Moshi hongereni kwa usafi; abiria aaibika

Moshi hongereni kwa usafi; abiria aaibika

inakera sana abiria anatupa taka nje ya gari kupitia dirishani wakati ndani ya gari kuna vyombo vya kuweka takataka.
 
Moshi kilakitu tumebarikiwa mfano Elimu,Matajiri,Usafi duhh ama kweli siiiiishi moshi bahati mbaya
 
Wakuu mlio wahi fika Moshi Kilimanjaro katika hili la usafi mtaniunga mkono.
Wakazi wa Moshi mjini na viunga vyake kwa kiasi flani wamejua umuhimu wa usafi kwani hawahitaji kupigiwa kelele.

Rais alipotoa tamko la usafi wa nchi nzima kufanya usafi Jumamosi ya kwanza ya kila mwezi, halikuwahusu wakazi wa Moshi kwani kwao usafi ni jadi yao tofauti na mikoa, manispaa na majiji mengine nchini.
Nikiwa safarini kupitia Moshi, nimeshuhudia abiria mwenzetu akiaibika bila kutegemea.
Jamaa akiwa anapiga vyombo a.k.a bapa amejikuta matatani baada ya kutupa chupa nje ya gari kwa kupitia dirishani wakati gari likiwa mizani eneo la Himo.
Baada ya kutupa chupa nje, tulishuhudia akina mama wauza mboga, matunda nk. wakipiga kelele utafikiri wameona jambazi. Ndipo kondakta alilazimika kufuatilia kulikoni, ndipo alipojuzwa kuwa abiria wako anachafua mji wetu.
Kondakta kwa ujasiri alimsaka mhusika na kumpata na kumwamuru jamaa ashuke kwenye gari akaokote au atoe faini ya 50,000.

Huu ndio uzalendo wa kupenda mazingira na nchi yako.
Binafsi huwa najiskia kichefuchefu kuona mtu anakunywa maji na kutupa chupa ovyo au uchafu mwingine.

Wito: Watanzania tubadilike, tutunze mazingira.

Wakuu wa mikoa, mabwana afya na wenye dhamana wahamasishe na kuwajengea wananchi tabia ya usafi.
HONGERENI WAKAZI WA MOSHI
Asante mkuu, chupà ishu kubwa sana jaribu hàta maganda ya Karanga uone
 
Twapaswa kubadilika, miji yetu inanuka sana, hasa majiji bila kuisahau Dar. Keenja aliliweza jiji
Adui wa Usafi wa Mimi yetu ni Wamachinga has a baada ya kupewa Ruhusa ya kutumia maeneo ya katikati ya Mimi Wapendavyo. Bus Stand, Sidewalks, barabara za kati kama vile za Kariakoo. Dar es salaam wali, mhogo, mishkaki, maandazi vinapikiwa juu ya barabara za lami za Mji na kumwaga Maji machafu. MaDc na MaRc hawatakiwi kuwasema.
 
Back
Top Bottom