Movie za Bongo Siziwezi


Umenivunja mbavu na hio story ya jini linaloogopa magari.
 

Hivi wewe unaweza linganisha hizi muvi za sasa za akina Aunt Ezekiel na maigizo ya zamani ya akina mhogo mchungu,kibakuli, Seki au hata Jumba la Dhahabu na mengineyo au hata yanayoigizwa sasa hivi?,kikubwa ni kwamba hiz muvi zina kiwango cha chini mno na niabu,kuna mwanangu jsna alikuwa anaangalia na wenzie akawa ananiuliza "eti baba hawa kwenye hizi picha wanakaaga uchi tu" nilishangaa hata mtoto wa miaka minne anajua kuwa huwa wanavaa uchi? Na hapa sio kulinganisha kuwa eti tunapenda muvi za wazungu sio kweli,na watu wengi wanazipenda kwa sababu wanafanya vizuri na hizo tu kwani hata waigizaji wa Tamthiliya hapa Tanzania wanajitahidi sana na watu wa Comedy pia wako vizuri hao akina Ray muvi zao
nyingi hazina uhalisia wa kitanzania zinaigiza maisha ya kwenye Mahoteli makubwa makubwa na ya Ulaya zaidi,bora hata za Nigeria.

Mi nadhani ndugu yangu unazipenda sana hizo muvi za akina Ray,we endelea kutazama ndugu kila mtu na akipendacho lakini kwangu mimi nafuata kilicho bora!
 

We acha hizo yaani hata kama ni cha ovyo mtu apende tu kwa sababu ni cha Tanzania? mi mbona nayapenda maigizo/tamthiliya za bongo na Comedy? hizo muvi za akina Anti Ezekiel hazifai zaidi zaidi kimaadili!
 

Upo sahihi kabisa,nakumbuka ile tamthilia ya Jumba la dhahabu ilipendwa sana,na ilikuwa ikionekana ni tamthilia ya kiwango cha juu hapa bongo na waigizaji wake tuliwaona wa kiwango cha juu.Lakini kama sikosei mwaka jana waliirudia ila dah! Nilishangaa hivi tulikuwa tukiipendea nini,maana niliiona ovyo tu ukiliinganisha na movie zetu hivi sasa.
 
Kama mimi vile yaani zangu ni NOLLYWOOD kwa sababu zinamafunzo ndani yake. Simjui mwigizaji yeyote wa Bongo movie kwa jina

Dah! Mie hizo za wanaigeria siku hizi ndiyo sisiwezi kabisa yani bora bongo movie,maana story zao wanaigeria ndiyo zilezile toka miaka ile, hasa hasa utaona wanafanya uchawi mwishoni kanisani.
 
Dah! Mie hizo za wanaigeria siku hizi ndiyo sisiwezi kabisa yani bora bongo movie,maana story zao wanaigeria ndiyo zilezile toka miaka ile, hasa hasa utaona wanafanya uchawi mwishoni kanisani.

Siku hizi wamebadilika sana ziko za action na upelelezi sana.
 

Kwani movie za Kanumba ndiyo zilikuwa nzuri?
 

Movie zengine za zamani hapo ukiziangalia sasa hivi ni Sheeeda!
 

Hivi sasa unaweza kuziangalia zile tamthilia za itv za zamani ambazo hao akina Ray walipoanzia?
 
Baadhi ni nzuri na zina uhalisia kabisaa' mfano ni KIGODOLO imeongozwa na Zamrad
 

Tatizo zinawalipa ndiyo maana hawajisumbui kuboresha.
 
Juzi niliamua kuangalia "filamu" inayojulikana kama Funga Kazi iliyotolewa mwaka 2009. Humo ndani ni vioja vitupu. Sehemu iliyoniacha hoi ni pale mhusika mkuu, akiwa jela, alipokuwa akikumbuka jinsi alivyolazimishwa na majambazi kuwaua wazazi wake alipokuwa mtoto mdogo mwenye umri wa kama miaka mitano. Kilichonishangaza ni kwamba sebuleni kwa wazazi wake kulikuwa na TV flat screen. TV za aina hii zimekuja miaka ya karibuni. Haiwezekani mtu uonyeshe tukio la miaka 20 au 25 iliyopita halafu waonekane watu wanaangalia flat screen. Ni sawa na kuigiza tukio la miaka ya 1970 lakini humo ndani watu wanaendesha Toyota Mark X au Nissan Murano.
 
Muvi za kibongo ni lazma kuwe na sini watu wawili mwanamke na mwanaume wanafanya shopping katika duka la nguo au wapo bichi.

Na hapo ndio wanavuta hata robo saa ili kutafutia part two.
 
Kwa producer's hawa hawa, editer's hawa hawa, director's hawa hawa na actor's hawa hawa, hakutatokea mabadiliko kwenye bongo film, tunahitaji mawazo mapya toka kwa watu wapya kuleta mabadiliko, tatizo walio ndani wamejijengea uzio ili waendelee kuwepo.
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…