Morogoro: Askari ajiua kwa uzembe wa uongozi wa jeshi la polisi

Zubedayo Kaelezea vizuri mwaka jana mwezi novemba uzi wenye maelezo ya kumshutumu Msangi kushirikia na majambazi uliandikwa na huyu afande anaesadikiwa amekutwa amejinyonga Morogoro, Msangi kipindi hicho alikuwa Morogoro kikosi cha kuzuia ujambazi na akina Kimaro a.k.a Saba sita.
wana JF wengi wako makini kusoma na kuchangia tafadhali Ulimboka hajafa yupo!! lakini Msangi aliyehusika kwa Uli ndiye aliyetajwa na Dunga mwezi November,2011
 
Unajua damu ya mtu haipotei bure,na mungu huwa hapendi watu wake waangamizwe,hii inaonyesha jinsi gani hao jamaa wameacha nafasi kwa mtu yeyote mwenye akili kujua huyu jamaa hajajinyonga,haiwezekani nguo ichafuke kwa vumbi inamaana kuna kilichotokea kwanza kabla ya hapo.Na kwanini afe akiwa hajaning'inia mtini?Ila kwa nchi yetu litapita tu,ingekuwa kwa wenzetu ingechukua hata miaka kumi ila ukweli ungejulikana na wahusika wangelipia mabaya yao.
 

tizama mkono wake wa kushoto,utaona ana koti lake lina vumbi na hata mkono wake wa kulia juu utaona kuna vumbi ktk kote,sasa hatuelewi je kabla ya kujinyonga alijirusha chini?
na ukitizama vyema mti aliojifunga,kama angejifunga vyema isingekuwa rahisi kufa kwani akining'inia ni lazima angegusa mti na isingekuwa rahisi kufa maana kamba haipo ktk maunganisho ya mti na slop ya mti na mahali kamba ilipofungwa si rahisi kwa mtu anae jinyoka kupata madhara

tunauzoefu kwani tumekaa iringa na hawa watu ni wataalamu wa kujinyonga
 
inasemekana mshkaj alijinyonga mwenyewe, na cku moja kabla ya kifo chake alionekana akinywa pombe sana usiku na kuvua nguo zote mbele ya watu, askari wenzake walimsihi avae nguo na akafanya hivyo but saa 11-asub ndio akakutwa kajinyonga.
 

Nakataa katakata dhana ya kwamba kijana huyu alijinyonga kwani alikutwa amesimama na si kuning'inia! isitoshe alikutwa na mavumbi kwenye nguo kiashirio cha mapambano kabla ya kuuwawa. Hii ni aibu nyingine kwa Jeshi la Polisi na IGP Mwema. Tungekuwa na serikali inayowajibika IGP Mwema angekaa pembeni, uchunguzi huru kuitishwa na ukweli kuanikwa; ukweli ambao ungemsafisha au kuhalalisha kuondoka kwake. Tunataka mabadiliko katika uwajibikaji katika Katiba mpya, uwajibikaji katika ngazi zote; kuanzia Rais hadi Tarishi. Kama Jeshi hilo limeshindwa kumlinda Polisi mwenzao aliyejitoa mhanga kuwataja wahalifu itakuwaje kwa raia wa kawaida?
 
Kuna kipindi flani songea kuna jamaa alikutwa kajinyonga akiwa kachuchumaa.
Tamthilia ya ACP Msangi inaendelea hususani ukizingatia ni mmoja wa askari walihoshutumiwa na marehemu huyu.

Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums
 
Kama inahusiana na Usalama wa Taifa wala msijichoshe kuichapa kwani ikiwekwa hapa Jamvini haitadumu zaidi ya dakika tano kabla mods hawajaifuta halafu ukicheza ucharazwe na Ban la mwezi pamoja na IDs zako nyingine zote waziunganishe
 
Natamani ningefanya mimi hiyo 'post-mortem'....

Mkuu hivi vitu sio hata vya kutamani, unaweza kuishia kuujua ukweli jinsi ulivyo ila ukaishia kutoa ripoti uliyopewa uitoe na sio iliyotokana na ulichopata kama post mortem findings, mwisho wa siku unaishia kupewa TCAs mwenyewe...!
 

Hilo ndilo walilonalo viongozi wa kidanganyika
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…