Morning kiss babe Before you go my love!!

UrbanGentleman

JF-Expert Member
Jun 19, 2016
2,584
1,885
Habari za maisha waungwana!? Good!!, kazi na dawa ili tuwe inspired hasa wenye malengo kama niliyojiwekea like 12 years ago

Kichwa cha habari hapo juu ndio ilikua salamu yangu ya kwanza toka kwa mke wangu kipenzi kabla hata sijachukua simu yangu na kujua dunia ina jipya lipi baada ya kuamka.

Wazee juzi member mwenzenu nimechukua jiko rasmi na kupiga teke maisha ya ubachelor rasmi. So hii ndio my first experince ndani ya ndoa tena mbali na mji wa dar es salaam kula honey moon.

Nimesikia wanasema mambo mengi juu ya ndoa ila hii raha ninayoipata my dear wewe kama utakuwa unampiga mkeo nahisi umeoa osama sio mke
Kukosea kupo lakini kujiuliza wapi nilikosea sio jinai ni busara zaidi ili kurekebisha makosa ili kila ukiamka utamani kubaki kifuani kwa mwenzio.

Sisi watoto wakiume tuna kasumba sana haigharimu kitu chochote kuwa romantic kwa wake zetu ukizingatia ndio sehemu ya maisha yetu maisha yote.
Hivi unajisikiaje ukiambiwa kuwa "babe give me a kiss whenever am mad" yani she's read to be ur selvant at any cost bila kujali how hard it is.

Narudia tena ndege wanaofanana ndio huruka pamoja huwezi kuta kunguru akaruka na njiwa hiyo haipo, kunguru atafute kunguru na njiwa atafute njiwa na kama ikitokea wapo angani pamoja hii umaanisha wanapita njia hawatadumu muda mrefu.

Wakuu jitihada ziongezeke kwenye kutafuta zaidi trust me kuna wadada wazuri wanaojiheshimu na kujua hadhi yao katika jamii kama wanawake wanaostahili kilicho bora na sio wababaishaji, sasa kwanini ukose mke bora?

Mi najivunia maamuzi yangu ya kuoa mke bora na mwema of all time i love her madly.
Niwashauri ndugu zangu ma Jr na Sr bachelors kua wanawake wa kuoa wapo pia wakupotezea muda wapo so ni umakini wako

74eaa62803a4a86479c24311164b1e93.jpg


Morning!
 
Dah mkuu kwanza hongera sana, Mungu azidi kumaintain hiyo furaha yenu siku zote. Ni vyema umeanza na positives. Ila sasa mke asichoke ukimaliza hanimuni then stress za kazi halafu dushe isinyae, usidhani kila siku mashine itaitika tu, hapo hanimuni unasimamia kucha kama beberu,nasikia ndoa si tambarare tu kuna ups and downs. Be ready and prepared.
 
Hahahaaaa chekelea dyudyu kudinda kila sekunde uionayo. Chekelea kupata makiss all the time. Huu ni mwanzo, believe or not kuna kipindi utakaa mpaka 3 weeks dyudyu unaifosi ilimame Kwa ajili ya kumsatisfy yeye. Ni mapema sana sana sana kuona umepata wa kufaa. You need to take at least 3-5 years ndio tuanze kujudge. Anyway, hongera sana mkuu
 
Mkuu UrbanGentleman

kwanza hongera sana kwa kuoa yule umpendaye

pili nakupa pongezi kwa kuwa na mawazo chanya kuelekea ndoa yako na kuwa na mepnzi mazito sana juu ya mke wako maanake wanaume wa siku hizi ni janga la dunia

tatu sorry to say this lakini nafikiri ni mapema sana kudeclare unaenjoy maisha ya ndoa ilhali ndo kwanza uko honeymoon mku ndoa ina ups and downs nyingi sana na mara nyingi huanza kukole ndo ikiwa ina muda kidogo,japo sikuvunji moyo nakueleza tu hali halisi ukae na jambo hili kichwani

ila yote kwa yote ndoa kuwa nzuri au mbaya inategemea na ninyi wenyewe,furaha ya ndoa yenu iko mikononi mwenu wenyewe kila la kheri mkuu.
 
Utansame mkuu sikuweza kusoma mpaka mwisho because iko vere boring,.. Sorry tho,ahsante
 
Hongera sana jamani
Hatimae ametokea wa kuisifia ndoa, ingawa ni changa usiruhusu mawazo hasi kwenye akili yako.
Mwanamke akipendwa anapendeka, jenga uaminifu kwa mkeo ndio nguzo. Usichoke kumwambia jinsi unavyompenda, na msali pia...

Ndoa yenye amani na furaha mtu huitegeneza mwenyewe na kweli mkuu ndege wafananao huruka pamoja!!!
 
Hongera sana jamani
Hatimae ametokea wa kuisifia ndoa, ingawa ni changa usiruhusu mawazo hasi kwenye akili yako.
Mwanamke akipendwa anapendeka, jenga uaminifu kwa mkeo ndio nguzo. Usichoke kumwambia jinsi unavyompenda, na msali pia...

Ndoa yenye amani na furaha mtu huitegeneza mwenyewe na kweli mkuu ndege wafananao huruka pamoja!!!
Thank you thanks alot
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom