Morogoro: Mbaroni kwa kuiba bango lenye picha ya Rais Samia

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Feb 7, 2022
2,296
5,431
Jeshi la Polisi Mkoa wa Morogoro linawashikilia watu wawili kwa shutuma za kuiba bango lenye picha ya Rais Samia Suluhu Hassan pamoja na vitambaa vyenye rangi ya bendera ya Taifa ambavyo hutumika kupambia jukwaa.

Kamanda wa Polisi mkoani humo, Fortunatus Muslim amesema waliokamatwa Emanuel John na Dickson Deus wote wote ni wakazi wa Morogoro.

Musilimu ameongeza kuwa Bango hilo lilitakiwa kutumika katika sherehe za uzinduzi wa miradi ya Jeshi la Magereza jijini Dodoma.



Chanzo: UFM
 
Kimsingi bendera ya taifa na picha ya rais havipo mikoani siku nyingi na ukuliuliza unaambiwa makao makuu hawajaleta kwenye mabohari ya serikali.
 
Issue ilivyokua ni hao walipewa kazi ya kuandaa hivyo vitu. Hawakulipwa, ndio wakaamua kuondoka navyo. Wala hawakuiba
Baadhi ya viongozi wa serikali wanapenda sana kuwafanyisha kazi watu bila posho wala malipo wakati wenyewe wamejilipa maelfu ya fedha bila jasho!

Waachiwe haraka na kulipwa fedha zao!
 
Hali ya uchumi ni mbaya sana.

Kinana anapaswa kuishauri vyema serikali.
 
Back
Top Bottom