Kilongwe
JF-Expert Member
- Feb 7, 2008
- 423
- 115
Ingawa wengi wetu wamekuwa wakifikiria sisi wana ICT tunaongoza kwa ubusy na hatuna muda wa kufuatilia mambo mengine,ukweli ni kuwa hilo sio kweli.Kuna wakati tunakuwa na muda wa kufanya mambo kadha wa kadha.Kwa wale walio site,mara nyingi hujiburidisha kwa miziki na movies pindi wanasubiria kifaa kirudi kwenye hali yake ya awali.
Binafsi pindi nimeboreka au mambo hayaendi ipasavyo kimbilio langu la kwanza ni kuangalia movies,kuna mtu aliwahi kuniuliza kwanini sio kuchat? Jibu linakuja unapoangalia movie pia unasoma kitu fulani ndani yake.
Swali linakuja,je ni movies gani watu wa ICT hupenda kuangalia? Au wewe kama mwana ICT je umevutiwa na movie gani ambayo ndani yake kuuna mambo mengi yanayohusiana na ICT? Swali hili lina majibu mengi ambayo yanategemeana na mtu husika.
Binafsi ninapenda sana kuangalia movies zenye masuala ya hacking au mambo ya uchunguzi wa masuala ya kompyuta(Computer forensic) kwa sana na ifuatayo ni orodha yangu.
One Point O - Hii ni moja ya movie ambayo biniafsi niliiangalia zaidi ya marambili ili kung'amua kila kitu kilichomo.Inaelezea mambo ya maprogrammer,niliipenda jinsi geek alivyokuwa akifanya mambo yake.
24 Hours - NImeipenda hii movie jinsi jamaa wanavyodili na teknolojia mpya,Cisco waliweka dola kibao ili kudhamini hii movie , sisi vijana wa Cisco wengi huwa tunavutiwa pindi tuonapo watu wakicheza na matechnolojia.
Live Free or Die Hard" ("Die Hard 4") Synopsis:- Ndani ya hii movie nilipenda pale jamaa walipovamia system za US na kuanza kuzima kila kitu haswaa pale walipoanza kujiongozea taa za barabarani ili kuruhusu maharamia kukamilisha mambo yao.
Mengi ya kusisimua ndani ya hii movie ila kunua kitu nimejifunza,inabidi uipende fani yako ili uweze kufanya vizuri kwenye hiyo fani.
Je wewe umevutiwa na movie ipi ambayo ndani yake kuna masuala ya ICT? sio lazima iwe ya nje hata kama nyumbani tuna movies zilizohusisha mambo ya ICT basi imwage dimbani na kutueleza umevutiwa na kitu gani ndani ya hiyo movie.