Hivi masoko kuwaka moto chanzo huwa ni nini?
Masoko hujuisha watu wa kaliba mbalimbali.
Namaanisha, wapo wanaojitambua na wasio jitambua
1. wengine wanachukua umeme wajisambazia hovyo hovyo kwenye vyombo vya umeme hata kwa kutumia nyaya laini kabisa za speaker.
2. Mama ntilie analaza maharage yake kwenye mkaa ili asubuhi akute yameiva
3. wengine wanapikia gesi ila kwenye kauchochoro hivyo ni rahisi moto kushika vitu na kusambaa
4. Mlundikano wa vitu hivyo moto kidogo, unashindikana kuzimwa na hivyo kuenea/kusambaa
5. Kutumia bidhaa feki za umeme hasa huko huko masokoni. Feni feki, extension feki, radio feki, TV feki nk nk ni rahisi kulipuka
6. Hujuma
Ushauri wangu
1. Kwenye ujenzi wa Masoko; Mama Ntile na wapikaji wote vya vyakula wawe na jengo lao mkabala na jengo kuu la soko ILI moto ukitokea uwe rahisi kupambana nao.
2. watu wanaouza bidhaa zinazo endana/fanana wakae upande mmoja
3. Soko kuu liwe sehemu ya kuuzia na sio sehemu ya stote (Masoko yawe na store ndogo ndogo ambazo wauzaji wanaweza kukodisha na kuhifadi bidhaa zao.
4. iwe maarufuku kutumia frame ya soko la umma kama store. Frame ni sehemu ya kuuzia bidhaa na sio store
5. Kama huna elimu ya kawaida ya umeme, omba ushauri/msaada unapotaka kusambaza umeme kwa vyombo vingi nyumbani/chumbani kwako.