MWEZI KAMILI (FULL Moon
MATAMBIKO:
1. Ndani ya saa 24 siku nzima ya full moon nikiwa na maana kwamba hakikisha kwamba siku nzima hiyo hugombani na mtu kwa sababu ya kutoathiri nguvu za full moon unaweza kuhisi mvurugano, hasira na mengineyo kwa kuwa full moon itaingia kwenye nyota ya Mshale kwa hiyo kwa kadri unavyoweza jitahidi usigombane na mtu ili kubaki na nishati (energy) nzuri.
2. Njia ya kuandika (journaling), chukua karatasi na peni fanya kama full moon iliyopita andika yale mabaya yote ambayo unataka kuyaachilia yaende kutoka maishani mwako. Mfano mimi Bakari naachilia hiki na hiki utataja hapo mwenyewe hicho unachotaka kuachilia iwe mtu au kitu ambacho hakina faida tena kwako kinachomaliza nguvu zako, kutokupewa kipaumbele na watu, kubebeshwa mizigo isiyo yangu, kurudishiwa nyuma kimaisha, kukatishwa tamaa, hofu, wasiwasi, chuki, wivu n.k yaani andika yote ambayo hayafai kwako, kila kinachokukosesha raha kiandike katika karatasi na kama unaona utasahau basi andika naachilia mambo yote mabaya nayoyajua na nisiyoyajua, niliyonenewa, yaani kutamkiwa n.k.
3.Njia ya tatu chukua mshumaa wa blue kama huna tumia mweupe maana mweupe unatumika kwa kila kitu, chukua karatas uliyoandika mambo yote ambayo huyataki ichome, ukishindwa sababu ya mazingira yako basi chana na amini Kwa kufanya hivyo ndivyo hayo mambo yanavyoondoka katika maisha yako. Usiache kutaja jina la Mwenyezi MUNGU akusaidie.
4. Njia ya tatu ni catalyst , popote ulipo chukua chumvi ya mawe + mchai chai ila kama mchai chai huna basi tumia chumvi pekee, chemsha maji kisha ipua weka katika ndoo, oga popote utapoona panafaa, chukua madonge ya chumvi ya mawe weka katika hayo maji hadi iyeyuke. Yakishapoa oga hayo maji usisahau kunuia Kwa Iman na pind unaoga vuta hisia kwamba mambo yote mabaya ndivyo yanavyoondoka katika maisha yako.
5. Njia ya tano ambayo sio lazima ila mimi huwa naitumia sana na inanisaidia sana kaa au simama huku ukiwa unauangalia mwezi ,mwanga wake ukiwa unakumilika jiunganishe na huo mwezi kwa kuongea/ nena/ tamka/ fanya uumbaji .ongea nao kama vile unakusikia, tengeneza story juu ya kitu unachotaka mfano ewe full moon mimi fulani kama jinsi mwanga wako unavyonimulika bas naomb ukamulike kila eneo katika maisha yangu n.k
6. Njia nyingine, chukua maji kwenye glasi yaanike kwenye huo mwanga wa mwezi yaani hakikisha mwanga wa mwezi unaingia ndani ya hiyo glasi yako yenye maji, iache hapo kwa muda wa masaa 6 ikitokea umelala hamna shida asubuhi utachukua maji yako utayanuia kwa kuongelea ndani ya maji yote unayoyataka maishani mwako kisha utakunywa hayo maji huku ukiwa na imani kuwa umefanikiwa.
6. BAADA YA HAYO YOTE ,KATIKA KILA HATUA SHUKURU MUNGU mfano Asante MUNGU Kwa kuwa nmeachilia kitu flan na flan YAN SHUKURU KAMA VILE TAYAR VIMEONDOLEWA KATIKA MAISHA YAKO.
AMIN NA ACHILIA USIJARIBU KUFANYA KAZI YA ASILI (NATURE), WEWE SHUKURU TU NATURE KWA KUWA KILA ULICHOKINENA KIMETOKEA ,KILA ULICHOKITOA KIMEONDOKA YAANI SHUKURU. KUNA NGUVU KUBWA SANA KATI YA NATURE NA SHUKRAN.
Utachagua njia inayokufaa iliyonyepesi kwako kati ya hizo
NB::nimeitoa sehemu itawasaidia wale ambao hawana idea hat kidogo kuhusu hiyo full moon