Movie ya kwanza ya Teknolojia kuchezwa na wa Tanzania

Teknolojia ni Yetu sote

JF-Expert Member
Apr 28, 2020
445
754
Tuwape hongera Azam Tv kwa kuthubutu kuleta movie yenye mifumo ya Teknolojia kwa mara ya kwanza nchini Tanzania Tena waigizaji wakiwa Watanzania.

Azam Tv wakishilikiana na Kampuni ya Power brush Studio wameweza kuachia movie ambayo inaitwa Eonii utaweza kuona kupitia Kingamuzi cha Azam tarehe 23/06/2023 kupitia channel ya Azam two.

Eonii Movie imekuja kubadilishi mtazamo mzima wa tasnia za filamu nchini Tanzania. ngoja tuwape maokoto kidogo kuhusu hii movie si unajua Teknolojia ni Yetu sote wapwa.

Eonii ni movie yenye mfumo wa sayansi za kufikilika (sayansi za Uongo) ambazo huitwa science fiction aka (sci-fi) , hii ni filamu inayohusisha Teknolojia za juu kabisa utakutana nazo ndani yake Kuna usaliti, mapenzi, mapambano, visasi na matukio mengine mengi tu.

Mfumo wa huu movie ni kuhusu Mwaka 2061 nchini Tanzania Teknolojia itakua imepiga hatua kubwa sana uvumbuzi mbalimbali wa Teknolojia utapatikana, ila utaweza kusababisha maafa maana Kuna watu walikua wana miliki ma roboti na kuleta usaliti kwa wengine.

Ni vita ya Maroboti na wanadamu kuweza kuiokomboa Tanzania utakutana na ile miroboti mikubwa kama ile ya kwenye transformers je ni nani wa kuikomboa Tanzania !!!

Inasemekana Gharama ya kuendesha hii movie mpaka kukamilika ilitumika kiasi cha zaidi ya milioni mia nne za kitanzania.

Hongereni Azam mmeweza kuleta mapinduzi makubwa ya filamu zetu tuache sasa kuigiza movie mtu ana Shati moja tu Toka movie ianze mpaka inaisha .

Ebu tuachie maoni yako unaonaje tasnia ya movie nchini Tanzania tutafika kweli tunapotaka au bado Sana !! View attachment 2656333View attachment 2656334
AzamTv%20%E2%80%93%202.jpg
mqdefault.jpg
 

Attachments

  • sddefault.jpg
    sddefault.jpg
    13.5 KB · Views: 20
Mara ya kwanza kuona tangazo nikasema mbona kamaa naangalia kitu nimekiona tayari… let’s wait labda macho yangu tu
 
Nimeiona gari ya mwaka 2008,Toyota IST old model katika mwaka 2061. Makosa madogo Kama haya yanaharibu maana nzima ya 'movie ya kiteknolojia'.

I hope safari nyingine tutaangalia details ndogondogo Kama hizo na kusahihisha makosa.

Naisubiri kwa hamu,mwanzo mzuri!!
 
Nimeiona gari ya mwaka 2008,Toyota IST old model katika mwaka 2061. Makosa madogo Kama haya yanaharibu maana nzima ya 'movie ya kiteknolojia'.

I hope safari nyingine tutaangalia details ndogondogo Kama hizo na kusahihisha makosa.

Naisubiri kwa hamu,mwanzo mzuri!!

Mkuu hata kwenye movie za wenzetu hio kitu inatokea mbona
 
Kwa mara ya kwanza Afrika Mashariki filamu ya kiswahili ya HD ya maroboti na kiwango cha kimataifa ya EONII yazinduliwa rasmi

Hii filamu ni kali na ni Quality ya HD azam wameleta mapinduzi nchini na Africa kwa ujumla.

Kongole Azam tv
FB_IMG_16875454402478314.jpg
FB_IMG_16875454200643741.jpg
FB_IMG_16875454168998520.jpg
FB_IMG_16875454112144919.jpg
FB_IMG_16875454141233392.jpg
 
Nimeona tangazo lao kuhusu hiyo filamu, nasubiri kuiona ndiyo nitoe maoni yangu.

Ila wanahitaji pongezi.

Nawapa 3/5
 
Back
Top Bottom