe mwenyewe

Tunawish sana kupenda na kupendwa na wale tunaowataka, but ikitokea hakuna mtu anayekupenda in return, au hawajali ule upendo wako, utafanyaje? Utalazimisha watu kukupenda?, hell no. Afu ukijua kujipenda pia ndo unajua na thamani yako na ya furaha yako. So mtu akikuzingua unamuangalia tu afu unamcheka coz there is no way utaruhusu mtu apoteze furaha yako kwa kukutreat anyhow. You simply deserve to be happy, whether upo single au una mtu. Happiness is a choice
 
Nina tamani walau siku moja moyo wangu upate kutulia, nimpate wa kunienzi, airejeshe furaha yangu ilopotea kwa miaka mingi, authamini moyo wangu, japo kidogo na mie nihisi nipo kwa hii dunia kwenye ulimwengu wa mapendo moyoni mwangu nipate kufarijika, hakika moyo wangu mpweke unahitaji kutulizwa:

nichek kwa PM kama uko serious
 
Back
Top Bottom