Moto Kiwanda cha Mafuta na Vipodozi cha Mamujee, Tanga

Moto Kiwanda cha Mafuta na Vipodozi cha Mamujee, Tanga

Richer

JF-Expert Member
Joined
Jun 9, 2025
Posts
2,297
Reaction score
4,027
Kampuni ya usambazaji wa mafuta ya GBP, iliyopo jijini Tanga, imeungana na vyombo vingine vya usalama, likiwemo Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, katika juhudi za kukabiliana na moto mkubwa uliolipuka na kuendelea kuteketeza Kiwanda cha Mafuta na Vipodozi cha Mamujee.

Moto huo ulianza kuwaka usiku wa Julai 24, majira ya saa tatu, na juhudi za kuuzima zimekuwa zikiendelea hadi sasa kwa ushirikiano wa wadau mbalimbali kutoka ndani na nje ya mkoa wa Tanga.

Katika taarifa ya awali kwa vyombo vya habari, Kaimu Kamanda wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Mkoa wa Tanga, Mrakibu Mwandamizi Ndatala Issa, amesema kikosi chake kilifika eneo la tukio mara baada ya kupokea taarifa na kuanza haraka shughuli za uzimaji moto huo hatari.

Juhudi zinaendelea kufanyika kwa nguvu zote ili kudhibiti moto huo usienee zaidi na kuleta madhara kwa maeneo ya jirani.




Chanzo: Global online Tv
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom