Moshi hongereni kwa usafi; abiria aaibika

Glenn

JF-Expert Member
May 23, 2015
65,787
156,908
Wakuu mlio wahi fika Moshi Kilimanjaro katika hili la usafi mtaniunga mkono.
Wakazi wa Moshi mjini na viunga vyake kwa kiasi flani wamejua umuhimu wa usafi kwani hawahitaji kupigiwa kelele.

Rais alipotoa tamko la usafi wa nchi nzima kufanya usafi Jumamosi ya kwanza ya kila mwezi, halikuwahusu wakazi wa Moshi kwani kwao usafi ni jadi yao tofauti na mikoa, manispaa na majiji mengine nchini.

Nikiwa safarini kupitia Moshi, nimeshuhudia abiria mwenzetu akiaibika bila kutegemea.
Jamaa akiwa anapiga vyombo a.k.a bapa amejikuta matatani baada ya kutupa chupa nje ya gari kwa kupitia dirishani wakati gari likiwa mizani eneo la Himo.​

Baada ya kutupa chupa nje, tulishuhudia akina mama wauza mboga, matunda nk. wakipiga kelele utafikiri wameona jambazi. Ndipo kondakta alilazimika kufuatilia kulikoni, ndipo alipojuzwa kuwa abiria wako anachafua mji wetu.
Kondakta kwa ujasiri alimsaka mhusika na kumpata na kumwamuru jamaa ashuke kwenye gari akaokote au atoe faini ya 50,000.

Huu ndio uzalendo wa kupenda mazingira na nchi yako.
Binafsi huwa najiskia kichefuchefu kuona mtu anakunywa maji na kutupa chupa ovyo au uchafu mwingine.

Wito: Watanzania tubadilike, tutunze mazingira.

Wakuu wa mikoa, mabwana afya na wenye dhamana wahamasishe na kuwajengea wananchi tabia ya usafi.
HONGERENI WAKAZI WA MOSHI
 
Afadhali umesema wewe mkuu maana tungesema akina sie tungeonekana tunapiga promo
 
Usafi ni tabia,

Unaweza kuanza kwa kumjengea mwanao tabia ya jinsi ya kulinda mazingira kwa kutokutupa takataka za aina yeyote ile hovyo hovyo.
 
Mkuu kuna mahali ukipita pale usalama magomeni kuna harufu mbaya sana,yani kuna nukaa balaa,alafu kuna vingunguti karibu na daraja,wanachoma sijui ni mapembe ya ng'ombe.Watu wa maeneo hayo sijui wanaishije.
Mkuu Dar yetu ni jipu, kila kona mifereji imejaa maji machafu hadi huwa najiuliza wahusika wako wapi?
Japo jukumu la usafi ni letu wote
 
Nimepishana na dereva wa daladala hapa Boko kwa Mpemba karibia na Hisaje /magengeni anatupa chupa ya mikojo Dar usafi OO aka FaFaFa

Sent using Jamii Forums mobile app

Dar nyo.ko kabisa,juzi tuko kwenye foleni Tazara,mbele yangu kulikuwa na mtu mzima yuko na Prado V8,bila aibu akatupa chupa ya mkojo chini.Alafu mida yenyewe saa kumi na moja jioni.Watu wamelaaniwa na mishipa ya aibu hawana.Nadhan mzigo ulimbana akaona isiwe tabu.
 
Back
Top Bottom