Movie of the weekend: JOLT

Ferruccio Lamborghini

JF-Expert Member
Apr 15, 2020
1,664
2,517
intermittent explosive disorder ilimtafuna vilivyo, udogo wake hakuufaidi sababu ya maradhi hayo, hakuna aliependa kumkalia karibu bila sababu,
Watoto wenzie walimtenga, wazazi wake wakamshindwa pia, Lindy Lewis akapelekwa hospitali ya watu waliothirika na ugonjwa kama wake, huko pia alishindwa kuishi..
Jeshini palipoonekana ndo panamfaa, ni siku mbili tu kanali wa jeshi alipigwa nusu afe, serikali haikuhitaji mtu wa aina yake kambini, napo pia akaondoka...
Hakuna kazi aliyofanya akaimudu, hakuna mtu aliedumu nae kwenye maongezi kwa masaa mawili wasivurugane, hakudiriki kulala na mwanaume mpaka asubuhi halafu huyo mwanaume akatoka akiwa salama, haijawahi kutokea..
Lindy Lewis anaumwa, ugonjwa wake ni wa ajabu kuwahi kutokea, ana hasira, hapendi mtu hata akipiga makelele, hapendi kufokewa, hapendi kuudhiwa, hapendi kumuona mtu anaonewa, yaani ye hapendi tu...
Kuumwa linaweza kuwa sio tatizo kubwa, shida inakuja alichojaaliwa kwenye mwili wake, yeye ni untouchable machine, kaumbwa na nguvu za ajabu, mwili wake unajua kila aina ya pigo la kumwadhibu binadamu..
Kwahiyo ni rahisi tu, anamiliki hasira za kutosha kama ugonjwa, na ana nguvu za kutumia kama silaha, wapi utamgusa!...
Suluhisho pekee la maisha yake ni Dr. Ivan Munchin, yeye alimvalisha vazi la waya kwenye mwili wake, akamkabidhi na batani mkononi,
kila anapopatwa na hali ya hasira, basi ataibonyeza, mwili wake utapiga shoti, itakwenda mpaka kwenye moyo, na hapo hasira zitaondoka, akatakiwa aishi hivo maisha yake yote yaliyobaki..
Msichana wa miaka ishirini na nane akawa mtumwa wa hasira zake mwenyewe, rafiki yake akawa ni dokta tu, hana mwingine, akaipokea hiyo hali, na akaiishi...
Matukio yalimpita, aliziona hasira kila sehemu, lakini kwa kuwa tiba alikuwa nayo mkononi, basi alikubali kuitii, mpaka ilipokuja siku ya leo..
Alikutana na Justin, kijana mtanashati, akampenda, akaonana nae kwa usiku mmoja tu, alizoea kuwaadhibu wanaomuudhi nje, leo alienda kuadhibiwa yeye ndani..
Lindy Lewis kwa mara ya kwanza akakubali kuwa kapenda, hakuwa na hasira, alifanya kila kitu kama kasomewa dua, alijishangaa, hadi waya alizovaa kama dawa alizivua, batani ya hasira akaiweka mezani, hakika mapenzi yalimkamata..
Asubuhi alijiona na yeye anastahili kuishi, aliamini kumbe furaha ilikuwepo ila haikuja kwa wakati sahihi, akasahau kwa muda kuwa anaumwa ugonjwa wa hasira kupitiliza, akajiweka kwenye watu wanaotakiwa kuyafurahia maisha, ila alikosea kuamini..
Asubuhi alimpigia simu mpenzi wake haikupatikana, mchana ikapokelewa na polisi, taarifa aliyoipata ilimuweka chini kwa dakika kadhaa na asijue anawaza nini, alilia sana...
Ni kweli, Justin wake alieonana nae kwa siku moja tu na kuamini kaipata furaha yake, amekutwa amepigwa risasi mbili kichwani, akiwa kavaa shati lile lile alilovaa wakati analala nae, Lindy alilia tena..
Hakuamini kuwa furaha yake iliyokuja ghafla, akaamini ataishi nayo, eti imechukuliwa kwa usiku mmoja tu, akajiona hana bahati, akajichukia sana..
Polisi hawakuwa na njia zaidi ya kufanya upelelezi, ni huo upelelezi wa polisi ndio uliozua kizaazaa, kwanini!, ntawaambia!...
Lindy Lewis sio mnyonge, alivaa waya ili atulize hasira na zile nguvu alizonazo tu, akawaambia polisi aliemuua mpenzi wake ataokotwa akiwa maiti, polisi hawakuiamini kauli yake, wakaishi na mwili wake mdogo kama ulivyo, nao walikosea...
Alipomgundua aliesababisha kifo cha mpenzi wake alimfata ili ampe sababu, kosa walilofanya wakamkamata, kisha wakamvua zile waya, na wakampokonya ile rimoti ya kupunguza hasira, bonge la kosa..
Waliitamani ardhi ipasuke, walikuwa wamemkorofisha mtu asiekuwa na cha kupoteza duniani, Lindy Lewis anaupenda ugomvi na ugomvi unampenda yeye..
Kama siku zote huwa anapiga na kuua watu kwa sababu
tu wamemuudhi, leo aliipata sababu nzuri tu ya kuwapunguzia matatizo duniani, mji ukakubali, mitaa ikaitika..
Ni vita ya polisi, majambazi na msichana mmoja tu, ndio, Lindy alikuwa peke yake, na alidhamiria kuumaliza huu mchezo kabla jua halijatoka...
Nani ataamini mpenzi wa Lindy iliesemekana amekufa ndio adui wa movie hii?, hamjaelewa?, ni hivi, Justin, mpenzi wa LIndy, ndio mastermind wa huu mchezo, hakupigwa risasi, na hakufa..
Kwanini?, ilikuwaje?, asa itakuwaje?, nendeni mkaangalie...
# JOLT2021 ..

©Kaisal Ally (Ninja)
 
Kaisal Ally (Ninja)
well said mzee huu mziki ni hatari
 
Niliiangalia nikaishia kati si kuelewa kabisa action zake ila hapa kwa yule jamaa kua mastermind ndo kumenifanya nitake kwenda kuimalizia
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom