Morogoro: Askari ajiua kwa uzembe wa uongozi wa jeshi la polisi

Toa chanzo ili kama kuna ukweli ndani yake tujue tu kwamba nchi iko mikononi mwa jeshi ili nasi tujipange kukimbilia nchi jirani kama wakimbizi kuyanusuru maisha yetu.
 
huyu jamaa kauliwa harafu wakamtundika,yaani nchi hii imejaa madudu kibao,yaani nasikia hasira mpaka kichwa kinauma,natamani niwafate mafisadi wote na AK 47 niwachape risasi,.wakuu mtanisamehe sana,ila naombea yanayotokea syria yatokee bongo,nitakuwa wa kwanza kufyatua risasi ya kuwaangamiza mafisadi wote wa ccm
 
Askari Polisi aliyemshutum ACP Msangi na mshutumiwa namba moja wa utesaji na vipigo vya Olimboka kakutwa kanyongwa na kamba na kuning'ing'ia katika daraja la shani mjini Morogoro

ASKARI jasiri aliyejizolea sifa mkoani hapa kwa kitendo chake cha kuwataja hadharani baadhi ya askari wenzake akiwashutumu kwa tuhuma mbalimbali zikiwemo za kushirikiana na majambazi kufanya uharifu, Donald Julius Mathew, mwenye namba ya jeshi la polisi F3276 amekufa akidaiwa kujinyonga. Mwili ya afande huyo ambaye ni maarufu mkoani hapa kwa jina la Dunga umekutwa ukiningin'ia juu ya mti eneo la Daraja la Shani ambalo liko katikati ya Mji wa Morogoro. Dunga aliwalipua maafande zaidi ya sita ambao walihamishwa na Mkuu wa Jeshi la Polisi IGP Said Mwema na yeye kuhamishwa mkoa wa Singida. Hata hivyo, Dunga aligomea uhamisho huo akipinga watuhumiwa kutochukuliwa hatua. Sababu alizotoa Dunga zinaelezwa katika barua aliyomwandikia Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi aliyoitoa kwa mtandao huu na ambayo tunaichapisha.
 
Bado ni kitendawili si sahihi kulihusisha jeshi zima inawezekana marehemu kajiua mwenyewe au ameuliwa, tuviachie vyombo vya usalama vifanye uchunguzi wake.

Chama
Gongo la mboto DSM

Uchunguzi upi unaoukumbuka ambao umewahi kutoa majibu yenye tija au ukweli?Hao hao polisi walikuwa wanashtumiwa na Marehemu kabla hajafa ndiyo waunde kamati ya Uchunguzi?Lets be serious
 
Askari Polisi aliyemshutum ACP Msangi na mshutumiwa namba moja wa utesaji na vipigo vya Olimboka kakutwa kanyongwa na kamba na kuning'ing'ia katika daraja la shani mjini Morogoro

Hizi ndio zile thread zinazoitia aibu jf? Jamani sio lazima kuanzisha uzi! Unaweza kusoma na kuchangia za wenzio!
Tulijulishwa hapa kwamba Dr Ulimboka alimtambua Msangi akiwa hospitali. Sasa huyo aliyekufa alimshutumu Msangi kuhusu Ulimboka lini, wapi na kwanini?
Naomba mods block hii halafu wapost sababu za kuiblock na aliyeileta apigwe ban. Hiyo ndio itarudisha heshima ya jf!
 
Bi Kongosho taratibu...unantukania baba yangu hapo ujue...
Si kila askari polisi ni muovu tafadhali. Its sad kitendo kilichotokea bt kwangu dots haziingiliaani..lets wait tuone uchunguzi utasemaje.
Najua kwamba samaki mmoja akioza...but hasty generalization is a fallacy..beware.

Kwa kitendo cha wewe kutokuwa police, inaprove baba yako ni kati ya wachache .5% ya police wenye akili; the rest 99.5% ni bogus na huishia kuwarithisha watoto wao upoliccm!
 
Last edited by a moderator:
CCM-MAMA uko wapi mkuu, njoo uone maajabu ya Tanzania. The Hague inawaita watu hivi hivi.
 
Bado ni kitendawili si sahihi kulihusisha jeshi zima inawezekana marehemu kajiua mwenyewe au ameuliwa, tuviachie vyombo vya usalama vifanye uchunguzi wake.

Chama
Gongo la mboto DSM

Unategemea nini katika matokeo ya huo uchunguzi? Polisi ndio wanaotuhumiwa na ndio wanaochunguza! refer issue ya dr Ulimboka
 
Hayahayaaaaaaa wale wa magumashi wale wa magumashi,katika sakata jingine la Msangi,askari aliyemlipua amekutwa AMENYONGWA,Msangi,IGP na SIDE MWEMA mmejivua nguo,Sasa hv hakuna majasusi kabisa ndani ya jeshi,hicho kiti ndio katumia kujinyongea? Hahaaaaa yani alivyopanda na kukipiga pembeni miguu itafika chini na hata kamba haitomgusa shingo hata kidogo!! Haya Tusubiri muvi nzima maana washasema kwamba alikua ana matatizo ya akili wakati niliwahi kumsikia akihojiwa live(Times FM) na aliongoe wazi kwamba yeye sio chizi kabisa!

Jamaa alivyopga kiti miguu ikagusa chnini..then akabonyea kidogo,
 
Jamaa alijigaragaza kwenye vumbi kwanza halafu akajitutinga kwenye mti, this is bongoland!!

na si ajabu alijipiga kwanza,akajing'oa meno na kucha then akajinyonga magoti yakiwa yamejikunja
 
Tanzania bana wacha viongozi wawe kunguru, hapo utakuta huyo anayemfungua ndiyo aliyeutundika mwili baada ya sumu, au kumkaba koo mpaka akafa. Ingekuwa nchi ya sheria hao aliowataja marehemu wangekuwa prime suspects.
 
Hivi ni macho yangu au niko sahihi? naona kama jamaa miguu imegusa chini vile!?
 
Back
Top Bottom