Movie za Bongo Siziwezi

uzuri wake movie inapoanza tu unajua itaishaje...so unaforward tu hadi last page
 
bongo movie S.Africa hapo inahusikaje sasa!
Aise.
Thats why nimasema hii inakuja kumshika kila mtu.
It is real BONGO MOVIE mkuu.
Hii itachezwa sehemu(nchi)tatu tofauti na lengo ni kuleta uhalisia wa story hii ambayo kwa mpenda filamu za hii itakua ni fursa nzuri kuona filamu ya kibongo iliyo kamilika.
 

Mkuu mjeda wa Tabora upo?
 

basi ikishatoka nistue....
 

kaka luka basi inatosha,onea huruma mbavu zangu mkuu.vp mitikasi lakini.habari za masiku.

twende kwenye mada:kuna hili tatizo la noise ktk movie zetu,mbaya zaidi sio real noise bali ni fake noise japo noise ni noise.

mfano scene inaonyesha ni usiku mtulivu na wahusika wapo chumbani wamelala,nje inasikika sauti ya vitoto nyumba ya jirani vinacheza,au unasikia sauti ya mtu anayetembeza sumu ya panya(sumu ya panya,nge, sisimizi,vitorobotooooo...).

unajiuliza ni watoto gani wanaocheza kimamama usiku wa manane?,au ni muuza sumu ya panya yupi anayetembeza bidhaa usiku mnene!!!.
hilo peke yake linaondoa uhalisia wa movie.

najua kuna mamia ya vigezo vinavyofanya "bongomuvizi" ziwe duni kiubora.wahusika wameshikiria kuibiwa kazi zao,waibiwe kwa ubora upi?.

siku nikititulia nitaeleza nini kifanyike ili movie za wabongo ziwe bora hata kama ni low- budget movie.
 
Bongo hawawezi kuwa na movie nzuri ikiwa wasanii wake wote wako pale kwa kujiuza tu na kulana uroda huko location kiasi kwamba wanasahau hata lines zao na kubaki kuboronga tu.
 
Njoo nikupe Series za Kaole enzi hizooo..haziishi hamu kuzitazama....achana na hawa waliofeli umiss Temeke,Kino na Ilala hata Miss Tz wameharibu kila kitu.....tatizo wameshindwa kufanya shughuli zingine wamekuja kutokea kwenye movies
 

Niko poa Kadoda, umesharudi bongo?

Tatizo sidhani kama hawa watayarishaji wa hizi tunazoita muvi wana muda wa kutembelea majukwaa kama haya ili kupata feedback ya kazi zao but its about time we changed jamani. Tusilazimishane tu kupenda visivyopendeka. Hiyo ishu ya sumu ya panya imeniacha hoi mkuu hahaha, umeua. Tutafutane kaka.
 
Mtu director,producer, screen play vyote vimeandikwa anafanya mtu mmoja!!!wanaigeria wametuacha sana binafsi nazifuatilia sana movie zao na cjawah kuchek nikawa bored..bongo movie hawapo serious na n conservantist kwa ujumla..
 

tukiacha teknolojia hata wao tu hawapo serious...kuna vitu vingine vinahitaji akili tu na kujiongeza..kwa mfano kuna movie ya kibongo nikaona eti jini linaagiza redbull bar na wakati wa kuvuka barabara jini linaangalia kulia na kushoto...sasa hapo si hata mtoto mdogo ataona they are not serious!!!
 

nilichoka kuna siku nlikua mbeya nikawa nasikiliza radio moja inaitwa bomba fm...marehemu kanumba alikua anafanyiwa interview...mtangazaji akamuuliza "kwa mwaka unaweza kufanya movie ngapi zako binafsi na za kushirikishwa" jibu lake likawa"nina uwezo wa kufanya movie zangu mwenyewe kila baada ya miezi miwili na za kushirikishwa naweza kufanya hata mbili kwa mwezi" jibu lake lilinipa majibu ya maswali yangu yote kwa nini bongo movies hazivutii.
 
Mimi huwa naziangalia ili nicheke maana vilivyomo humo ni vitimbi mwanzo mwisho kama hicho cha jambazi kuvua viatu mlangoni asichafue nyumba.
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…