Moro Town: Mji unaoongoza kwa wajanja Tanzania

nilikuwa pale saba saba manzese na wanangu wa kota! na baba yetu butelez mtemi wa enzi hizo hata achimpota anampata vizuri tu nakumbuka wakati tunataka tuzamie india mimi,mwanangu bitebo(marehemu),wa sobibo,side mpare,na juma mtoto wa chamwino tukamshawishi mtoto wa watu wa kihind khan akamwibie baba yake dukan pale amadiya.baada ya kufanikisha dili tukaondoka moro breki ya kwanza arusha huku kichwan tukipanga ishu ya kumtoroka khan na kumwacha soremba dili likatiki nasikia huko moro muind alianzisha mtiti walokuwa karibu na mimi wote walionja mahabusu nasikia boka alifatwa home akabebwa akiwa na kufuli tu manzese ilitikisika sitaisahau moro

hahahaaaaa,mkuu TADPOLE kama nakusoma vilee,manake hao unaowataja wakina bitebo,mpare wote ni wa kitaa changu,umemsahau isihaq sadallah,achimpota mosses kawa bonge la mtu kama mzee mukhi vile
 
na michael mliga alikuwa mzuri kwa basketball sijui kaishia wapi classmate wangu bungo kwa achimpota
Ha haa longtime bungo primary nlisoma enzi za mama msimbe Mwl mkuu....
Ilikuwa raha Siku za mechi na mchikichini.... Alafu mihogo maarufu kwa baunsa pale opposite na morosek

Longtime saaana Moro nakumbuka enzi za kitenga jambazi maarufu.

Jamaa kamsahau yule ombaomba maarufu sijui ndio matonya??? Pale darajani
 
hahahaaaaa,mkuu TADPOLE kama nakusoma vilee,manake hao unaowataja wakina bitebo,mpare wote ni wa kitaa changu,umemsahau isihaq sadallah,achimpota mosses kawa bonge la mtu kama mzee mukhi vile
sadallah bado yupo moro?,achimpota mwalimu huyu bonge la mtu,bute unamjua? said mpare nasikia yupo moro,hashim mdugwa unamjua mkuu!?
 
sadallah si yupo bongo movie sasa,achimpota mwalimu huyu bonge la mtu,bute unamjua? said mpare nasikia yupo moro,hashim mdugwa unamjua mkuu!?

wote nawajua vizuri sana mkuu,side mpare yupo ndugu anakimbiza maisha tu,hashim mdugwa mzee wa hood limited nampata mkuu,unawambuka dumuli,yagilo,hao nao ni watoto maarufu wa kota
 
wote nawajua vizuri sana mkuu,side mpare yupo ndugu anakimbiza maisha tu,hashim mdugwa mzee wa hood limited nampata mkuu,unawambuka dumuli,yagilo,hao nao ni watoto maarufu wa kota
mama yangu unanitajia ndugu zangu kabisa hashim mzee wa hood,dumuli,yagilo wote watoto wa bute hao dah maisha ya kota noma sana
 
mkuu unajua wajanja wanaosumbua dar sasa hv wengi wao wametokea moro,said fella,slim,heri mzozo,dalaz mtoro wa wolper,tevez,kitale,nk sema nashangaa kwa nn huu mji hauendelei??
heri mzozo alikuwaga mtemi enzi zake
 
Naizungumzia zaidi Moro ya kipindi cha nyuma kidogo ya miaka ya 90 hadi 2000 mwanzoni... Hii town ya wajanja , vijana wanaojua kuvaa,wenye exposure, wapenda burudani na utafutaji... Ni mji uliofikia kuitwa jiji kasoro bahari kutokana na upatikanaji wa kila kitu kinachotakiwa... Kulikuwa na shule kubwa mbili Forest Hill na Kigurunyembe ambapo Forest ilikuwa ya watoto wa kishua na Kigurunyembe ilikuwa ya watoto wa kihuni... Mitaa maarufu ilikuwa ya kishua ni Forest, Liti, Sua na Rock garden... Mitaa maarufu ya ushenzini kulikuwa na Mji mpya, Kichangani, Mafiga.

Watu wa Moro ni wapenzi sana wa burudani haswa muziki na soka.... Kulikuwa na timu ya mji maarufu Reli kiboko ya vigogo hii ilikuwa daraja la kwanza alikuwa akija Simba au Yanga atoki.. Hiyo Reli naizugumzia ya kina Duncan Butinini, David Mihambo, Fikiri Magoso, Mohamed Mtono hapo kuna mshangiliaji maarufu sana wa kuitwa Ya mungu ambae ndio shabiki wa kwanza mtanzania kujichora mwilini... Licha ya Reli mtaani kulikuwa na team nyingi sana za mchangani kama chama langu Jamaica, kulikuwa na Black Viba, Small boys, Zaragoza baadae ikawa Moro United, Uruguay, Burkina Fasso, Rhino nk mtaani ilikuwa ni hatari.

Kwenye muziki Moro ina historia ndefu kidogo siwezi kuzungumzia enzi za kina Mbaraka Mwishehe kwa kuwa sikuwepo mimi nilikuwepo enzi za shimoni Morogoro Hotel na Rock Garden na maonyesho ya Forest Hill... Hapa kuna mtu anaitwa Dj Sweet Coffee alikuwa pale mtaa wa Konga ndio alomfundisha Udijei John Dilinga enzi hizo akiitwa John Mkimbizi sababu baba yake alikuwa mkimbizi kambi ya Solomon Mahlangu.. Disco lilikuwa linapigwa shimoni na mara nyingi alikuwa anakuja Dj Joseph Kusaga akimfundisha kazi Dj Peter Moe.

Watu wa Moro najua mpo wengi umu Jf naomba tukumbashane mawili matatu matukio, maujanja na mazuri ya Moro Town.

Moro Town ulikuwa pia mji wa kibabe.. Kulikuwa na watemi wa mji kina Slim mtoto wa sheikh mkuu, Matata, Gamba mcheza judo, vijana wa siafu toka mji mpya nk

Unaikumbuka Miss Morogoro? Unamkumbuka Alex Nictas?

Unawakumbuka mabingwa wa kudansi kitaifa? Kina Askofu, Bob Tigger, Super Ngedere nk

Unakumbuka mashindano ya magari? Unawakumbuka wakimbiza magari maarufu kina Collen, Steve, Pat, Kararambe, Shanto, De Santos nk

Unakumbuka wagiriki na bata zao kwa Mama Perina na Acropol? Unakumbuka masista duu na mabraza meni wa mitaa ya Forest?

Unakumbuka enzi za Mnet inaingia mjini? Moro mji wote ulikuwa na access ya kuona dstv bure.

Unakumbuka heka heka za ligi za mbuzi uwanja wa shujaa, makaburini kilakara na kikundi?

Unakumbuka Fete Fete? Unakumbuka Shan cinema? Unakumbuka swimming pool ya rock garden?

Unamkumbuka Mzee Mkwidu na Patel wakuu wa shule maarufu KG & Forest?

Unamkumbuka Maneno Big G rip? Unamkumbuka Mnambo wauza ngada maarufu?

Unamkumbuka Ndanje jambazi aliyetikisa mji? Unakumbuka ishu yake ya silaha na February Ma rope?

Unamkumbuka toz wa kipindi hicho Puzzo na kundi lake la kurap Watukutu akiwa na Sallam meneja wa Diamond sasa hivi? Unawakumbuka Gangster Family? Unawakumbuka Ze domp?

Unamkumbuka Achimpota? Unaikumbuka bus la Chambo?

Unakumbuka ule upepo uliokuja wa watu kuzamia Sauz na ulaya?

Umeishi mtaa gani Mafisa, Msufini, Kilakara, Ngoto, Kingo, Mlapakoro, Boma road, Sua, Vibandani, Relwe magorofani, Kigurunyembe, Madizini? Au wapi Umeishi?

Kuna watu maarufu wengi sana DSM ambao maujanja yao wamejifunzia Moro Town... Hakika Morogoro ni jiji kasoro bahari.
yaaani ujanja kuvua nguo jukwaani kama Afande sele

Swissme
 
mkuu unajua wajanja wanaosumbua dar sasa hv wengi wao wametokea moro,said fella,slim,heri mzozo,dalaz mtoro wa wolper,tevez,kitale,nk sema nashangaa kwa nn huu mji hauendelei??

Yeah kweli kabisa Sallam wa wcb ni wa Moro

Shamim huyu sasa hivi ni dada wa mjini Dsm kahaso sana pale moro.

Dj JD John Dilinga kwao Manzese pale.

AY kwao rock garden kule.

Maimatha wa Jesse.. Mdogo wake alikuwa mwanangu sana.

Yani wengi wengi sana.

Hivi Rama mtoro na Dallas ni ndugu?
 
sadallah si yupo bongo movie sasa,achimpota mwalimu huyu bonge la mtu,bute unamjua? said mpare nasikia yupo moro,hashim mdugwa unamjua mkuu!?

wote nawajua vizuri sana mkuu,side mpare yupo ndugu anakimbiza maisha tu,hashim mdugwa mzee wa hood limited nampata mkuu,unawambuka dumuli,yagilo,hao nao ni watoto maarufu wa kota,sadallah siyo yule wa bongo muvi,huyu ni mtoto wa mitaa ya kota kule kwa kina sub golikipa wa zamani wa bukina faso,sasa hv anakula ngada kama chid benz
 
Sabu golikipa wa Rhino na Yemen ndio unamzungumzia hapa alisoma Jabar Hilla? Alikuwa anapiga ngumi za hatari alishawai kumng'oa mtu meno kwenye bash rock garden jamaa alikuwa noma.
 
Ha haa longtime bungo primary nlisoma enzi za mama msimbe Mwl mkuu....
Ilikuwa raha Siku za mechi na mchikichini.... Alafu mihogo maarufu kwa baunsa pale opposite na morosek

Longtime saaana Moro nakumbuka enzi za kitenga jambazi maarufu.

Jamaa kamsahau yule ombaomba maarufu sijui ndio matonya??? Pale darajani
Daaaah hiv baunsa sikuiz yupoooh
 
Duu longtime kinona mkuu...
Ila umeisahau Jabar Hiraa kwa mpira wa umiseta ilikua ipo vizuri sana kulikua na jamaa wa kuitwa Pepe Kale na pia Forest kulikua na mshangiliaji wao alikua anaitwa Aideed yule wa kiarabu duu zamani sana!!!
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom