Moshi hongereni kwa usafi; abiria aaibika

Moshi hongereni kwa usafi; abiria aaibika

32287f7847a7d66633783dc45564fab4.jpg
7a41850b27e9004da0e28d3ff69a1f6e.jpg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Dar nyo.ko kabisa,juzi tuko kwenye foleni Tazara,mbele yangu kulikuwa na mtu mzima yuko na Prado V8,bila aibu akatupa chupa ya mkojo chini.Alafu mida yenyewe saa kumi na moja jioni.Watu wamelaaniwa na mishipa ya aibu hawana.Nadhan mzigo ulimbana akaona isiwe tabu.
Umeshawahi kubanwa na mkojo au haja kubwa ukiwa kwenye mazingira tatanishi mkuu!?
Mkojo hauna adabu kabisa. Kuna siku maeneo ya Sinza mapambano kuna jamaa alizua taharuki watu wakifikiri ni mwizi,kumbe alikuwa kabanwa na inye na ilikuwa imeshaanza kupasua mwamba.
 
Marekebisho:

Hakuna mizani ya Himo... Bali mizani ipo Njia Panda..... Huo Usafi unaozungumzia upo Moshi mjini.... Himo ipo Vunjos
 
Marekebisho:

Hakuna mizani ya Himo... Bali mizani ipo Njia Panda..... Huo Usafi unaozungumzia upo Moshi mjini.... Himo ipo Vunjos
Hiyo njia panda iko wapi kama sio Himo?
 
Umeshawahi kubanwa na mkojo au haja kubwa ukiwa kwenye mazingira tatanishi mkuu!?
Mkojo hauna adabu kabisa. Kuna siku maeneo ya Sinza mapambano kuna jamaa alizua taharuki watu wakifikiri ni mwizi,kumbe alikuwa kabanwa na inye na ilikuwa imeshaanza kupasua mwamba.
Mwamba gani huo mkuu?!
 
Mijitu mingine sijui imezaliwa wapi unakuta jitu zima linakula ndizi maganda linatupa popote. Ustaarabu wa kikanda, kiwilaya, kimkoa mpaka kitaifa huanza na mtu mmoja mmoja, sasa kama huyu mtu mmoja mmoja tunaemtegemea ajenge ustaarabu anakuwa pumbavu hivi tutasonga Kweli.
 
Wakuu mlio wahi fika Moshi Kilimanjaro katika hili la usafi mtaniunga mkono.
Wakazi wa Moshi mjini na viunga vyake kwa kiasi flani wamejua umuhimu wa usafi kwani hawahitaji kupigiwa kelele.

Rais alipotoa tamko la usafi wa nchi nzima kufanya usafi Jumamosi ya kwanza ya kila mwezi, halikuwahusu wakazi wa Moshi kwani kwao usafi ni jadi yao tofauti na mikoa, manispaa na majiji mengine nchini.

Nikiwa safarini kupitia Moshi, nimeshuhudia abiria mwenzetu akiaibika bila kutegemea.
Jamaa akiwa anapiga vyombo a.k.a bapa amejikuta matatani baada ya kutupa chupa nje ya gari kwa kupitia dirishani wakati gari likiwa mizani eneo la Himo.​

Baada ya kutupa chupa nje, tulishuhudia akina mama wauza mboga, matunda nk. wakipiga kelele utafikiri wameona jambazi. Ndipo kondakta alilazimika kufuatilia kulikoni, ndipo alipojuzwa kuwa abiria wako anachafua mji wetu.
Kondakta kwa ujasiri alimsaka mhusika na kumpata na kumwamuru jamaa ashuke kwenye gari akaokote au atoe faini ya 50,000.

Huu ndio uzalendo wa kupenda mazingira na nchi yako.
Binafsi huwa najiskia kichefuchefu kuona mtu anakunywa maji na kutupa chupa ovyo au uchafu mwingine.

Wito: Watanzania tubadilike, tutunze mazingira.

Wakuu wa mikoa, mabwana afya na wenye dhamana wahamasishe na kuwajengea wananchi tabia ya usafi.
HONGERENI WAKAZI WA MOSHI
 
Back
Top Bottom