Morogoro: Seleman Msindi (Afande Sele) ajiunga na CCM

Morogoro: Seleman Msindi (Afande Sele) ajiunga na CCM

Mwanamuziki Selemani Msindi "Afande Sele", ametangaza kujiunga rasmi na CCM leo Mkoani Morogoro, na kupokewa na Rais John Magufuli [HASHTAG]#MwananchiUpdates[/HASHTAG]
29186395_10156257359624339_819016204256542720_n.jpg
 
Kwa hali aliyokuwa nayo ilikuwa lazima ajiunge ccm

Alikuwa hana tena la kufanya, usanii hoi, kiuchumi chali, kwa hiyo ilibidi atafute tu njia ya kuchomokea, hata hivyo hana atakalopata CCM kwa sasa
 
Mvuta bangi afande Sele kajiunga na ccm kwenye uzinduzi wa kivanda cha sigara yah hapo ndio mahala pale moshi juu ya moshi
 
Amethibitishwa au amejiunga?

Dikteta anasema "Wenzao wanajiunga huku na wao wanabaki kule kuandamana"
 
Hizi ndio siasa zetu kama comedy huku walishangilia Wema ,baadaye akarudi na leo nao wamempata msindi.Hizi oya oya ndio zinafanya mpaka wanasiasa niwaone watu waajabu kwani wanaupeo mdogo sana.
 
Aliwahi kutia nia kugombea ubunge akadhani atakuwa kama profesa j au sugu. Walipomkata ndio sasa bado anahangaika. Anadhani ccm watakuwa hawana akili hadi wampe nafasi ya kugombea ubunge?! Imekula kwake hiyo.
 
Shughuli za kiserikali jpm na polepole wanafanya siasa majukwaani. Upinzani unaambiwa jukwaani mpk 2020 cjui ujasili huu wa kuvunja katiba na sheria unaupata wap
 
Msanii mkongwe nchini Afande sele ametangaza rasmi kujiunga na Chama cha Mapinduzi (CCM) leo mbele ya Rais Dkt. Magufuli kwa lengo ka kuunga mkono jitihada zake anazozifanya katika kupigania na kukiomba chama kimpokee kama kijana wao


Afande Sele ametoa kauli hiyo wakati alipokuwa anatumbuiza muziki kwa wananchi wa mkoa wa Morogoro walioweza kuhudhuria shughuli za uzinduzi wa kiwanda cha Sigara mkoani humo na Rais Magufuli.


"Nataka nimuhakikishie Mhe. Rais Dkt. John Magufuli kwamba mimi ni mtu wakufikiri, mbishi na mgumu sana katika kukubali jambo fulani lakini niseme kwa uwazi kabisa tangu ulipochukua madaraka ya kuwa Rais na Mwenyekiti wa CCM umeweza kuinyosha nchi na kukisafisha chama chako na kimeweza kurudi katika uimara wake kama alivyokuwa anataka muasisi wetu wa taifa Hayati Mwalimu Julius Nyerere lakini leo kimekuwa hivyo", amesema Afande Sele.


Pamoja na hayo, Afande sele ameendelea kwa kusema "naomba nikupongeze sana kwa hilo lakini kama haitoshi naomba nikuhakikishie kwamba leo hii kutoka kwa dhati ya moyo wangu nimeamua nisimame upande mmoja na wewe ili nisiachwe katika maendeleo.


"Ninaamini kabisa Mhe. Rais sasa hivi Tanzania kama gari basi dereva ametulia na gari linakwenda na mimi kama abiria niachwe ninywe soda yangu kwa amani kwasababu naamini kabisa chombo chetu kinaenda sehemu salama na sipendi kesho historia ije kunihukumu kwa watu wale ambao hawakuchangia walichonacho katika kufikisha mahali kinapoenda.


"Nawaomba viongozi ngazi ya mkoa wa CCM mnipokee kijana wenu nije kuongeza nguvu", amesisitiza Afande sele.

Screenshot_2018-03-15-14-50-41-1-1.jpg
 
Uma**ya wa kisiasa,
Biashara zake zimekufa.
mke kamkimbi kamwächia mtoto anaitwa Tunda.

kajaribu kufuga samaki wapi?

kaona wenzie wanapata hela za kampeni huku ZITTO kamtosa afande ndiyo kaamua kuhama,mkia wake bado upo,awaulize akina katambi wamezunguka pale Lumumba mpaka wameamua kurudi Tabora kuĺima tumbaku
 
Back
Top Bottom