Moshi hongereni kwa usafi; abiria aaibika

Moshi hongereni kwa usafi; abiria aaibika

Wakuu mlio wahi fika Moshi Kilimanjaro katika hili la usafi mtaniunga mkono.
Wakazi wa Moshi mjini na viunga vyake kwa kiasi flani wamejua umuhimu wa usafi kwani hawahitaji kupigiwa kelele.

Rais alipotoa tamko la usafi wa nchi nzima kufanya usafi Jumamosi ya kwanza ya kila mwezi, halikuwahusu wakazi wa Moshi kwani kwao usafi ni jadi yao tofauti na mikoa, manispaa na majiji mengine nchini.

Nikiwa safarini kupitia Moshi, nimeshuhudia abiria mwenzetu akiaibika bila kutegemea.
Jamaa akiwa anapiga vyombo a.k.a bapa amejikuta matatani baada ya kutupa chupa nje ya gari kwa kupitia dirishani wakati gari likiwa mizani eneo la Himo.​

Baada ya kutupa chupa nje, tulishuhudia akina mama wauza mboga, matunda nk. wakipiga kelele utafikiri wameona jambazi. Ndipo kondakta alilazimika kufuatilia kulikoni, ndipo alipojuzwa kuwa abiria wako anachafua mji wetu.
Kondakta kwa ujasiri alimsaka mhusika na kumpata na kumwamuru jamaa ashuke kwenye gari akaokote au atoe faini ya 50,000.

Huu ndio uzalendo wa kupenda mazingira na nchi yako.
Binafsi huwa najiskia kichefuchefu kuona mtu anakunywa maji na kutupa chupa ovyo au uchafu mwingine.

Wito: Watanzania tubadilike, tutunze mazingira.

Wakuu wa mikoa, mabwana afya na wenye dhamana wahamasishe na kuwajengea wananchi tabia ya usafi.
HONGERENI WAKAZI WA MOSHI
Tunashukuru bwana mchafu

thA God thA bubbs!!
 
Usafi ni hulka ya mtu hata majumbani mwetu tunamoishi baadhi yao ni shida aje na ujasiri wa kusafisha mji.

Sent using Jamii Forums mobile app

...Kama alivyosema mlete mada, hiyo hulka ya uchafu labda iishie huko huko nyumbani kwani kwa Moshi akijifanya ni hulka mshahara wote utaishia kwenye faini ya elfu 50 kwa sababu wale mgambo wa pale Moshi wakikukamata kwa kosa la uchafuzi wa mazingira, na ukalipishwa nao wanapata percent yao kwa kazi nzuri ya kudhibiti hao wenye hulka ya uchafu.
 
Moshi kusafi pongezi Kwa uongozi wa cdm pia!
Wana mikakati mizuri ya kupambana na uchafu
Rc dar ameshindwaa Issue ya usafi dar mikakati Yao mibovu

Ova
 
Moshi kusafi pongezi Kwa uongozi wa cdm pia!
Wana mikakati mizuri ya kupambana na uchafu
Rc dar ameshindwaa Issue ya usafi dar mikakati Yao mibovu

Ova
Dar hakuna mkakati wowote wa usafi
 
Hello brother...Ndio umeondoka kimya kimya Hata haujaniaga
 
Enzi izo sikukuu tunaenda Moshi kwa babu Timbirini,basi tukienda kanisa tunaonekana watoto wa mjini kinoumer maana mavazi tuliyokuwa tunapiga ma jeans ya Savco enzi izo tunaonekana wajanja.
Kama ulivaa savco ww ni muhenga mwenzangu
 
xsmas huko vijijini ndo mbwembwe zinazidi kipindi icho njia za kuingia nyumbani zinavyochongwa ukoka wake nyingine wanaziandika kwa unga wa mbao (maranda) yani ilikua fulu kutambiana asubuh mda mnaenda kanisani unajua kabjsa kweli kuna sikukuu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom