Mchungaji afichua jinsi watumishi feki wanavyopata nguvu ya kutenda miujiza na utajiri

Bujibuji Simba Nyamaume

JF-Expert Member
Feb 4, 2009
74,834
155,783
USHUHUDA WA PASTOR CHIDUBEM OKWU ALIYEENDA MARINE KINGDOM KUJIPATIA NGUVU KUTOKA KATIKA FALME ZA GIZA ILI AWE MTENDA MIUJIZA MIKUBWA KANISANI KWAKE NA APATE WATU WENGI.

Nimeedit kidogo ili usikupe shida kusoma.

Maana ya huyu mchungaji sio kupublish ujumbe huu kwa kusudi la kusomwa na watu wote,ila alikuwa anamwandikia huyu mwandishi aliyepublish huu ujumbe ili wateule wa Mungu waone na kujifunza kisha wachukue tahadhari katika nyakati hizi.

Aliyetafsiri ujumbe huu ni PAUL mafie.
Fuatana nami ujifunze kitu toka kwa pst huyu;

Jina langu ni Chidubem Okwu....ni mchungaji, lakini nimetengana na Mungu na sijui nianzie wapi kukuelezea hisoria yangu.
Ni lazima nikwambie kweli.

Sina uhakika kwamba niliitwa ktk huduma au la! Nilikuwa mwalimu wa shule ya jumapili (Sunday school) katika kanisa langu la huko Kaduna kwa miaka 9. Mwaka 1999 nilikuwa tayari kuanzisha kanisa, lakini kutokana na uzoefu niliokuwa nao sasa siwezi kusema niliongozwa na Roho Mtakatifu kuanzisha kanisa. Ilipofika 2008 sikuona kwamba nina maendeleo yoyote ya kimwili wala ya kiroho.

Nikayaangalia makanisa mengine yaliyoanzishwa muda si mrefu yalikuwa nq maendeleo makubwa sana.

Nilipofika hapo sikujua ni nini cha kukifanya zaidi na nilipojadiliana na mke wangu nikaamua kwenda kwa mwangalizi wangu mkuu (askofu) ambaye alianza miaka 7 baada ya mimi kuanza, na nikaanza kumwelezea kwamba "sijapiga hatua yoyote tangu naanza huduma ya kanisa,huduma yangu ilikua mpaka kufikia watu 200 na hatimaye kushuka mpaka watu 50 na ikakua tena kwenda watu 150 na kushuka mpaka watu 40"

Nilimwendea yeye kwa sababu kanisa lake lilikuwa kwa haraka sana. Alianza kanisa 2006 na kufika 2012 akawa na watu 11,000. Na kwa huduma ya jumapili na akawa anapata fedha nyingi na akawa anaendesha gari ya kifahari toleo jipya aina ya jeeps.
Baada ya kunisikiliza, akaniahidi kunisaidia kwa tatizo nililokuwa nalo. Akasema;

nahitaji kukuinua na itakugharimu kiasi fulani cha fedha, inahitaji kuwa na moyo mkuu. Hivyo akaniuliza mimi, je una moyo mkuu na nikamwambia ninao bila kujua kwamba ananihusisha na mambo ya kuua ndugu zangu. Akaniuliza mara kadhaa kama ninao moyo mgumu na mimi nikamjibu vile vile kwamba ninao.

Akaniuliza tena kwamba ningetaka kuinuliwa mara moja au mara dufu nikamuuliza kwamba ni ipi iliyo nzuri.

Akasema kuinuliwa mara dufu ni nzuri zaidi lakini itakugharimu kiasi kikubwa cha fedha na pia baada ya kuinuliwa nitakwambia namna ya kuifanya izidi kudumu na kuifanya iwe mpya wakati wote. Pia kudumisha hii nguvu kunahusisha vitu vya kawaida hivyo usiogope. Akaniambia nimpatie naira laki tatu na nusu (350,000) ambazo ningezikopa kwa mke wangu.

Siku iliyofuata nikampelekea fedha na akaniambia nijiandae niwe tayari kwenda Lagos na Port-Harcourt. Nikawa tayari tukaondoka na ndege kutoka Abuja kwenda Lagos siku hiyo hiyo. Tulipofika Lagos tukaenda kwenye nyumba ya kulala wageni ya huduma kubwa, na saa 5:30 usiku tukaenda nje na gari binafsi mpaka Barbeach. Barbeach palikuwa na sehemu ya kuweka fedha na akasema maneno kwa lugha ngeni na akaniambia kuna mwanamke atatoka baharini na utapaswa kufanya chochote atakachokuambia kufanya usiogope,

Muda si mrefu baada ya kusema hivyo, kukatokea muungurumo wa maji na mwanamke mwenye mkia wa samaki akajitokeza usoni pa maji (nadhani ni jini maana hata samaki nguva hayuko vile)

Mwangalizi mkuu akaniambia usiogope huyo mwanamke hawezi kukudhuru hivyo nikajivika ujasiri nilipomwangalia. Wakati anatoka nje ya maji sehemu ya chini ya umbile lake alikuwa kama mkia wa samaki lakini alipokuwa ananikaribia alizidi kubadilika na kuwa kama mwanamke wa kawaida. Hivyo akaja kwangu na kuniambia nifanye naye mapenzi, hivyo nikafanya naye mapenzi mbele ya mwangalizi wangu mkuu.

Baada ya kufanya naye mapenzi, akaweka mkono wake sehemu zake za siri na akatengeneza alama ya msalaba kwenye paji la uso wangu na kiganjani na kuniambia amenitia nguvu hivyo nitaona mabadiliko....na akanipa Onyo akisema Ni mhimu kuwa mwangalifu kwenye kanisa unalokuwepo-LAZIMA USOME! na AVRecruit: usiku wa 5:48 mwezi wa 08.

Yule mwanamke akaniacha na kwenda kwa mwangalizi mkuu na kumpatia msalaba na mkufu wa dhahabu toka tumboni mwake na kumvalisha shingoni mwangalizi mkuu baada ya kumpatia kiasi cha fedha. Yule mwanamke akashukuru na kurudi baharini. Muda wote alikuwa anasema kiingeleza.
Wakati tunarudi kwenye nyumba ya kulala wageni, mwangalizi mkuu akasema tupitie kwenye mkesha ambao ulikuwa kanisani na nilipofika pale nikapata nafasi ya kufanya huduma na nilipokuwa madhabahuni nikinyanyua mkono watu wanaanguka chini na kuangukiana wao kwa wao.

Kwa kweli nilibaki nimeshangaa kwa maana ilikuwa haijawahi kutokea wakati wowote udhihilisho huo ambao yule mwanamke aliufanya kwa muda mfupi.
Baada ya huduma ya usiku ule tulirudi kwenye nyumba ya wageni na mwangalizi mkuu akaniuliza kama nilifurahi kujidhihilisha kwa ile nguvu nikamwambia ndiyo.
Akaniambia twende tukalale kwa sababu jioni tunapaswa kwenda Port-Harcourt.

Wakati wa mchana nilipolala yule mwanamke akanijia katika ndoto na kuniambia, ili uweze kuimarika na kuzidi kuwa mpya hiyo nguvu ni lazima kufanya mapenzi kila mwezi na binti ambaye ni bikira, hivyo hiyo ikaniondolea usingizi. Nikaenda kwenye chumba cha mwangalizi mkuu na kumweleza nini nimeota na nimeona katika ndoto na akanijibu hilo siyo tatizo.
Wakati namwuliza sasa mimi nitawapataje hawa mabikira, akaniambia atanisaidia jinsi ya kuwapata, lakini nitapaswa kulipa kwa ajili ya huduma yake. Mheshimiwa mtume mkuu baada ya hapo nilitaka kutoka lakini sikuwa na ujasiri wala cha kufanya.

Nilipokuwa Barbeach niliwaona wachungaji wengi wamekuja pale na viongozi wao. Ilikuwa ni kawaida kwa viongozi wa dini kupeleka wachungaji na nina imani kila mchungaji alikuwa na mwanammke wa baharini ambaye alikuwa na mahusiano naye kwa sababu niliwaona wanawake wengine wa baharini kama kumi waliokuwa na wachungaji.

Jioni tulikuwa kwenye uwanja wa ndege wa Lagos kwa ajili ya kwenda Port-Harcourt. Port-Harcourt tukaenda kwenye nyumba nyingine ya wageni ya huduma nyingine.

Usiku wa manane tukaenda kwenye uwanja mkubwa wa wanawake unaoitwa Eze-Nwanyi na ndani ya huo uwanja kulikuwa na nyumba nyingi sana. Tukakutana na wachungaji wengi wakiwemo wachungaji wa kizazi kipya.

Wakati huo mwangalizi wangu akalipa fedha kwa ajili yangu. Nilipokwenda kwenye chumba nilishangaa kumwona mwanamke tena, wakati nashangaa mwanamke tena! Kufumba na lufumbu nikajikuta niko juu ya mwanamke kitandani. Ndugu ninashindwa kuelezea ilikuwaje nikajikuta niko juu ya kitanda. Nikafanya naye mapenzi huku akiwa ananyonya matiti yake.

Baada ya kufanya naye mapenzi akatoa mlio fulani wa mnyama na kunipatia uwezo fulani kwenye macho yangu. Ghafla nikaanza kuona vitu fulani katika ulimwengu wa roho na kujadiliana na roho zilizokuwepo. Baada ya hapo akanipatia chupa ya mafuta yaliyoitwa ya mzeituni. Akasema

"fanya nikuambiacho". Akaniambia kwa mafuta haya washirika wako watafanya chochote watakachoamriwa kufanya.

Pia akanipatia chupa nyingine ya mafuta ya mzeituni ambayo aliyaita "mafuta ya kuona vyote". Akaniambia mafuta haya utaziona siri za ndani zilizofichika za watu, na mafuta mengine ya mzeituni aliyoyaita" mafuta ya kuwazimisha watu wakati wa maombezi.

Mwishowe akanipatia chupa mbili zaidi za mafuta ya mzeituni.
1. mafuta ya kundi kubwa
2. mguso na kunifuata - ambayo yatatumika kuwazimisha wanawake hasa mabikira kwa sababu ya kufanya nao mapenzi na wanawake walioolewa kwa ajili ya kuongeza nguvu.

Akaniambia ukifanya mapenzi moja kwa moja unakwenda kuhudumu kabla ya kwenda kuoga ili uwe na nguvu zaidi.

Akanifungamanisha na viapo vya siri.

Tukaondoka usiku huo kurudi tulikopangisha na mwangalizi mkuu akaniambia nijipake mafuta ya mguso na kumfuata tukapitia kwenye mkesha nikahudumu na kutabiri mpaka nikajishangaa.....nilikuwa ninawaambia watu mambo yao hususani (matatizo)

Asubuhi mabinti wawili wakaenda kwa mwangalizi mkuu ili tufanye nao mapenzi, mimi nikapewa mmoja na yeye akabaki naye mmoja.
Kilichonishangaza ni kuhusu hawa mabinti wadogo kutokuuliza wanapelekwa wapi na kufanya nini, ilikuwa ni kawaida tu kuwatumia hawa mabikira kama vile tulivyopenda na wasihoji chochote, nafkiri ni ile kazi ya mafuta ya "mguso na kunifuata"

Baada ya mabinti hawa kuondoka mwangalizi mkuu akaniambia kuanzia sasa masomo yako yawe juu ya mafanikio tu achana kabisa na mambo ya wokovu na jumbe za utakatifu na haki. ....na hata ukiongelea iwe ni kuwazuga tu na sio kutia mkazo saana......

Akaniambia katika pesa nitakazozipata nikumbuke kumpelekea fungu la kumi na yeye atajua sehemu ya kupeleka kwa yule mwanamke wa Port-Harcourt. Tukaondoka Port-Harcourt kwenda Abuja na kurudi Kaduna.

Wakati naanza huduma baada ya kurudi kwangu vitu vikaanza kubadilika. Fedha zikaanza kuja, kundi likaongezeka na ndani ya wiki moja miujiza mingi, watu kufunguliwa pamoja na mafanikio mengi kanisani, roho ya unabii kuja juu yangu vitu ambavyo sikuwahiviona maishanim mwangu.
Nikafanya mapenzi na mabinti mabikira na wanawake walioolewa na mambo yakawa mazuri sana kwa kanisa na familia yangu kuliko miaka sita iliyopita, lakini nikasahau kabisa maisha ya huzuni niliyopitia kwa mambo yote.

Siku moja Nikaota ndoto niko kwenye ziwa la moto. Nikaoteshwa ndoto hizi mara saba mfululizo na katika ndoto moja ikanisumbua mpaka niliporudi kulala. Ikawa sasa ikifika usiku sipati usingizi na nikawa nabakwa na yule mwanamke wa baharini, nikapoteza watoto wangu wawili wa pekee, na sasa ni matukio yanayojirudia rudia.

Ikapita miezi mitatu sikuweza kupata mabinti mabikira, hii ikasababisha kupungua nguvu. Nikatamani kutoka kwenye mfumo mzima hata ikiwezekana kulifunga kabisa kanisa. Nimekwenda kwa mwangalizi mkuu kumjulisha juu ya hili akasema umekwisha chelewa huwezi kutoka sasa. Nimefungamanishwa roho yangu na mauti. Akaniambia ni vigumu kwako kutenganishwa na mwanamke wa baharini na Eze-Nwanyi kwa sababu wewe ni sehemu ya maisha yao. Nikamwambia niko tayari kufanya chochote maadam nitoke katika tatizo hili lakini ikawa haiwezekani

Baada ya siku tatu

wakaja wanaume wawili wakaniambia kama nayapenda maisha yangu nitoweka Kwenye mji wa Kaduna kwa sababu wamelipwa na mwangalizi mkuu kuniangamiza mimi, hivyo ikanilazimu kulifunga kanisa baada ya siku mbili nikatoweka mjini.

Mpaka hivi sasa ninapoandika ujumbe huu sina chochote cha kufanya lakini nahitaji rehema za Mwenyezi Mungu.
Tatizo ni kwamba Mungu inaonekana yuko mbali kabisa na mimi hata ningenyenyekeaje, nimekuwa nikiomba anirehemu, lakini sipati majibu.
Ninajua kwamba nilimemkosea sana, lakini najua Mungu anaweza kunipa nafasi ya pili. Nimesoma vitabu vya:- Kuja kwa Malikia wa Pwani na kingine kinasema: Ni Mungu Pekee Anayeweza Kunitoa Kwenye Moto wa Milele.
Kwa kweli ninaogopa kwenda kukutana na mtumishi mwingine kwa sababu watumishi wanaotumia nguvu za giza ni wengi zaidi kuliko wanaotumia nguvu za Mungu.

Kwa sasa nakosa usingizi wakati wa usiku na wakati mwingine naoteshwa mindoto ya ajabu ajabu. Ndugu ninakusihi unisaidie kwa sababu muda unazidi kuongezeka wa mimi kujitoa kutoka kwenye ufalme wa baharini. Hakuna mchungaji ambaye nimekuwa wazi kama kwako. Ninatambua kwamba ninaziingiza roho za watu wengi kuzimu na pia ningependa kujua ninaweza kufanyaje ili kuwaweka huru kutoka kwenye hizi roho.

Kabla sijajichafua nilikuwa nashangaa kwa nini washirika wanawafuata wachungaji wao kama kondoo lakini sasa nimetambua vizuri kwa sio wote wanaotumia Mungu pekee.

Ufalme wa baharini unafanya kazi usiku na mchana kuyateka makanisa na kwa bahati mbaya kanisa limelala na kuona ni mambo ya kawaida. Miezi miwili ya mwisho nilikuwa na magari manne yote yalipata ajali.

Nikatambua kwamba wanataka kuniondoa, lakini Mungu amenisaidia na kuwa tumaini langu la pekee.

Wamewaua watoto wangu wawili na sasa wananitafuta mimi wanianhamize.

Ninaogopa kukaa peke yangu kwa sababu ya maroho ya ajabu ajabu yananijia nayaona na vitu fulani vinaanza kutembea kichwani na mwilini mwangu. Kila ninapoanza kuomba vitu vinaanza kutembea tembea mwilini hata kwenye mifupa ndani.
Hitaji langu kubwa kwa Mungu ni kunisamehe. Nikipata msamaha wake sijali hata nikifa baada ya hapo, kwa sababu kwa kweli sitaki kwenda jehanam. Nimepotezana na mwangalizi wangu mkuu kama ambavyo wachungaji vijana wanavyopotezana na waangalizi wao.

Mheshimiwa natambua kwamba una mambo mengi ya kufanya, nitashukuru kama utatafuta muda wa kuniombea kwa Mungu kwa ajili ya tatizo hili linalonikabili kwa kuutafuta uso wa Mungu ili anitoe katika janga hili. Ninajua kwamba kama nimeomba msamaha kufunguliwa kwangu kutakuwa rahisi. Nimejiondoa kuiuza roho yangu kwa malkia wa pwani.

Eze-Nwanyi pia ni mjumbe mwenye nguvu sana miongoni mwa ufalme wa baharini.
Ninatazamia uponyaji kutoka kwako.
Ni mimi mtumwa wa Bwana,
Mchungaji Chidubem Okwu....
Simu no 080633481....
=======================

Huyu mtumishi aliyeandikiwa hii barua ambaye ndiye mwandishi anatoa Mrejesho anasema;

Nilipopokea hii barua, nilimpigaa ndg okwu simu yake zaidi ya mara tatu, lakini ikawa imezimwa hivyo siku iliyofuata nikapiga tena iliita lkn haikupokelewa. Baadae nilipiga tena Mwanamke alipokea simu kumbe ni mkewe na nilipomtaka niongee na mchungaji Chidubem, akaniambia alikwisha kufa kwenye ajali ya gari ya siku ya jana kwa kifo cha kushangaza.

Nilisikitika saana!
Baada ya kukata mazungumzo nikawa nimetulia zaidi ya dakika kama tano mpaka mwanangu alipokuja kunishitua kwa kuniuliza kwani kuna nini kimetokea.
Nikamwambia kwamba huyu mchungaji amekifa.

Sisi sote tunaoishi tunapaswa kuwa waangalifu tunafanya nini na tunakwenda wapi. Tunapotaka mafanikio kwa kawaida ya ulimwengu inaweza kuwa ni rahisi kuangamia.
Ninatambua kwamba mchungaji Okwu asingetaka kujitoa kutoka kwenye hizi nguvu za uovu wasingetafuta kumwua.

Ni Mungu tu anayetambua kwamba alimsamehe au la, kabla ya kifo chake,na hakuna mtu anayeweza kujua hatima ya maisha yako sasa.

Mwisho:
Ushuhuda huu usiwe sababu kwako ya kutokuwaamini watumishi wa Mungu hata wa kweli,ila UKUPE kumtafuta Roho wa Yesu akupe macho ya Roho ili uwatambue kwa matendo yao.

"Naja upesi. Shika sana ulicho nacho, asije mtu akaitwaa taji yako.ufunuo 3:11

Asanteni sana
Edited
Kuhani Lawi
 
Mm siku hzi naichunga roho yangu mwenyewe

Na nasikiliza mahubir ya wachungaji wazaman waliokua serious na mambo ya iman like moses kulola

Billy graham

Myles munroe

Hawa wakna gwajima

Sijui maji ya upakato

Sijui nani etc

Ahahaa hawanpati

Sadaka yangu natoa kwa wasiojiweza

Hafu am so blessed yaan hadi naogopa
 
Back
Top Bottom