More Money, More Problems - Ushindi wa Bilion 50 ulivyosababisha kifo chake

Nafaka

JF-Expert Member
Feb 17, 2015
6,166
2,000
Ulishawahi kusikia ule msemo wa More money more problems? Hebu fikiria iwapo unashinda bahati nasibu ya $20 million (kama billion 50 za kibongo)! Shida zako zote unahisi zimekwisha, huhitaji kuajiliwa, huwezi kuwaza kuhusu bills, maana ni pesa ndefu sana. Lakini muda mwingine unapopata pesa nyingi ndiyo mwanzo wa matatizo yako na huenda ikawa tiketi yako ya kukuondoa Duniani.

Na hiki ndicho kilimpata Jeffrey Dampier, Muamerika Mweusi aliyeshinda kitia cha Dollar milioni 20 katika bahati nasibu. Jeffrey Dampier aliposhinda Bahati nasibu, alifurahi akidhani sasa ametimiza ndoto yake ya kuwa na maisha bora. Masikini kumbe hakujua kuwa, kuna mtu ambaye atachukua kila kitu kutoka kwake.

jofre.jpg

Jeffrey Dampier alikuwa mtu wa kawaida tu. Alizaliwa na kukulia Chicago huku akifanya shughuli ya ulinzi. Mwaka 1996, Dampier alishinda kiasi kikubwa cha pesa, $20 Million kwenya bahati nasibu ya Jimbo la Illinois. Dampier aligeuka kuwa milionea ndani ya usiku mmoja, maisha yake na ya familia yake yalibadilika kabisa.

Dampier alikuwa kaoa na ana mtoto mmoja wa kike. Alinunua jumba kubwa, gari za kifahari, kwa ajili yake na familia yake. Alianza kuva vito vya thamani, yeye na mke wake walikuwa wanatoka kwenye mitoko katika migahawa na mahoteli ya kifahari. Pesa uleta marafiki pia, na hivyo wapambe nao hawakuwa nyuma kumfuata fuata ili wapate kufaidi ukwasi wake.

Pia pesa huwavutia sana wanawake, mwanaume akipata pesa hata akiwa na uso wa mbuzi ataitwa handsome na pisi kali zote. Kwani umesahau mwanamuziki maarufu almasi almaarufu kama Diamond alivyoimba kwenye Remix ya Fresh kuwa "Wakati sijawa maarufu waliniita domo, sasa eti nimekuwa maarufu wanasema nina lips denda".

Na hili ndilo lilitokea kwa huyu Bwana Dampier. Mademu kama wote wanamtaka. Kuanzia wale waliomkataa zamani hadi wale ambao alikuwa anawaona siyo level zake. Kwakweli inahitaji uwe na moyo mgumu kushinda majaribu kama haya. Mwisho jamaa akashindwa kukaza akaanza kutoka na binti mkali kuliko mke wake. Huyu pisi kali anajulikana kama Crystal Jackson. Kusema kweli namlaumu nusu maana wakati akiwa mlinzi alioa mke ambaye alikuwa ana uso wa baba yake, kwakuwa huyo ndiye aliweza kummudu.

Baadae yeye na mkewe walipeana taraka, wakagawana kila kitu 50/50 kuanzia mali mpaka pesa iliyokuwa wenye akaunti ya benki. Ila jamaa alikuwa ana roho safi kabisa, angekuwa mimi taraka ningempa na nyumba moja na gari moja na milioni kumi, nusu kwa nusu siwezi kukubari. Dampier akamuoa huyo kimwana mpya. Kisha yeye na mkewe mpya wakahamisha makazi yao katika mji wa Tampa Bay huko Florida. Huko Florida Dampier alifungua kiduka chake kidogo alichokuwa akiuza Popcorn.

Kupenda ni hatari sana, yani ukimpenda mtu halafu ukawa unapesa unaweza mnunulia hata ikulu au hata ukamhonga Ukuu wa Mkoa. Damper kwa mapenzi aliyokuwa nayo kwa Jackson alikuwa akihakikisha anampa kila kitu. Pia alikuwa akihudumia familia ya Jackson kwa kila kitu. Alikuwa ana tabia ya kuwapeleka matembezi kwenye meli za kifahari na kuwamwagia zawadi.

Mdogo wake Jackson wa kike kuna kipindi alikuwa anapitia maisha magumu, Dampier aaamua kumsaidia kwa kuhakikisha anamlipia kila kitu. Lakini ukweli ni kwamba msaada hakuwa anautoa bure eti kisa ni shemeji yake. Unajua sisi wanaume hata upange wanawake 1000, uniambie nichague mmoja ninayemwona mkali niondoke naye, nitachagua ila roho bado itaniuma kwa wale 999 nilioyowaacha nyuma. Basi kumbe Bwana Dampier alikuwa anamtafuna shemeji yake huyo aliiyejulikana ama Victoria Jackson.

victoria-jackson-lover.jpg

Victoria alikuwa ana mahusianao na kijana mwingine aliyekuwa anajulikana kama Nathaniel Jackson (hawakuwa na uhusiano jina la Jackson wamefanana tu). Nathaniel alikuwa anafahamu kuwa Dampier ana ukwasi mkubwa, hivyo akaja na mkakati kabambe wa kupata pesa kutoka kwa Dampier iwapo Victoria angekubali kumsaidia kutimiza mpango huo.

Kutokana na maelezo ya Victoria anadai ya kwamba, alienda kumwona Nathaniel nyumbani kwake tarehe 26 mwezi wa saba. Nathaniel akamwambi a Victoria ampigie simu Dampier na kumwambia aje pale nyumbani. Victoria alimwongopea Dampier kuwa alikuwa na tatizo gari lake limegoma kuwaka. Dampier kusikia mpenzi wake ana tatizo bila kupoteza muda akaenda. Alipofika pale, Nathaniel akamteka kwa bunduki ya shotgun na kumlazimisha aingie kwenye gari.

Hawa wawili walimfunga Dampier mikono yake kwa nyumba kwa kutumia kamba za viatu. Kisha Victoria alienda gari huku Nathaniel akiwa anampiga Dampier kwa kutumia kitako cha bunduki akimtaka Dampier ampatie pesa. Dampier alikuwa ana roho ngumu kama kunguni, na kipigo chote alichoshushiwa bado aligoma kutoa hata sumni. Nathaniel na Victoria walibadilisha muda mwingine Nathaniel aliendesha gari huku Victoria akijaribu kumshawishi shemeji ya atoe pesa.

Ilifika mahali ambapo nathaniel alimkabidhi bunduki Victoria akamwambia amtandike risasi Dampier. Alimwambia ampige risasi kama hatofanya hivyo atamandika yeye. Yani ua ama uuawe. Victoria aliamua kumtandika Dampier risasi moja iliyopenya kwenye utosi na kumuua mara moja.

Baada ya kutekeleza unyama huo, wawili hawa waliendesha gari na kulitelekeza kwenye barabara isiyokuwa na vurugu nyingi wakakimbia na kuacha mwii wa marehemu ukiwa ndani. Haikuchukua muda polisi kugundua mwili huo, na hao wawili walikamatwa siku kadhaa mbeleni.

Wakati wa kusikilizwa kwa kesi ilidaiwa na upande wa utetesi kwamba Nathaniel alimlazimisha Victoria kumuua Dampier. Ila upande wa mashitaka ulipinga hoja hiyo wa kudai kwamba alipompigia simu akimdanganya ili aje pale alijua nini ambacho kingefuata.

Wote wawili walihukumiwa kifungo cha maisha ambapo wanakitumikia mpaka leo.

More money more problems, but it is better to cry while sitting in a Benz!
 

johnman

JF-Expert Member
Jun 10, 2017
818
1,000
Tatizo kadri unavyo pata pesa nyingi ndivyo matumizi nayo yanakuwa mengi, hapo atataka uendeshe magari mazuri ambapo matunzo yake ni gharama, utataka ukae kwenye jumba la kifahari/hoteli ambapo kodi yake si ya kitoto, utataka kula misosi ya gharama n.k, sasa kama umeshindwa kuzalisha hizo pesa kifidia matumizi yako hapo baada ya muda mfipi sana ni lazma uwe kapuku tuu.
 

jkipaji

JF-Expert Member
Sep 22, 2019
2,008
2,000
Huyu jamaa anahitaji viboko vingi tuu anapata pesa alafu anakuwa bwege bwege, mimi nilipataga pesa nyingi tuu vidada vikaanza kuniita handsome nilikuwa navikamata na kuviweka viboko vya nguvu, sipendagi ujinga kabisa mbele ya pesa
Siku zote usiombe kupata pesa peke yake,omba na maarifa ya kuzimudu hizo pesa, kabla hazijakumudu wwe!
 

Nafaka

JF-Expert Member
Feb 17, 2015
6,166
2,000
Story ndio imeisha au?
Soma tena nmeimaliza mkuu, tatizo mimi uwa naandika moja kwa moja hapa hapa jf na uwa sirudii kusoma ndo maana unaona kuna grammatial error nyingi, nikiandika ikafika urefu flani napost halafu anendelea kuandika hapo hapo huenda wewe ulisoma nilipopost mara ya kwanza rudia kusoma.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom